TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Monday, February 6, 2012

KANISA LA BABTIST TIMBOLO LAWAJENGEA WATOTO SHULE


NA GLADNESS MUSHI- ARUMERU
Kanisa la Baptist Timbolo lilopo sambasha wilayani arumeru limetoa msaada wa kujenga shule kwa ajili ya watoto yatima, wasiojiweza, pamoja na walemavu a mbapo shule hiyo itagarimu zaidi ya million 150 sanjari na kuanza kuwapa elimui ya sekondari bure mayatim a 30 mwaka huu.
Akiongea na Mwandish wetu mkurugenzi ambaye pia ni mchungaji wa kanisa hilo Bw Saitoti Mollel alisema kuwa lengo ni kuhakkisha kuwa motto wa kike anapata elimu ambayo ni bora zaidi
Alisema kuw a shule hiyo ya timbolo ambayo ni ya sekondari imelenga kuhakikisha kuwa inatoa kipaumble zaidi kwa motto wa kike ambaye amesaulika na jamii hasa za wakazi wa eneo hilo ambapo ni jami za kimasai, na waarusha
Alisema kuwa shule hiyo ambayo inanza rasmi kutoa elimu ya sekondari kwa mwaka huu itaanza na wanafunzi 90 kutoka katika jamii mbalimbali huku kati yao 30 wakiwa ni watoto mayatima ambaoi wataweza kusoma bure ikiwa ni mchango wao kwa kanisa dhidi ya watoto ambao ni mayatima
“Haya ni maono ya kanisa hili la Baptist Timbolo kwa kuwa hapa jirani hakuna shule ambayo inalenga katika kuhakikisha kuwa hawa watoto ambao wanaishi mazingira magumu, na mayatima wanapata elimu lakini sasa kupitia shule hii wataweza kupata haki zao za msingi ambapo ni elimu “alisema Mchungaji Saitoti
Pia aliongeza kuwa mbali na kuweza kuwajengea shule ambayo imegarimu zaidi ya million 150 pia wamefanikiw a kutoa elmu mbalimbali za uasiamli kwa wananchi wa maeneo yao pamoja na khakkisha kuwa wanawajenga kimwili wakristo wao
Alisema kuw a mpaka sasa tayari wameshahamasisha wakristo ndani ya kanisa hilo kuhakikisha kuwa wanajiwekea uataribu maalumu wa [kufuga ambapo kanisa limetoa mbuzi wa kienyeji kama 40 kwa ajili ya vikundi hivyo
“Hawa mbuzi pia ni msada kw a wakristo0 wertu kwa kuwa tunaamini kuwa kupitia mbuzi hawa ambao tumewapa bure tutaweza kuwatoa katika suala zima la umaskini na hivyo wataweza kujikita katika suala zima a ufugaji na kuachana na tabia ya kukaa bure”alisema Mchungaji Saitoti
Hataivyo alisema kuwa ni vema kama makanisa ya leo yatahakikisha kuw a yanatoa msaada hata kwa wakazi wa maeneo ya jirani ambnayo yanazungukwa na makanisa ili waweze kuwasaidia katika kuondokana na umaskini ndani ya maisha yao
Mchungaji huyo aliwataka wakristo kuhakikisha kuwa wanajikita zaidi katika shuguli za maendeleo na kuachana na tabia ya kukata tama kwa kisingizio kuwa maisha yao ni magumu

No comments:

Post a Comment