Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Jakaya Mrisho Kikwete jana, Jumapili, Februari 5, 2012, alikutana na kufanya mazungumzo na
Meya wa Mji wa Wurzburg wa Ujerumani, Mh.George Rosenthal.
Katika
mazungumzo hayo yaliyofanyika kwenye Ikulu Ndogo mjini Mwanza, Meya
Rosenthal ameambatana na madiwani wanne, mkewe, Hanna Rosenthal na binti
yake, Lisa Rosenthal.
Ujumbe
huo wa mji wa Wurzburg unatembelea Jiji la Mwanza kwa muda wa wiki
moja ikiwa ni ziara ya kirafiki kati ya miji hiyo miwili uhusiano wa
kindugu.
Mji
wa Wurzburg ulianzishwa miaka 1,300 iliyopita, una vyuo vikuu vitatu
na wanafunzi kiasi cha 30,000 wanaosoma katika vyuo hivyo.
Mji
wa Wurzburg unalisaidia Jiji la Mwanza katika maeneo kadhaa ikiwa ni
pamoja na utunzaji mazingira, afya, nishati. Pia miji hiyo miwili ina
program ya kubadilishana wanafunzi kwa maana ya wanafunzi wa miji hiyo
miwili kutembeleana na pia Jiji la Wurzburg linaisaidia taasisi za
kijamii za Jiji la Mwanza.
Rais
Kikwete amemwambia Meya Rosenthal kuwa Tanzania na Ujerumani zina
uhusiano mzuri na wa karibu na Serikali yake imedhamiria kukuza na
kuimarisha zaidi uhusiano huo.
Rais
pia amesifu uhusiano huo wa kindugu kati ya miji ya Mwanza na Wurzburg
na ametaka miji hiyo kuimarisha uhusiano huo kwa sababu ni muhimu na
unanufaisha pande zote mbili. Rais Kikwete yuko katika ziara ya siku
tatu mkoani Mwanza.
Mwisho.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
No comments:
Post a Comment