TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Wednesday, January 9, 2013

RAIS MSTAAFU MZEE MWINYI AFUNGUA SKULI MPYA YA MAPINDUZI,CHAANI ZANZIBAR

 
Rais mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mzee Ali Hassan Mwinyi akifungua Skuli mpya ya ,Sekondari ya Mapinduzi Chaani ikiwa ni shamra shamra za kuadhimi miaka 49 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
PICHA NA MAKAME MSHENGA-MAELEZO ZANZIBAR.
…………………………………………………….
NA RAMADHANI ALI /MAELEZO
 Rais mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mzee Ali Hassan Mwinyi amesema Zanzibar ni miongoni mwa nchi chache Duniani zinazoendelea kutoa Elimu bila malipo tokea kuasisiwa Mapinduzi matukufu ya mwaka 1964.
 Akizungumza katika ufunguzi wa Skuli mpya ya Sekondari ya Mapinduzi, Chaani katika maadhimisho ya sherehe za kutimiza miaka 49 ya Mapinduzi ya Zanzibar, Mzee Mwinyi amesema mafanikio hayo yanatokana na viongozi shupavu wa Mapinduzi na wale waliofuatia kuongoza Zanzibar.
 Amewapongeza viongozi na wananchi  wa Zanzibar kwa jumla kwa kuendeleza malengo  ya Mapinduzi ya 1964 ya kuimarisha maendeleo katika nyanja mbali mbali.
 Rais mstaafu amewahimiza wananchi kuendeleza Umoja kwani bila umoja na mshikamano hakuna maendeleo yatakayopatikana.
 Amewashukuru wahisani wanaosaidia   maendeleo ya Zanzibar hasa katika nyanja ya elimu na afya na amesema misaada yao itaendelea kuthaminiwa .
 Amewataka wazee wa Chaani kuendelea kuwasimamia watoto wao na kuhakikisha wanaitumia skuli hiyo katika kubadilisha uwezo wao wa kusoma kuwa bora zaidi.
 Akizungumza katika sherehe hiyo, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Ali Juma Shamhuna amesema baada ya kupata msaada wa  skuli mpya 19 za sekondari na Benki ya Dunia na skuli mbili msaada wa BADEA, Wizara yake inatilia mkazo katika kuondosha tatizo la walimu wa sayansi linalokabili Skuli nyingi za Zanzibar.
 Amesema  Nigeria imewapatia msaada wa walimu 13 wa sayansi na tayari wamefanya mazungumzo na nchi ya Marekani, Uingereza, Ghana, India, Palestina, Misri na Oman na wote wameonyesha azma ya kusaidia kupunguza tatizo hilo.

TABOA YAMPONGEZA WAZIRI DK. EMMANUEL NCHIMBI KWA UAMUZI WA KUPUNGUZA VITUO VYA UKAGUZI

 
CHAMA cha Wamiliki wa Mabasi Tanzania(TABOA) kimepongeza hatua zilizochukuliwa na Waziri wa Mambo ya Ndani Dk Emmanuel Nchimbi kupunguza kero katika usafiri wa mabasi iliyokuwa ikichangiwa na wingi wa vituo vya ukaguzi vilivyopo katika maeneo mbalimbali nchini.
Aidha kimemtaka Waziri huyo kudhibiti tabia inayofanywa na  baadhi ya mabasi yasiyo na leseni za usafirishaji, kusafirisha abiria kinyume na utaratibu uliopo,jambo alilosema litasaidia  kupatiakana kwa haki za abiria pindi tatizo lolote litakapotokea.
Akizungumza na waandishi wa habari jana,Katibu wa Taboa Enea Mrutu alisema  hivi karibuni walimuomba Waziri huyo kuyafanyia kazi baadhi ya mapungufu yaliyoyopo barabarani, ikiwemo ya kupunguza vituo vya ukaguzi, jambo alilosema kuwa amelitekeleza kikamilifu na hivyo kuwaondolea usumbufu uliokuwepo.
Alisema mbali na kero hiyo pia Nchimbi amefanikiwa kudhibiti tabia ya baadhi ya askari waliokuwa na tabia ya kujificha vichakani na kujitokeza ghafla barabarani pindi wanapoona basi  limekalibia na kuliandikia faini  kwa madai kuwa lilikuwa katika mwendo mkali.
“Tunashukuru siku chache baada ya kulilalamikia suala hili na kumuomba Waziri kulifanyia kazi, tayari majibu yake tumeyaona na tunawaomba viongozi wengine wawe mfano wa viongozi hawa ambao mara nyingi hufanyia kazi kero zinazofikishwa mbele yao” alisema Mrutu.
Aidha alisema kumekuwepo na mabasi katika mikoa mbalimbali yanayofanya kazi ya kusafirisha abiria bila kuwa na leseni za usafirishaji, jambo alilosema ni hatari pindi ajali inapotokea na hivyo kumtaka waziri kulisimamia suala hilo kupitia kitendo cha usalama barabarani.

RAIS WA ZANZIBAR DK ALI MOHD SHEIN AFUNGUA KATUO CHA KURUSHIA MATANGAZO YA DIJITALI ZANZIBAR

 
Rais wa Zanzibar Dk Ali Mohd Shein akikata Utepe kuonyesha Ufunguzi wa Kituo Kikuu cha Kurushia Matangazo ya Dijitall huko Rahaleo Mkoa wa Mjini Unguja.ikiwa ni Shmra shamra za Kuadhimisha Sherehe za Kutimia Miaka 49 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
PICHA NA YUSSUF SIMAI -MAELEZO ZANZIBAR.
 
Kituo kikuu cha Mtambo wa Kurushia Matangazo ya Dijitall kilichofunguliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza La Mapinduzi huko Rahaleo Mkoa wa Mjini Unguja.ikiwa ni Shmra shamra za Kuadhimisha Sherehe za Kutimia Miaka 49 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
 
Rais wa Zanzibar Dk Ali Mohd Shein wapili kushoto akipata maelezo mafupi kwa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Agape Association LTD Dr Vernon Fernandes wakwanza kuli kuhusiana na Chanall za Dijitall zinavyofanya kazi,baada ya Rais kufungua Kituo Kikuu cha Kurushia matangazo ya Dijitall hapo Rahaleo Mjini Zanzibar.wapili kulia ni Waziri wa Habari Utamaduni Utalii na Michezo Said Ali Mbarouk.
 
Rais wa Zanzibar Dk Ali Mohd Shein katikati akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Wizara ya Habari Utamaduni Utalii na Michezo na Mainjinia wa Ujenzi wa Kituo Kikuu cha Kurushia matangazo ya Dijitall hapo Rahaleo Mjini Zanzibar.
…………………………………………………….
Na Khadija Khamis –Maelezo Zanzibar  
 SHIRIKA la Utangazaji  Zanzibar ZBC limetakiwa kuhakikisha kwamba linafanyakazi kwa ufanisi mkubwa kulingana na mfumo uliopo hivi sasa.
Alisema kuwa wafanyakazi wa shirika hilo wameonakana wakifanya kazi kimazowea tu bila kufuata taratibu za kikazi.  
Hayo yameelezwa leo na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi  Dkt Ali Mohammed Shein katika Uzinduzi wa Miundombinu ya Dijitali na Jengo la Studio ya Kisasa
Alisema kuwa kubadilika kwa watendaji kazi ni suala la lazima kutokana na mabadiliko makubwa yalioko duniani .
Dkt Shein alisema kuwa ZBC wananchi wengi wanapiga kelele juu ya utendaji wa wafanyakazi wa ZBC kutokana na  vipindi vyao kutoridhisha na kukatika katika kwa matangazo yao zaidi wakati wa taarifa ya habari.
Alisema kuwa Zanzibar inaheshima yakekatika masuala ya Utangazaji kwani Redio nyingi za Nje zinawatangazaji kutoka Zanzibar ambao ni mahiri katika masuala ya Utangazaji.
Dkt Shein amesema kuwa hivi sasa hatoweza kuvumilia tena kutokana na utendajihuo ambao hauridhishi hata kidogo na hasa sasa tulivyoingia katika mfumo huu wa DIGITALI.
 “Sitaki kuiona Serikali ambayo nnayoiongoza mie iwe ‘tiro’(mwisho) alisema Dkt Shein.
Alisema kuwa kuingia katika mfumo mpya wa dijitali ni kazi kubwa lazima watendaji wafanyekazi kwa mashirikiano na kuwe na uwiano baina yao ili kuweze kuwa na kiwango ambacho kitaweza kuwajengea sifa wafanyakazi hao.

TUME YA MABADILIKO YA KATIBA YAENDELEA KUKUTANA NA VYAMA VYA SIASA

Mwenyekiti wa Chama cha Kijamii (CCK), Constantine Makitanda akizungumza katika mkutano uliofanyika katika Viwanja vya Karimjee Jijini Dar es Salaam na Wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba mara baada ya  Chama hicho kuwasilisha maoni yao kuhusu Katiba Mpya leo (Jumanne Januari 8, 2013).
 
Katibu wa Chama cha Union for Multiparty Democracy (UMD),Ndg.  Juma  akizungumza wakati wa mkutano uliofanyika leo (Jumanne Januari 8, 2013) baina ya Chama hicho na Tume ya Mabadiliko ya Katiba, ambapo Chama hicho kiliwasilisha maoni yao kuhusu Katiba Mpya. Kulia ni Kulia ni Mwenyekiti wa Tume hiyo, Jaji Joseph Warioba na Katibu wa Tume,Assaa Rashid.
 
Baadhi ya Viongozi wa Chama cha Union for Multiparty Democracy (UMD) wakifuatilia mkutano baina yao na Tume ya Mabadiliko ya Katiba leo( Jumanne Januari 8, 2013), ambapo Uongozi wa Chama hicho uliwasilisha maoni ya Chama hicho kuhusu Katiba Mpya.
 
Katibu Mkuu wa Chama cha Wakulima (AFP), Rashidi Mohamed akiwasilisha maoni yao kuhusu Katiba kwa Wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba katika mkutano uliofanyika katika Viwanja vya Karimjee Jijini Dar es Salaam leo (Jumanne, Januari 8 2013).
 
Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Mhe. Raza Hamad akizungumza  katika mkutano na Viongozi wa Chama cha Wakulima (AFP) uliofanyika katika viwanja vya Karimjee Jijini Dar es Salaam wakati Chama hicho kilipowasilisha maoni yao kuhusu Katiba Mpya leo (Jumanne Januari 8, 2013).
 
Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Dk. Salim Ahmed Salim akizungumza katika mkutano na Viongozi wa Chama cha Kijamii (CCK) uliofanyika katika Viwanja vya Karimjee Jijini Dar es Salaam wakati Chama hicho kilipowasilisha maoni yao kuhusu Katiba Mpya leo (jumanne Januari 8, 2013).
 
Mjumbe Wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Ndg. Ussi Khamis akizungumza katika mkutano na Viongozi wa Chama cha Kijamii (CCK) uliofanyika katika Viwanja vya Karimjee Jijini Dar es Salaam wakati Chama hicho kilipowasilisha maoni yao kuhusu Katiba Mpya leo (jumanne Januari 8, 2013).

Dkt. Mgimwa avutiwa na vijiji 16 vya mfano vya utelezaji wa mradi wa malengo ya Milenia



Waziri wa Fedha Dkt William Mgimwa akikata utepe wa uzinduzi wa maabara ya kisasa iliyogharimu milioni 49 ikiwa ni sehemu ya mradi wa vijiji vya Milenia wa Mbola  jana wilayani Uyui wakati  Waziri huyo alipotembelea Wilaya hiyo kuona mradi wa mfano ulivyoboresha maisha ya wananchi katika vijiji 16 zinavyoteleza mradi huo. Kulia ni Mwenyekiti wa Halmashauri  ya Uyui Said Shaban Ntahondi na kushoto  ni Mbunge wa Jimbo Tabora Kaskazini Mamlo Shafin Sumar na wapili kutoka kushoto ni Kiongozi wa Mradi wa Vijiji vya Milenia wa Mbola Dkt Gerson Nyadzi.
 PICHA na GCU – HAZINA
Waziri wa Fedha Dkt William Mgimwa(kushoto) akiongea na viongozi wa vijiji 16 vinavyotekeleza  mradi wa vijiji vya Milenia wa Mbola  jana wilayani Uyui juu ya kuufanya mradi huo kuwa darasa endelevu kwa ajili ya vijiji vingine nchini kwenda kujifunza juu ya utekeleza wa malengo 8 ya Milenia . Waziri huyo alitembelea Wilaya hiyo kuona mradi wa mfano ulivyoboresha maisha ya wananchi katika vijiji 16 zinavyoteleza mradi huo. Katikati ni Mwnyekiti wa Halmashauri  ya Uyui Said Shaban Ntahondi na kulia ni Mwenyekiti wa Kijiji cha Ilolangulu Ally Magoha.
…………………………………………….

Na Mwandishi wetu -GCU-Hazina- Uyui- Tabora
Waziri wa Fedha Dkt William Mgimwa amewataka wakazi wa Wilaya ya Uyui mkoani Tabora  waliopo katika wa utekelezaji malengo ya Milenia chini ya mradi wa vijiji vya Milenia wa Mbola kuufanya mradi huo kuwa endelevu kwa kutunza vizuri miradi yote iliyoibuliwa kwa ajili ya uboreshaji wa maisha ya wananchi wa eneo hilo .
Waziri huyo alitoa kauli hiyo jana wilayani Uyui mkoani Tabora mara baada ya kuzindua maabara iliyochini ya mradi huo ambayo imegharimiu shilingi milioni 49 hadi kukamilika.
Alisema kuwa ni vema wananchi hao wakahakikisha miradi yote iliyotekelezwa chini ya mradi wa vijiji vya milenia wa Mbola inatunza vizuri ili iwe darasa la kufundishi vijiji vingine hapa nchini katika utekelezaji wa malengo 8 ya milenia.
Dkt. Mgimwa aliongeza kuwa itasikitisha kuona kuwa mara baada ya muda wa mradi kuisha wa 2006-2012 na wafadhili ambao ni Milenia Promise Tanzania kumaliza muada wao na miradi inakufa na kusema kuwa hatua hiyo haitakuwa nzuri.
Aidha alitoa wito kwa wanavijiji wengine ambao hawapo katika mradi huo kwenda katika Kijiji cha Ilolanguru wilayani Uyui ili wajifunze jinsi ya utekelezaji wa malengo ya Milenia kwa kutumia juhudi za wananchi.
Awali akitoa taarifa kwa Waziri wa fedha, Mwenyekiti wa Kijiji cha Ilolangulu Ally Magoha alisema kuwa  katika utekelezaji malengo ya Milenia chini ya mradi wa vijiji vya Milenia wa Mbola wameweza kuboresha maisha yao katika vijiji 16 katika eneo hilo.
Alitaja manufaa waliyokwishapata ni pamoja na ujenzi wa nyumba za kisasa kwa kutumia matofali ya kuchoma na bati na kuongeza uzalishaji wa mazao ya chakula na fedha.
Mogoha aliongeza kuwa pia mradi huo umewawezesha kupunguza tatizo la vifo vya watoto waliopo chini ya maika 5 na mamawajawazito ambapo awali vifo vilikuwa wastani wa watoto watatu(3) hadi watano (5) na wanawake wajawazito 3 hadi 5 katika kipindi cha miezi mitatu lakini hivi sasa vifo ni wastani huo katika kipindi cha miezi sita na wakati mwingine hakuna.
Alisema kuwa hatua hii imefikiwa mara baada ya kuwaelimisha wananchi juu ya kutumia vyandarua na kuua mazalia ya mbu na hivyo kupunguza malaria katika eneo hilo.
vilevile Mwenyekiti huyo aliongeza kuwa kiwango cha wanafunzi wanaoishia njia(drop out) kimepungua mara baada ya mradi huu kuanza kwani mbinu mbalimbali zimesaidia watoto wengi kumaliza darasa la saba .
Mbinu hizo ni pamoja na kutoa chakula kwa wanafunzi na kuhamasisha michezo mashuleni jambo liliwavutia watoto wengi.
kuhusu suala la maji alisema wanaendelea vizuri ambapo wastani wa asilimia 60 ya wakazi wa eneo hilo wanapata maji safi na salama.
Mradi wa vijiji vya Milenia wa Mbola unatelelezwa katika vijiji vya Ilolanguru, Isenga, Ngokolo, Ulimakafu, Mpenge, Isila, Mbola, Kasisi A, Mabama, Ideka, Mbiti, Msiliembe, Iberi, Inonalwa, Usagari, Msima na Migungumalo.

IBF YAAWAALIKA WAFANYABISHARA WA KITANZANIA BERLIN, UJERUMANI

 


Shirikisho la Ngumi la Kimataifa (IBF) katika bara la Afrika, Ghuba ya Uajemi na Mashariki ya Kati linawaalika wafanyabishara wa kitanzania kuhudhuria mkutano wa mwaka wa IBF/USBA utakaofanyika katika jiji la Berlin nchini Ujerumani kuanzia tarehe Mei 21-25th, 2013.
 Katika mkutano huo wanachama zaidi ya 3000 wa IBF/USBA kutoka nchi zaidi ya 200 duniani watahudhuria.
 Hii ni fursa pekee kwa wafanyabishara wa Kitanzania kuweza kutumia mkutano huu kutangaza biashara zao katika sekta mbalimbali hususan sekta ya Kitalii, TEHAMA, usafirishaji wa bidhaa za kitanzania nje ya nchi pamoja na uwekezaji katika sekta mbalimbali nchini.
 Mkutano wa mwaka wa IBF/USBA huwakutanisha wafanyabishara waliowekeza katika sekta mbalimbaki za kiuchumi na hutoa fursa kubwa kwa wafanyabishara kujenga mitandao mzuri wa biashara.
 Rais wa Rais wa IBF katika bara la Afrika, Ghuba ya Uajemi na Mashariki ya Kati Mtanzania Onesmo Ngowi anawahimiza Watanzania kuchangamkia fursa hizi ili waweze kufaidika kiuchumi,
 Aidha, Ngowi anawahamasisha wakuzaji wa mchezo wa ngumi pamoja na wale wanaofanya shughuli za Branding (kukuza biashara) kuhudhuria mkutano huu na kujipatia fursa mbalimbali za biashara.
 Ngowi ataongoza ujumbe nzito kutoka bara la Afrika, Ghuba ya Uajemi na Mashariki ya Kati wakiwamo Mawaziri wa Michezo kadhaa kutoka nchi zilizo katika ukanda huu.