Ligi
Kuu ya Vodacom ambayo iko katika raundi ya 16 inaendelea kesho kwa
mechi moja kati ya Yanga na Mtibwa Sugar. Mechi hiyo namba 112 itachezwa
kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia saa 10.30 jioni.
Mechi
hiyo itachezeshwa na mwamuzi Ibrahim Kidiwa kutoka Tanga wakati
wasaidizi wake ni Michael Mkongwa kutoka Iringa na Kudura Omary wa
Tanga. Kamishna wa mechi hiyo ni Mohamed Nyange kutoka Dodoma.
Viingilio
katika mechi hiyo vitakuwa sh. 3,000 kwa viti vya bluu na kijani, sh.
5,000 kwa viti vya rangi ya chungwa, sh. 10,000 kwa VIP B na C, na sh.
15,000 kwa VIP A.
Timu
14 za Ligi Daraja la Kwanza (FDL) zitakuwa kwenye viwanja saba tofauti
kesho (Februari 8 mwaka huu) katika mfululizo wa ligi hiyo ambayo iko
katika hatua ya makundi.
Transit
Camp na Mgambo Shooting zitachuana kwenye Uwanja wa Mkwakwani jijini
Tanga katika mechi pekee ya kundi A itakayochezeshwa na mwamuzi Said
Ndege wa Dar es Salaam.
Kundi
B litashuhudia mechi tatu. Tanzania Prisons itakuwa mwenyeji wa Small
Kids kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya, JKT Mlale
itaoneshana kazi na Mbeya City kwenye Uwanja wa Majimaji mjini Songea na
Polisi Iringa itacheza na Majimaji kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya
Samora mjini Iringa.
Mechi
za kundi C zitakuwa kati ya Polisi Morogoro na Morani FC itakayochezwa
Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro, AFC na Rhino zitacheza kwenye Uwanja
wa Sheikh Kaluta Amri Abeid jijini Arusha na Polisi Tabora itakuwa
mwenyeji wa 94 KJ kwenye Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora.
No comments:
Post a Comment