BUNGE LAAHIRISHWA LEO HUKU HOJA YA MGOMO WA MADAKTARI IKIIBUKA KWA MARA YA SITA BUNGENI,SPIKA KUTOA UFAFANUZI KESHO.
Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania wakiwa wamesimama mara baada ya Naibu Spika wa
Bunge Job Ndugay Kuahirisha kikao cha Bunge leo mjini Dodoma.Pamoja na mambo
mengine yaliyojitokeza wakati wa kuahirisha kikao hicho ni hoja ya Mgomo wa
madaktari ambayo iliibuliwa na mbunge wa Kigoma mjini Peter Selukamba ambaye
aliitaka serikali kutoa tamko la hatma ya mgomo huo ambapo Naibu spika Job
Ndugay aliwataka wabunge kuwa na subira ili Ofisi ya spika ikutane na kamati ya
uongozi ya bunge ili kutoa maamuzi hapo kesho kabla ya kuahirisha
mkutano huo wa sita.
Aliyekuwa waziri mkuu na mbunge wa
Monduli Edward Lowasa (kushoto) akijadili jambo na Waziri wa nchi Ofisi ya Rais
Mahusiano na Uratibu Stephen Wasira (katikati) na mbunge wa viti maalum
CHADEMALeticia Nyerere leo mjini Dodoma.
Picha na Aron
Msigwa – MAELEZO.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira
Dkt. Terezya Huvisa (Kulia) akizungumza na Zainabu Kawawa mbunge wa viti maalum
CCM mara baada ya kumalizika kwa kikao cha saba cha bunge leo mjini
Dodoma.
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Emmanuel Nchimbi
(katikati)akifurahia jambo na Mbunge wa Mbeya mjini Joseph Mbilinyi (kulia)
maarufu kwa jina la Sugu (CHADEMA) na mbunge wa Kigoma mjini Peter Selukamba
(kushoto) nje ya ukumbi wa bunge mjini Dodoma.
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Job Ndugay akitekeleza majukumu yake wakati wa Kipindi cha maswali na
majibu leo mjini Dodoma .
No comments:
Post a Comment