Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa tanzania Dk Jakaya Mrisho Kikwete,akiendesha Kikao cha kamati Kuu
ya Chama hicho katika ukumbi wa Makao Makuu ya CCM Dodoma leo,(wa
pili kushoto) Rais Msataafu wa Zanzibar,na Makamo Mwenyekiti wa CCM
Zanzibar Dk Amani Abeid Karume,Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa
Baraza la Mapinduzi,pia Mjumbe wa Kamati Kuu,Dk Ali Mohamed
Shein,kushoto) na Katibu Mkuu wa Chama hicho Taifa Wilson Mkama.
Mshabuliaji
wa timu ya Simba Emmanuel Okwi akishangilia mara baada ya kufunga goli,
katika mchezo wa Ligi kuu ya Vodacom, unaoendelea kwenye uwanja wa
Taifa jijini Dar es salaam jioni hii dhidi ya Azam FC ya Chamazi.
Mpira umekwisha na timu ya Simba imeshinda magoli 2-0 dhidi ya Azam FC
yaliyofungwa na mshambuliaji wa timu hiyo Emmanuel Okwi, mchezo wa leo
ulikuwa ni wa kuvutia sana kwa kila timu lakini Simba imeonekana
kutawala sana mchezo katika kipindi cha chote cha mchezo
Wachezaji wa timu ya Simba wakishagilia kwa pamoja na mashabiki mara baada ya kujipatia goli la kwanza katika mchezo wao dhidi ya Azam FC ya Chamazi.
Hiki ni kikosi cha timu ya mpira wa miguu ya Mango Garden kilichoshiriki katika bonaza la Serengeti Intebar Soccer Bonanza kwa ajili ya kutambulisha Muonekano Mpya wa Dhahabu na Serengeti Lager lililofanyika leo kwenye viwanja vya Leaders jijini Dar es salaam na kushirikisha bar mbalimbali hapa jijini Dar es salaam.
Wachezaji
wa timu ya Mango Garden na Breakpoint wakichuana vikali wakati timu
hizo zilipocheza katika bonanza la mpira wa miguu kwa timu za baa
mbalimbali jijini Dar es salaam kwenye viwanja vya Leaders.
Timu ya Lakers ya Namanga na na timu ya Temboni wakichuana kuwania mpira wakati wa mchezo wao kwenye michezo ya Serengeti Interbar soccer Bonanza kwa ajili ya kutambulisha Muonekano Mpya wa Dhahabu na Serengeti Lager.
Kikosi cha timu ya Lakers kutoka Namanga kikiwa katika picha ya pamoja kabla ya mpambano wao na timu ya Breakpoint.
Wakati wenzake wakipata maji ya Muonekano Mpya wa Dhahabu na Serengeti Lager Mdau Victor Makinda yeye aliamua kupoza koo kwa Dafu kama anavyoonekana hapa katika picha.
Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akiwasili ukumbini kuzungumza
na wabunge wa CCM katika kikao chake na wabunge hao kilichofanyika jana
jioni Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma.Wengine kutoka kushoto ni Spika
wa Bunge Anne Makinda, Katibu wa Wabunge wa CCM, Jenista Mhagama na
Waziri Mkuu Mizengo Pinda na Kulia ni Katibu Mkuu wa CCM, Wilson Mukama
na Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Pius Msekwa.
Katibu wa Wabunge wa CCM, Jenista Muhagama akitoa maelezo ya awali
kabla ya Mwenyekiti wa CCM Rais Kikwete kuzungumza na wabunge hao.
Wapili kushoto ni Waziri Mkuu Mizengo Pinda na kulia ni Katibu Mkuu wa
CCM Wilson Mukama na Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara ) Pius Msekwa.
Mwenyekiti
wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akisisitiza jambo wakati alipozungumza na
Wabunge wa CCM, katika kikao chake na wabunge hao jana katika ukumbi wa
Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma. Kushoto ni Waziri Mkuu Mizengo Pinda
na kulia ni Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Pius Msekwa.
Mwandaaji wa onyesho la mavazi la 'Lady in Red' Reloaded 2012 Asia
Idarous akiwa katika picha ya pamoja na mume wake Bw. Wa Hamsini katika
onyesho hilo lilinalofanyika usiku huu kwenye hoteli ya Serenea Dar es
salaam jijini Dar es salaam, onyesho hilo pia litatumika kuchangisha
fedha kwa ajili ya kujenga kituo cha kuhudumia watu walioathirika na
madawa ya Kulevya hapa nchini. kitakachojengwa huko Kikale, Rufiji mkoani Pwani
Mmoja
wa wanamitindo akipita na moja ya mavazi yaliyobuniwa kwa ajili ya siku
ya wapendanao katika onyesho la mavazi la Lady In Red jijini Dar es
salaam.
Mshereheshaji wa onyesho hilo akitoa ratiba ya onyesho hilo siku huu katika hoteli ya Serena Dar es salaam.
Mtangazaji wa Clouds TV akifanya mahojiano na warembo wa zamani Jaquiline Patrick na mrembo Lisa Jensen katika onyesho hilo.
Bandi ya muziki wa
Dansi ya Kalunde na uongozi wa hoteli ya Trinity ya Oysterbay jijini Dar
es salaam, imeandaa onyesho kali katika siku ya wapendanao (Valentine
Day) itakayofanyika Februari 14 duniani kote.
Akizungumza
na FULLSHANGWE Mkurugenzi wa bendi hiyo Deo Mwanambilimbi, amesema
bendi yake imejiandaa vyema kuhakikisha inatoa burudani kabambe siku ya
wapendanao, ikiwa na wanamuziki wake kama Bob Ludala, Gringo Junior,
Deo Mwanambilimbi mwenyewe na Debora Nyangi pamoja na wanamuziki
wengine.
Siku hiyo kutakuwa na zawadi
mbalimbali zikiwemo Wine pamoja na zawadi zingine kemkem, huku
mwanamuziki mwalikwa Shilole akishiriki katika onyesho hilo na kutoa
burudani kwa kuimba nyimbo zake zote, katika usiku huo wa wapendanao.
Kiingilio katika onyesho hilo kitakuwa
bei rahisi kabisa yaani shilingi elfu 15.000 kwa kila mtu, watu wote
mnakaribishwa kuja kuona burudani kutoka kwa Kalunde Band.
WASANII
wakali wa muziki wa kizazi kipya nchini, Mwana FA, AY, Kundi la TMK
Wanaume Family na Bendi ya African Stars ‘Twanga Pepeta’ kwa pamoja
wanatarajiwa kuangusha bonge la shoo siku ya Jumapili hii ndani ya
Ukumbi wa Dar Live jijini Dar es Salaam huko Mbagala.
Akizungumza
na wanahabari mchana huu, mratibu wa burudani katika ukumbi huo, Juma
Mbizo, alisema maandalizi yote kuhusiana na tamasha hilo
yamekamilika.kama anavyoonekana mwanamuziki Mwana FA akielezea jinsi atakavyofanya makamuzi ya nguvu. Ambwene Yessayah ‘AY’ akiumwagia sifa ukumbi wa Dar Live ambao baada ya kuuona aligundua kuwa una hadhi ya kimataifa.
KOCHA Mkuu wa Simba, Milovan
Cirkovic akizungumza na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa mikutano
wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini Tanzania TFF, wakati alipoelezea
maadalizi ya timu yake, kabla ya kushuka dimbani kwenye uwanja wa Taifa
Kesho jumamosi,kumenyana na vijana wa Bakhressa yaani Azam FC ya huko
Chamazi.
Kocha
Milovan ameisifu timu ya Azam FC na kusema ni timu nzuri na yenye
ushindani mkubwa, lakini pamoja na kwamba kuna baadhi ya wachezaji wake
hawako fiti sana, wamejiandaa vyema kupambana na timu hiyo na lengo ni
kupata Pointi tatu muhimu, ili kujweka vizuri katika msimamo wa Ligi kuu
ya Vodacom
Naye Msemaji wa timu hiyo Ezekiel Kamwanga amewaomba
mashabiki kujitokeza kwa wingi ili kushuhudia mchezo huo utakaokuwa wa
kuvutia kutokana na viwango vya timu zote mbili, ameongeza kwamba kama
inavyofahamika michezo mingi katika ya Simba na Azam FC inakuwa siyo ya
kukamiana, hivyo ana imani kuwa mchezo wa kesho utakuwa na burudani
tosha kwa mashabiki wa mpira, katika picha kushoto ni msemaji wa Simba
Ezekiel Kamwanga.
.Spika
wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Anne Makinda akiingia
ndani ya ukumbi wa bunge leo mjini kuongoza kikao cha tisa cha mkutano
wa sita wabunge ambapo bunge linahitimisha shughuli zake mjini Dodoma.
Picha na Aron Msigwa – MAELEZO.
Mbunge
wa Same Mashariki Anna Kilango akijadili jambo na Mwanasheria mkuu wa
serikali Jaji Frederick Werema ndani ya ukumbi wa Bunge leo wakati wa
kipindi cha maswali na majibu mjini Dodoma.
Mbunge wa Singida mjini Mohammed Dewji akimsikiliza kwa makini Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais Uhusiano na Uratibu Stephen Wasira ndani ya ukumbi wa bunge leo mjini Dodoma.
Wajumbe na Viongozi wa chama cha wamiliki wa shule Vyuo
na shule binafsi (TAMONGSCO) wakiwa katika picha ya pamoja mara baada
ya kutoka ndani ya ukumbi wa bunge leo mjini Dodoma. Viongozi hao wapo
bungeni Dodoma kukutana na kamati ya kudumu ya bunge ya huduma za jamii kwa lengo la kuhimiza ushirikiano kati yao na wabunge pamoja na serikali ili kubadilishana uzoefu na kujadili changamoto zinazoikabili sekta binafsi ya elimu nchini Tanzania.
Mbunge wa Bumbuli January Makamba akiwasilisha Hoja binafsi kuhusu
sheria ya udhibiti wa shughuli za upangaji nyumba za makazi aliyoitoa
chini ya kanuni ya 54 (1) ya kanuni za bunge toleo la 2007 ya kuliomba
bunge kuazimia kwa kauli moja ,kuitaka serikali katika mkutano ujao wa
saba kuleta Muswaada wa Sheria ya kudhibiti Upangaji wa Nyumba na Makazi
kufuatia malalamiko mengi kutoka kwa wananchi wanaoishi mijini
kutokana na adha wanazopata katika kutafuta nyumba za kupanga au kuishi
kwenye nyumba hizo.
Spika
wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Anne Makinda akiwasalimia
viongozi na wachezaji wa timu ya Villa Squard ya Kinondoni jijini Dar
es salaam waliofika bungeni hapo kuona shughuli mbalimbali zinazofanywa
na bunge.
Spika
wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Anne Makinda akifurahia
jambo na wanafunzi wa shule ya sekondari Hijra ya mjini Dodoma nje ya
ukumbi wa Bunge Dodoma.
No comments:
Post a Comment