Mwenyekiti wa wafanyabishara wa mifugo Nyaga wa Nyaga akitoa
mapendekezo ya wafanyabiashara kupinga kuhamia katika soko hilo
kutokana na kutokamikilia kwa miundombinu huku Dkt Mugarula na Dkt
Qwali wakitupia kisogo kamera wakiwa wameweka mikono nyuma kuashiria
kushindwa kwa hoja zao.
Wafanya biashara hao wamesema kama
Wizara ya Mifugo na Uvuvi haitarekebisha kasoro ambazo ziko katika soko
la Nyamatala, hawako tayari kuhama katika soko la Igoma ambako
wanafanyia biashara yao kwa sasa, na kama watalazimishwa kuhama
watasitisha kutoa huduma ya kuuza na kuchinja mifugo ili kuipa serikali
ujumbe kuhusu kutatua tatizo hilo.
Choo kinachotarajiwa kutumiwa na wafanyabiashara wa mifugo pamoja na
wateja mbalimbali watakaofika katika soko la Kimataifa la mnada wa
Nyamatala, Misungwi Mwanza.Choo hicho kina matundu manne mawili kwa
ajili ya wanawake na mengine kwa matumizi ya wanaume.
Trekta
na bolzer la maji likiwa limeegeshwa katika soko la Kimataifa
Nyamatala, Misungwi bolzer hilo linauwezo wa kubeba maji lita 4000,
maji ambayo yatatumika kwa ajili ya kunywesha mifugo pamoja na matumizi
ya choo
Jengo
la kujikinga na mvua ama jua liliojengwa katika soko la mnada wa
Kimataifa wa Nyamatala ,Misungwi Mkoani Mwanza, ambalo linalalamikiwa
na wafanyabiashara wa mifugo kuwa ni dogo na halikidhi mahitaji ya soko
hilo kulingana na hadhi yake.
Sehemu ya kunyweshea mifugo maji katika soko la mnada wa Kimataifa, Nyamatala wilayani Misungwi kama linavyoonekana.
Dkt Mugarula wa kwanza kushoto akisikiliza maswali kutoka kwa Joseph Sikila, Makamu Mwenyekiti wa MWASIBA aliysimama kulia.
No comments:
Post a Comment