Naibu spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugay
akitoa ufafanuzi wa hoja mbalimbali zilizowasilishwa na wabunge wakati
wa kikao cha tano cha mkutano wa sita leo mjini Dodoma.
Waziri wa Nishati na Madini William Ngeleja akijibu maswali ya wabunge kuhusu upatikanaji wa umeme wa uhakika nchini na
uondoaji wa tatizo la mgawo wa umeme unaoendelea kwenye baadhi ya
maeneo nchini na kufafanua kuwa serikali inaendelea na mikakati ya
utekelezaji wa miradi mbalimbali ya utoaji wa huduma ya umeme katika
maeneo yasiyo na huduma hiyo na kuimarisha uzalishaji wa umeme wa
uhakika katika Gridi ya Taifa kupitia vyanzo mbalimbali.
Mbunge wa Kigoma Kusini (NCCR –Mageuzi) David Kafulila akichangia bungeni kuhusu namna bora ya ukusanyaji wa mapato kupitia kodi zinazotozwa kwenye makampuni ya simu nchini ili kuongeza mapato ya serikali leo mjini Dodoma.
Waziri
na Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Hadji Mponda(kushoto) akizungumza
jambo na Waziri Mkuu Mizengo Pinda (kulia)ndani ya ukumbi wa Bunge leo
mjini Dodoma.
Naibu waziri wa Wizara ya Fedha Gregory Theu (kushoto) akizungumza jambo na Naibu waziri wa Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika Christopher Chiza (kulia) nje ya ukumbi wa Bunge leo mjini Dodoma.
Waziri
wa Fedha Mustapha Mkulo (kulia) akitoa ufafanuzi wa masuala mbalimbali
kwa wabunge mara baada ya kumalizika kwa kikao cha tano cha mkutano wa
sita leo mjini Dodoma.Kutoka kushoto ni mbunge wa Kigoma Kaskazini
Zitto Kabwe na Davidi Kafulila (wa pili kutoka kushoto) kutoka Kigoma
kusini.
Picha na Aron Msigwa –MAELEZO.
No comments:
Post a Comment