Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete
leo, Jumapili, Februari 5, 2012, amezindua Kitabu kiitwacho Uongozi na Utawala wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere katika halfa fupi iliyofanyika kwenye Viwanja vya Ikulu Ndogo Mjini Mwanza.
Kitabu
hicho kilichoandikwa na Makamu Mwenyekiti wa CCM, Mheshimiwa Pius
Msekwa kinaelezea uzoefu wa miaka 25 ya Mzee Msekwa katika utumishi wa
umma chini ya uongozi wa Baba wa Taifa, Mwalimu K. Nyerere.
Sherehe
za uzinduzi wa kitabu hicho chenye kusara 156 zimehudhuriwa na
viongozi mbali mbali wakiwamo mawaziri, viongozi waandamizi wa Chama
cha Mapinduzi (CCM) akiwamo Katibu Mkuu Mheshimiwa Wilson Mukama na
viongozi wa Mkoa wa Mwanza.
Akizungumza
kabla ya Mheshimiwa Rais Kikwete hajazindua kitabu hicho, Mzee Msekwa
amesema kuwa moja ya mambo yaliyomchochea aandike kitabu hicho ni
pamoja na changamoto aliyopata kuitoa Rais Kikwete kwa viongozi
wastaafu wa umma kuchangia maendelea na historia ya Tanzania kwa
kuandika vitabu kuelezea uzoefu wao katika utumishi wa umma.
Akizungumza
mara baada ya uzinduzi wa kitabu hicho, Mheshimiwa Rais Kikwete
amempogeza Mzee Msekwa kwa kuandika kitabu hicho na kuwataka wastaafu
wengine wa utumishi wa umma kufuata mfano wa Mzee huyo kwa kuandika
uzoefu wake katika kuwatumikia Watanzania.
Kabla
ya kuwa Makamu Mwenyekiti wa CCM, Mheshimiwa Msekwa ameshika nafasi
nyingi za madaraka katika Serikali na siasa ikiwa ni pamoja na kuwa
Katibu wa Bunge, Makamu wa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Katibu
Mtendaji wa chama cha TANU, Mtendaji Mkuu wa CCM, Katibu Mkuu Ofisi ya
Waziri Mkuu, na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Rais
Kikwete yuko katika ziara ya siku tatu mjini Mwanza ambako leo alikuwa
Mgeni Rasmi kwenye Sherehe za Miaka 35 ya CCM zilizofanyika kwenye
Uwanja wa CCM, Kirumba.
Mwisho.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
No comments:
Post a Comment