Spika
wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Anne Makinda akitoa
ufafanuzi kwa wabunge leo mjini Dodoma baada ya kuzuia hoja ya mgomo wa
madaktari bingwa kujadiliwa Bungeni iliyoibuliwa na mbunge wa Mbozi
Magharibi Godfrey Zambi na kufafanua kuwa suala hilo
tayari limeshaanza kufanyiwa kazi na Bunge ikiwemo kuiagiza kamati ya
huduma za jamii kulifuatilia suala hilo kwa kukutana na pande
zinazohusika na kupeleka majibu bungeni.
Naibu waziri , Ofisi ya Waziri mkuu Tawala za mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Aggrey Mwanri akitoa ufafanuzi wa maswali mbalimbali yaliyoulizwa na wabunge kwenye ofisi ya waziri mkuu yakiwemo masuala ya migogoro ya mipaka ya viwanja kwenye Halmashauri na
manispaa ya Kigoma –Ujiji pamoja na suala la kuongeza madaktari bingwa
na manesi katika manispaa ya Dodoma kufuatia ongezeko la watu na vyuo
mbalimbali leo mjini Dodoma.
Mawaziri
na wabunge wakifuatilia kwa makini mkutano wa sita wa Bunge la Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania leo mjini Dodoma. Kutoka kushoto ni Makamu wa pili wa Rais wa serikali ya Mapinduzi Zanzbar Balozi Seif Ali Idd ,mbunge wa Songea Jenista Mhagama
na Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki Samueli Sitta (kulia),
wengine waliokaa nyuma ni Waziri ,Ofisi ya Waziri mkuu Uwekezaji na
Uwezeshaji Dkt. Mary Nagu, Waziri wa Habari, Vijana ,
Utamaduni na Michezo Dkt. Emmanuel Nchimbi na Naibu waziri wa Kazi na
Ajira Makongoro Mahanga.
Raia wa kigeni ambao wako nchini wakiwa
ndani ya Bunge wakifuatilia kipindi cha Maswali na majibu cha mkutano
wa sita wa Bunge kufuatia mwaliko wa Spika wa Bunge la Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Anne Makinda.
Wafanyakazi wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC Taifa) wakitekeleza majukumu yao ndani
ya ukumbi wa Bunge kwa kuhakikisha kuwa watanzania wanayapata
matangazo ya Bunge kupitia TBC Taifa moja kwa moja kutoka mjini Dodoma.
Picha na Aron Msigwa –MAELEZO.
No comments:
Post a Comment