Na Ashura Mohamed – Simanjiro
Jumuiya ya wananchi wa Korea Kusini wamechimba kisima cha maji katika kata ya Naberero wilayani Simanjiro mkoani Manyara ambacho kimegharimu dola za kimarekani 6500.
Akizungumza
wakati wa kuzindua kisima hicho mchungaji wa kanisa la Juan Jung Ang
lililopo Korea Kusini Park Eung Soon, amesema kuwa maji ni muhimu hivyo
wameona ni vyema kuwasaidia wakazi wa maeneo hayo kwa kuwapunguzia adha
ya kutembea umbali mrefu kutafuta maji.
Park Soon amesema ikiwa kama wananchi wa Tanzania
watakuwa na moyo wa kujitolea kama ilivyo kwa wananchi wa Korea Kusini
basi ni wazi wataweza kubadili nchi kwa kiasi kikubwa.
Amesema kuwa miaka 50 iliyopita hali ya kiuchumi katika nchi hiyo ilikuwa ni mbaya sana kuliko Tanzania lakini wananchi waliweza kujengewa imani kuwa wananafasi kubwa ya kuibadili nchi yao na wakafanikiwa kwa kiwango kikubwa.
“Wananchi waliojitolea msaada huo sio kama ni matajiri bali ni ile hali ya kujitoa na uaminifu juu ya wengine ndio kinachowasaidia” alisema Park Soon.
Naye
Askofu Erick Mkwenda wa Kanisa la kikristo la Marannatha ambaye ni
mwenyeji wa ugeni huo amesema ni jambo la neema kwa kuwa kisima hicho
kitaweza kuwasaidi wakazi wa kata hiyo kutokana na wilaya hiyo kuwa na
tatizo la maji.
No comments:
Post a Comment