Ofisa
Mkuu wa masoko na Mahusiano wa Vodacom Tanzania Mwamvita Makamba na
Kaimu Mkuu wa kitengo cha Mahusiano wa Vodacom Rukia
Mtingwa,wakimsikiliza jambo kwa umakini mmoja wa wanawake alietibiwa
ugonjwa wa fistula katika hospitali ya CCBRT Stella Nzyemba,mara baada
ya uzinduzi wa kampeni ya MOYO inayolenga kuhamasisha jamii kuchangia
fedha kwa ajili ya kusaidia wanawake wenye matatizo ya ugonjwa huo hapa
nchini, Kwa kuchangia kwa njia ya M-PESA tafadhali tuma kwenda namba
200500,na kwa njia ya SMS tuma ujumbe usemao mfupi MOYO kwenda namba
15599.
Baadhi
ya akina mama wanaotibiwa ugonjwa wa Fistula katika Hospitali ya
CCBR,Dar es Salaam.wakiimba wakati wa uzinduzi wa kampeni ya MOYO
inayolenga kuhamasisha jamii kuchangia fedha kwa ajili ya kusaidia
wanawake wenye matatizo ya ugonjwa huo.Kwa kuchangia kwa njia ya M-PESA
tafadhali tuma kwenda namba 200500,na kwa njia ya SMS tuma ujumbe mfupi
usemao MOYO kwenda namba 15599.
Thamani ya
mwana aijuae mzazi, Wote tumezaliwa na hivyo wote ni watoto. Zaidi ya
wanawake 3,000 nchini hupatwa na tatizo la Fistula kila mwaka, Hii
hutokea wakati wanapojifungua.
Fistula husababishwa na uchungu wa muda mrefu wakati wa kujifungua baada
ya mzazi kutopatiwa huduma kwa muda muafaka kutokana na upungufu au
kutokuwapo kwa vifaa vya afya. Hatimae mwanamke hupoteza kichanga chake
na pia kujikuta katika hali ngumu ya kupoteza udhibiti wa haja kubwa na
ndogo na hivyo kumtoka kwa mfululizo.
Vodacom Tanzania kwa kushirikiana na CCBRT mnamo Februari 5, mwaka huu
ilizindua kampeni ya umma MOYO inayolenga kuchangisha fedha kiasi cha
Sh. Bilioni Moja kugharamia ujenzi wa Hospitali maalum ya afya ya uzazi
na matibabu ya bila malipo kwa wanawake wanaosumbuliwa na ugonjwa wa
Fistula nchini.
"Ugonjwa huu unawatesa mama zetu na dada zetu hasa wanaoishi katika
mazingira duni, unawakosesha raha/amani unawasababishia unyonge wa
maisha na upweke hata kunyanyapaliwa, kukimbiwa na waume ambapo ni
miongoni mwa athari kadhaa za kisaikolojia.alisema"Ofisa Mkuu wa Masoko
na Mahusiano wa Vodacom Bi. Mwamvita Makamba.
Vodacom tangu mwaka 2010 imekuwa ikisihirikiana na Hospitali ya CCBRT
katika program ya kuwapatia fedha wanawake wenye matatizo ya Fistula
kugharamia nauli za kutoka sehemu mbalimbali nchini kupitia M-PESA
kuwawezesha kufika jijini Dar es salaam kupata matibabu.
Kila mmoja anayo nafasi ya kuonesha upendo na thamani kwa mama kwa
kuokoa maisha yao, Taasisi za Umma na Binafsi, mtu binfasi ama shirika
la kijamii changia sasa kwa njia ya M-PESA kwenda namba 200500, au na
kwa njia ya SMS kwa tuma ujumbe usemao MOYO kwenda namba 15599.
Kama sio wewe basi jirani au rafiki anaweza kuwa shahidi wa jambo hili.
No comments:
Post a Comment