Madereva
mbalimbali hasa wa masafa marefu wanatarajia kunufaika na bima ya
maisha kwa kupewa Kiasi cha Milioni Mbili kutoka katika Bima ya jubilee
hali ambayo itawafanya madereva walio wengi kuweza kujikwamua katika
suala zima la umaskini, ulemavu, vifo ambavyo vinasababishwa na ajali
hizo.
hayo yamebainishwa na Meneja wa kanda
ya kaskazini kutoka katika bima ya Jubilee(JUBILEE INSUARANCE} Bw
Charles Magori wakati akiongea na vyombo vya habari jijini hapa mapema
wiki hii.
Bw
Magori alisema kuwa Bima ya maisha ambayo itaweza kuwafikia madereva
wengi zaidi itakuwa na manufaa makubwa sana kwa kuwa baadhi ya madereva
hasa wale wa masafa marefu wamekuwa katika maisha ya taabu mara ya
kupata ajali.
Alibainisha kuwa mara baada ya kupata ajali asilimia kubwa ya madereva
hao hushindwa kufikia malengo yao kwa kuwa tayari wanakuwa wameshapata
vilema vya maisha,vifo ambapo hupelekea kukosa garama za mazishi hali
ambayo ni hatari kwa maisha ya sasa.
“tulichoweza
kugundua ni kwamba hawa madereva mara nyingi wanakuwa katika hatari
mbaya sana ya ajali na hivyo hata kwa wale ambao wanakufa familia zao
zinakuwa katika wakati mgumu sana huku nyingine nazo zikiwa hata kwenye
hatari ya kukosa fedha kwa ajili ya mazishi lakini tunachoweza
kukifanya hapa ni kuhakikisha kuwa tunasaidia jamii kwa kuwapa milioni
mbili kwa ajili ya maandalizi mbalimbali'alisema Bw magori
Awali alisema kuwa mbali na kutoa bima hiyo hasa kwa madereva pia kwa sasa zoezi hilo
la kutoa bima litaenda sanjari na elimu mbalimbali ambazo zinahusu uimu
wa bima kwa maisha ya mtanzania kutokana na kuwepo kwa matukio
mbalimbali ambayo yana historia ya kutokea sana kwa ndani ya jamii.
Bw. Magori alisema kuwa endapo kama madereva hao wataweza kupata elimu hiyo ya bima basi watanufaika kwa kiwango cha hali ya juu sana ambapo kwa sasa bado baadhi ya jamii hazina mwitikio wa masuala ya bima.
Pia aliwataka
wananchi wote kuhakikisha kuwa wanajijengea tabia ya kutafuta elimu
mbalimbali za bima kwa kuwa bima ni msingi wa maisha ya kila mtanzania
hususani kwa sasa ambapo jamii nyingi kukosa elimu hali ambayo
inachangia kuwepo fikra hasi juu ya uimu wa bima kwa maisha ya
mtanzania wa sasa.
No comments:
Post a Comment