Chama
Cha Mapinduzi (CCM) kimesema kinajiendesha kwa kuheshimu maoni,
maamuzi na ushauri unaotolewa na wananchama wake katika ngazi
mbalimbali.
Hayo
yamesemwa na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Profesa Makame Mnyaa Mbarawa
wakati akimnadi mgombea wa CCM Jimbo la Uzini Mohamedraza Hassanal
Dharamsi katika shehia ya Mchangani Mkoa Kusini Unguja.
Profesa
Mbarawa amesema Kamati Kuu ya Taifa ya CCM hufanya uchambuzi, kupima
mambo kwa vigezo husika hatimaye huzingatia maamuzi na ushauri wa
wananchama wake.
Amesema CCM si chama kinachochakachua, kubadili au kupuuzia maoni na maamuzi ya wanachama wake kwa kufanya upendeleo.
Ameeleza kuwa CCM ni taasisi ya kisiasa yenye uzoefu mkubwa Barani Afrika, viongozi wake ni mahiri, wajuzi na wenye uwezo wa kupima mwenendo ulivyo.
Aidha
Mjumbe huyo Kamati Kuu ya CCM amesisitiza kuwa CCM huongozwa na
mwelekeo wa Katiba na Kanuni zake bila ya kufanya ubaguzi, upendeleo na
maonevu.
Akizungumzia
mchakato wa kumpata mgombea wa Uzini, Profesa Mbarawa amesema Kamati
Kuu ya CCM imefanya tafakuri pana, uchambuzi wa kutosha na kukusanya
vielelezo vilivyomthibitisha kuwa Raza anatosha kuwa mgombea.
Amewataka wananchi wa Uzini kujipanga na kuhakikisha Mgombea huyo wa
CCM anashinda katika uchaguzi wa Februari 12 mwaka huu, ili
ashirikiane na wananchi wenzake kuleta maendeleo.
No comments:
Post a Comment