UCHAGUZI
MDOGO JIMBO LA ARUMERU MASHARIKI KUFANYIKA APRIL MOSI
Na Lydia Churi, MAELEZO
Uchaguzi mdogo
wa ubunge katika jimbo la Arumeru Mashariki unatarajiwa kufanyika April Mosi
mwaka huu.
Uchaguzi huo
utafanyika baada ya jimbo hilo kuwa wazi kutokana na kifo cha aliyekuwa mbunge
wake Marehemu Jeremia Solomon Sumari aliyefariki dunia Januari 19 mwaka
huu.
Taarifa
iliyotolewa na Tume ya Taifa ya uchaguzi leo jijini Dar es salaam imesema pamoja
na uchaguzi huo mdogo pia kutakuwepo na chaguzi ndogo za madiwani katika kata za
Halmashauri mbalimbali nchini.
Taarifa hiyo ya
Tume ya Taifa ya uchaguzi inaonesha kuwa katika uchaguzi mdogo wa ubunge kwenye
jimbo la Arumeru Mashariki uteuzi wa wagombea utafanyika Machi 8, na kampeni
zitaanza Machi 9 hadi 31 mwaka huu.
Aidha, Tume
hiyo pia itafanya chaguzi ndogo za madiwani katika kata nane zilizoko katika
halmashauri mbalimbali nchini kufuatia kuwepo wazi kwa nafasi za viti vya
madiwani ambazo zimetokana na vifo vya madiwani husika.
Katika chaguzi
ndogo za madiwani uteuzi wa wagombea utafanyika Machi 5 na kampeni
zitaanza Machi 6 hadi 31 mwaka huu. Kata zitakazohusika kwenye uchaguzi huo ni
zile vijibweni-Temeke, Kiwanga-bagamoyo, Kirumba-Mwanza, Logangabilili-Bariadi,
Chan’gombe-Dodoma, Kiwira-Rungwe, Lizaboni-Songea na Msambweni-Tanga.
Taarifa hiyo
iliyosainiwa na Mwenyekiti wa Tume hiyo Jaji Damian Lubuva imesema kuwa
hakutakuwa na kuandikisha wapiga kura kwa ajili ya chaguzi hizo ila daftari la
kudumu la wapiga kura lililotumika wakati wa uchaguzi mkuu uliopita litatumika.
Tume inawasisitiza wananchi na vyama
vyote vya siasa kuzingatia na kufuata ratiba ya uchaguzi na kujitokeza kwa wingi
kushiriki katika mchakato wa uchaguzi kuanzia siku ya uteuzi wa wagombea,
kampeni za uchaguzi na siku ya kupiga kura. Vituo vya kupigia kura vitafunguliwa
saa 1.00 asubuhi na kufungwa saa 10.00 alasiri
No comments:
Post a Comment