Benjamin Sawe
Kitengo cha Habari
Zanzibar
Watanzania wametakiwa kulinda na kuheshimu tamaduni ili waweze kusonga mbele na kujiletea maendeleo.
Hayo
yamesemwa na Kaimu Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Maendeleo ya
Utamaduni Bi. Lily Beleko katika mafunzo kwa maafisa wa Idara mbalimbali za serikali.
Akiongea
kwenye mafunzo hayo Bi Beleko alisema lengo la mafunzo hayo ni
kuelimisha umma wa watanzania kulinda,kuheshinu,ikiwa ni pamoja na
kushirikiana katika nyanja za kiutamaduni.
Akifungua
mafunzo hayo Kamishna wa Utamaduni na Michezo Zanzibar Bwana Hamadi
Bakari Mshindo alisema kuna umuhimu wa kulinda utamaduni na kuheshimu
tamaduni za mataifa mengine.
“Kuna
umuhimu wa kulinda na kuheshimu tamaduni zetu na tamaduni za mataifa
mengine lakini tuheshimu tamaduni zile zilizo nzuri pekee na kuacha
tamaduni zisisoendana na mila mna tamaduni za mwafrika”.Alisema Bwana
Mshindo.
Bwana Mshindo alisema ni wajibu kwa kila mtanzania kulinda na kuheshimmu tamaduni za mwafrika na za mataifa mengine kwa ujumla.
Alisema
mara nyingi kuna miradi mingi ya maendeleo inafanyika katika maeneo
mbalimbali lakini tamaduni za sehemu husika zinakuwa hazifuatwi.
Aidha alisema kwa upande wa Zanzibar wameshaanza kutoa elimu jinsi ya kulinda na kuheshimu tamaduni za jamii mbalimbali
No comments:
Post a Comment