NA GLADNESS MUSHI - ARUSHA
VIONGOZI wa dini ya kiislamu mkoani Arusha,
wameongoza kongamano maalumu la kulaani mauaji yanayofanywa na kikundi
kidogo cha kiislamu chenye msimamo mkali cha Boko haramu nchini
Nigeria dhidi ya madhebebu ya dini ya kikristo.
. Wakizungumza kwenye kongamano la amani lililofanyika mwishoni mwa
wiki katika msikiti Al hamadiyya jijini hapa,walidai kuwa hakuna maagizo
ya mwenyezi mungu yanayotoa mamlaka kwa kikundi hicho ama mtu yoyote
kutekeleza mauaji hayo dhidi yawaumini wa dini nyingine.
Amiri na mbashirimkuu wa jumuiya ya waislamu wa Ahmadiyya
nchini,Tahir Mohmood Choudhly aliwaomba waislamu kote duniani kuungana
na kulaani vitendo vya kinyama kama hivyo vinavyofanyika kwa kutumia
mgongo wa uislamu
.Aliwaomba watanzania kuwalilia wananchi
wote waliouawa kutokana na kikundi hicho cha Boko haramu nchini
Nigeria,na aliiomba serikali nchini humo, kukakikisha inadhibiti
mauaji hayo na kukishughulikia kikundi hicho kinachotumia mgongo wa
uislamu.
‘’Sisi waislamu tufike mahali tuelezane ukweli kwani matukio mengi ya
uvunjifu waamani yakiwemo kujilipua yanasababishwa sana na waumini
wenzetu ,hakuna maandiko yanayoagiza dini ya kiislamu iteketeze dini
nyingine ‘’alisema Choudhly.
Aidha aliongeza kwa kuwataka viongozi wamadhehebu ya dini nchini
kusimama imara katika kutetea amani na kujiepusha na uchochezi,kwani
taifa linawategemea sana katika kuepusha machafuko yanayoweza kuibuka
. Katika hatua nyingine, aliwataka wananchi kuheshimu viongozi waliopo
madarakani na kuacha kupinga kila kitu kinachotamkwa na kiongozi
aliyeko madarakani, badala yake watoe mchango wakusukuma maendeleo ya
taifa hadi utakapo fanyika uchanguzi mwingine.
Naye Sheikh mkuu wa
Ahamadiyya kanda ya kaskazini, Mzafara Ahamad,alisema kuwa lengo lakongamano hilo lililowashirikisha
viongozi mbalimbali wa madhehebu ya dini ya kiislamu nchini
ni kutoa mada ya kuomba amani na kulaami mauaji ya kikatili
yanayoongozwa na kikundi haramu cha kiislamu nchini Nigeria.
Alisema kuwa kongamano hilo lilienda sanjari na uzinduzi wa msikiti
huo wa Ahmadiyya Muslim Jamaint uliogharimu kiasi cha shilingi milioni
70 kwa ajili ya ukarabati ulioanza mwishoni mwa mwaka jana
. Kwa upandewa sheikh mkuu wa Ahamadiyya mkoa wa Morogoro,Bakari
Kaluta,aliwataka viongozi wa dini nchini kutawala kiuadilifu
huku wakiongozwa na mwenyezi mungu katika mahubiri yao na kuacha kuwa
sehemu yakuleta mitafaruku ya kidini
. Ameyasihi madhebebu ya dini kuwa na utaratibu wa kuandaa makongamano
ya kuomba amani,kwani bila hivyo nchi itaelekea kubaya kwakuwa baadhi
ya viongozi wa dini wamekuwa wakitumia vibaya maandiko matakatifu kwa
kuhubiri uvunjifu wa amani kwa maslahi yao binafsi.
Naye meya wa jiji la Arusha ,Gaudence Lyimo aliyekuwa mgeni rasmi
katika kongamano hilo,aliyasifu madhehebu ya dini ya kiislamu kwa
kuandaa kongamano hilo la kuomba amani ,aliwatia moyo viongozi
hao kuwa serikali inatambua mchango wao na inawaungamkono kwa jambo
hilo.
Aliwasihi viongozi hao wa dini kuwa sehemu ya serikali katika
jitihada zake za kuhakikisha kuwa amani inapatikana kwa kila mtu hapa
nchini na duniani kote.
NA GLADNESS MUSHI - ARUSHA
WANASAYANSI nchini
kwa kushirikina wenzao duniani, wametakiwa kufuatilia hewa ya ukaa
katika misitu iliyopo nchini, ili kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya
nchi, ambayo huathiri upatikanaji wa mvua kwa msimu .
Katibu
Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii, Maimuna Tarishi kwa niaba ya
Waziri wa mali asili na utalii, Ezekiel Maige, ameyasema hayo leo wakati
alipokuwa akifungua mkutano wa 3 wa wadau wa mazingira, kuhusu uhifadhi
endelevu na kupambana na mabadiliko ya tabia ya nchi, unaofanyika
Jijini Arusha na kushirikisha wanasayansi 53 kutoka duniani kote.
Alisema
kuwa Tanzania tayari wanampango wa Nafoma unaojihusisha na upandaji
miti ya uhifadhi mazingira, ambayo ina uwezo mkubwa wa kukabiliana na
changamoto za mazingira hususani hewa ya ukaa inayozalishwa nchini.
“Watu
lazima wapande miti kwa wingi na siyo bora miti tu, bali wapate ushauri
aina ya miti watakayopanda, tukifanya hivi tutapata mvua kwa wakati
unotakiwa kwa sababu mpango huu umefanikiwa Mkoani Iringa, ambapo zamani
walikuwa hawapati mvua kwa wakati na hewa ilikuwa mbaya ila baada ya
kupanda miti mingi sasa mvua huja kwa mpango na hewa safi” alisema
Maimuna.
Aidha alisema kuwa huwenda wananchi wengi wakashindwa kupanda miti na
kuisubiri kukomaa na kuvuna, badala yake wanapopata shida huivuna kabla
ya kukomaa, ili kuondoka na na tatizo hilo aliwashauri wananchi kubuni
mradi wa ufugaji nyuki kwa kuweka mizinga katika miti watakayootesha
shambani mwao.
Naye Mkurugenzi wa Mazingira kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais, Dk. Julius Ningu alisema kuwa, asilimia 80 ya watanzania hutumia
nishati ya kuni na mkaa na asilimia 10 tu wanatumia umeme, hali mbayo
ni hatari kwa taifa, katika uharibifu wa mazingira.
Alisema
kuwa serikali ili kuondokana na tatizo hili, ipo mbioni kufanya juhudi
za makusudi kutoa ruzuku katika nishati ya gesi, ili wananchi wengi
wamudu gharama ya gesi na kuitumia, na kuondokana na matumzi ya kuni na
mkaa ambayo yamekuwa yakisababaisha uharibifu mkubwa wa mazingira
nchini.
No comments:
Post a Comment