Na Ashura Mohamed - Arusha
Serikali
kupitia Wizara ya ulinzi na usalama imeombwa kuendelea kuwaboreshea
makazi askari polisi ili waweze kuishi katika mazingira mazuri na
kuongeza ufanisi katika kazi.
Akizungumza
katika sherehe za kukaribisha mwaka mpya 2012 zilizoandaliwa na jeshi
la polisi mgeni rasmi katika hafla hiyo ambaye ni hakimu mkazi mkoani
arusha Charles Magesa amesema kuwa ili kuongeza ufanisi katika kazi pia
ni vyema polisi nao wakaboreshewa makazi yao.
Magesa
ameongeza kuwa taasisi yeyote inayofanya kazi ya kuihudumia jamii ni
lazima changamoto zake zishughulikiwe hivyo amewataka polisi kufanya
kazi kwa uwazi na umakini zaidi ili jamii inayoizunguka iweze kuwa na
imani nao.
Aidha
amesema kuwa jamii ni lazima iweze kulisaidia jeshi la polisi katika
kuhakikisha kuwa linatekeleza majukumu yake ipasavyo ikiwa ni pamoja na
kuwapa ushirikiano zaidi ili kuhakikisha kuwa wanafikia malengo yao.
Kwa
mujibu wa kamanda wa polisi mkoa wa Arusha Thobias Andeng’enye
amesema kuwa vitendo vya uhalifu katika mkoa wa Arusha vimepungua
ukilinganisha na mwaka 2010.
Andeng’enye
amesema kuwa jumla ya matukio 25,833 yaliripotiwa mwaka 2011
ikilinganishwa na matukio 26,698 yaliyoripotiwa kwa mwaka 2010 ambapo
ni pungufu ya matukio 865.
Amefafanua kuwa matukio hayo yamegawanyika katika makundi manne ni makosa dhidi ya binadamu,makosa dhidi ya mali,makosa dhidi ya maadili ya Jamii na makosa ya usalama barabarani ambapo ni pamoja
na mauji,kubaka,kulawiti.wizi wa watoto,kutupa watoto,unyang’anyi wa
kutumia silaha,unyang’anyi wa kutumia nguvu,wizi wa magari,wizi wa
mifugo,ajali za moto na makosa ya usalama barabarani.
Hata
hivyo kamanda Andengenye ametaja changamoto wanazokabiliana nazo kwa
mwaka 2012 ni pamoja na Tatizo la ajira kwa vijana ni changamoto
nyingine inayosababisha kuongezeka kwa vitendo vya uhalifu kutokana na
vijana hao kutokuwa na namna ya kutafuta kipato hivyo inakuwa rahisi
kujiingiza katika vitendo vya uhalifu.
No comments:
Post a Comment