TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Wednesday, June 13, 2012

Akili za wasomi zitumike kuendeleza sekta ya elimu

Posted: 12 Jun 2012 12:52 AM PDT

Posted: 12 Jun 2012 12:48 AM PDT

Na Willbroad Mathias

MWISHONI mwa wiki  Waziri wa Mambo ya Nje, Bw. Bernard Membe, aliwakaribisha nyumbani kwake viongozi wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na kula nao chakula cha mchana.

Wakati wa chakula hicho alizungumza na viongozi hao masuala mbalimbali ya kisiasa ukiwemo mwenendo wa upepo wa kisiasa nchini.

Katika mazungumzo hayo Bw. Membe alikitabiria ushindi CHADEMA katika uchaguzi mkuu unaokuja na akasema kwamba chama hicho kimetokea kupendwa na wananchi katika kila kona ya nchi na hata operesheni yao ya Kusini imekitikisa chama tawala.

Viongozi hao waliookutana na Bw.Membe ni Mjumbe wa Kamati  Kuu, Bw. Godbless Lema, aliyekuwa Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Arusha kabla ya kuhamia CHADEMA, Bw.James Millya na viongozi wakuu waandamizi.

Waziri Membe aliwaambia viongozi hao kwamba ameishi nchi mbalimbali duniani zenye demokrasia ya hali ya juu hivyo hatashangazwa hata kidogo kama CHADEMA itaingia Ikulu.

Katika mazungumzo hayo Bw. Membe alienda mbali zaidi na kugusia  kesi iliyotengua ubunge wa Bw. Lema  ambapo alidai kushtushwa na kusema kwa vile amekata rufaa anaamini mahakama ya rufaa itamrejeshea ubunge wake.

Kwa kitendo hicho nashawishika kumpongeza  Bw.Membe  kwani  ameonesha kukomaa kisiasa na anastahili kuwa mfano wa kuigwa na wanasiasa wengine nchini.

Mbali na kumpongeza  naweza kusema kuwa ameonesha ushujaa  kwa kusema ukweli  kwani ni wachache ndani ya CCM ambao wanaweza kusimama wakaeleza ukweli huku wakifahamu chama kinakoelekea siko.

Wana CCM wenye moyo wa dhati na chama wanatambua kuwa hali ya upepo kwa sasa ndani  ya chama sio shwari kutokana na wimbi  la wanachama wake kukimbilia CHADEMA, lakini ni wachache wanaoweza kutamka hili japo  moyoni wanajua ukweli wengine wanashindwa kutamka kwa kuhofia ugali wao, wengine kuhofia posho, huku hali halisi inaonekana wazi.

Kwa kuamua kuwa muwazi, Bw.Membe ameongea yaliyo moyoni mwake na pia, ameonesha busara, hata kuna baadhi ya mawaziri na wabunge kama Ezekiel Maige amewahi kutoa kauli kama hii zaidi ya mara moja.

Na kwa kufanya hivyo, basi ni mtu mkweli asiyetaka kuficha ukweli kwa mgongo wa kukipendezesha chama kinachoshindwa kuangalia maslahi ya umma, ubinafsi na umimi, hivyo hakuna haja ya kumshambulia.

Nasema hivyo kutokana na kwamba hakuna mtu anayekuwa mtenda dhambi wa milele, isipokuwa sheteni, huongea maneno yenye upako wa Mungu, tuyaheshimu na kuyafanyia kazi kwa tahadhali ya hali ya juu.

Nashawishika kusema hivyo  kutokana na kwamba kwa hapa nchini, nina uhakika itakuwa ni mara ya kwanza kwa mbunge kuwaalika wapinzani nyumbani kwake na kuwaandalia chakula huku akiwapa maneno ya faraja kama hayo.

Hii ni kutokana na kuwa baadhi ya wanasiasa ambao wamekuwa wakichukulia siasa kama uhasama huku wakiwabeza wapinzani kwamba hawana uwezo wa kuingia Ikulu, licha ya kuelewa uwezo mkubwa waliokuwa nao baadhi ya viongozi wa vyama vya upinzani.

Hali hiyo imekuwa ikitokana na baadhi ya wanasiasa  kutojiamini wakidhani endapo utamkaribisha kiongozi ama mwanachama wa upinzani nyumbani kwako utakuwa unaliweka jimbo lako rehani.

Imani hiyo ndiyo imekuwa ikiwafanya baadhi ya wanasiasa  kujenga fitina miongoni mwa wafuasi wao ili wawachukie wapinzani.

Pia imani  hiyo  imekuwa ikiwafanya kujiona miungu watu huku wakiwaona wapinzani kama maadui ambao muda wote wanatishia kukitia mchanga kitumbua chao.

Kwa sasa taifa letu linakabiliwa na  hali ngumu kiuchumi iliyosababisha pia kupanda kwa gharama za maisha ,lakini wapo wapinzani ambao wamekuwa wakitoa maoni yao yenye mwelekeo wa kulinusuru taifa, lakini matokeo yake wamekuwa wakionekana kuwa maadui kwa baadhi ya wanasiasa, wakati wangeweza kuwasaidia kufikia malengo.

Nichukue fursa hii kuwaomba viongozi wengine wa siasa kulitambua jambo hilo la kuwa upinzani siyo uhasama bali ni chachu ya kusukuma mbele gurudumu la maendeleo.

Viongozi wakikubali changamoto katika siasa hawataweza kuchukiana bali kujengana  kisiasa na kuongeza mshikamano baina yao.

Hii itawasaidia pia kusimama palipo na ukweli kwa maslahi ya wananchi na kuweka itikadi za kivyama mbali.

Siasa isichukuliwe kama uhasama ambao unaweza kuzaa migogoro isiyoisha, mnatakiwa kukaa pamoja na kujadili ni kwa jinsi gani mtatoa tulipo.

Hakuna kitu kinachonisikitisha ninapowaona wanasiasa wakongwe wakipanda jukwaani na kulumbana badala ya kutoa hoja za msingi kwa wananchi za utatuzi wa matatizo yaliyopo.

Tumechoshwa na siasa za uadui, siasa ni urafiki na kuiga mazuri anayofanya ama aliyofanya mwenzako hadi kukubalika na kupewa ridhaa na wananchi wake.

Hongera sana waziri Membe umekuwa  mfano wa kuigwa, wengine wafuate nyayo hizo.
Posted: 12 Jun 2012 12:40 AM PDT

Waimbaji wa bendi ya muziki wa dansi ya Msondo Music, wakiimba Dar es Salaam mwishoni mwa wiki kutoka kushoto ni Eddo Sanga, Muhidini Gurumo na Juma Katundu. Picha na Rajabu Mhamila

Posted: 12 Jun 2012 12:37 AM PDT

Na Mwandishi Wetu

KAMPUNI ya Bia Tanzania (TBL), kupitia bia yake ya Safari Lager imekabidhi vitendea kazi mbalimbali kwa wajasiriamali 11 walioshinda kupewa ruzuku za Safari Wezeshwa vyenye thamani ya sh. milioni 50.

Akizungumza katika sherehe za makabidhiano ya vifaa hivyo jijini Arusha jana katika viwanja vya Soweto Meneja wa Safari Lager, Oscar Shelukindo alisema mashindano hayo ya Wezeshwa na Safari Lager nia yake kubwa ni kuwapatia ruzuku wajasiriamali wadogo na wakati kuendeleza biashara zao.

Shelukindo alisema jumla ya sh. milioni 50 zimetumika katika kununulia vifaa hivyo kwa Kanda ya Kaskazini, ambapo mwaka 2011 ruzuku ilikuwa ni milioni 200 kama vifaa vya vitendea kazi kwa wajasiriamali hao walioshinda katika mashindano hayo.

Alisema utaratibu huo huo ulianzia Mbeya na Arusha na wanatarajia wiki ijayo kuwa Mwanza na mwisho watamalizia Dar es Salaam.

Naye Mgeni rasmi katika sherehe hizo, Niarire Magunda ambaye ni Ofisa Biashara Manispaa ya Arusha, aliipongeza TBL kupitia bia yake ya Safari Lager kwa kuanzisha programu hiyo yenye nia ya kuwasaidia wajasiriamali wadogo na wakati.

Katika sherehe hizo wajasiriamali 11 kutoka Arusha, Moshi na Tanga walikabidhiwa vifaa mbalimbali vya vitendea kazi.

Posted: 12 Jun 2012 12:35 AM PDT

Bondia Nassibu Ramadhani (kushoto) na Fadhili Majia wakioneshana ufundi wa kutupa masumbwi wakati wa pambano lao la ubingwa wa Taifa. Ramadhani alishinda kwa point. Picha na Rajabu Mhamila

Posted: 12 Jun 2012 12:31 AM PDT

Na Zahoro Mlanzi

MCHEZO wa timu ya Taifa (Kilimanjaro Taifa Stars) na Gambia, uliochezwa juzi Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, umeingiza sh. 124,038,000.

Mechi hiyo ilikuwa ni ya Kundi D ya kuwania kufuzu kucheza Kombe la Dunia 2014 nchini Brazil, ambapo wenyeji Kilimanjaro Taifa Stars iliibuka na ushindi wa mabao 2-1.


Timu zingine za kundi hilo ni Ivory Coast na Morocco, ambazo nazo zilifungana kwa mabao 2-2.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari Dar es Salaam jana na Ofisa Habari wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Boniface Wambura ilieleza kwamba mapato hayo yametokana na washabiki 31,122 waliokata tiketi kushuhudia pambano hilo.

"Asilimia 18 ya mapato hayo ambayo ni sh. 18,921,050.85 ilikwenda kwenye Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) wakati gharama kabla ya mgawo zilikuwa (sh. 6,555,000) na bonasi kwa Taifa Stars (sh. 15,767,542.37)," alisema Wambura.

Alisema waamuzi sh. 13,372,000, usafi na ulinzi sh. 2,350,000, maandalizi ya uwanja ni sh. 400,000, Wachina ni sh. 2,000,000, umeme sh. 300,000 na mafuta ya jenereta sh. 200,000.

Aliongeza kwa upande wa mgawo asilimia 20 ya gharama za mechi ni sh. 12,834,481, asilimia 10 ya uwanja sh. 6,417,241, asilimia 5 ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) sh. 3,208,620, asilimia 20 ya Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 12,834,481 na asilimia 45 ya TFF (sh. 28,877,583).

Wakati huohuo, Waamuzi 54 wameanza kozi ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) jana Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa Wambura, alisema kozi hiyo itamalizika Juni 14, mwaka huu na inaendeshwa na wakufunzi wawili kutoka FIFA wakisaidiwa na wakufunzi wengine wanne wa TFF. Wakufunzi wa FIFA ni Carlos Henriques na Mark Mizengo.

Wakufunzi kutoka TFF ni Kapteni mstaafu Stanley Lugenge, Leslie Liunda, Soud Abdi na Riziki Majala.
Posted: 12 Jun 2012 12:29 AM PDT
Vyakula vya kuoka maarufu kama burgers ambavyo vimeelezwa kuwa na madhara katika afya ya binadamu.

Posted: 12 Jun 2012 01:28 AM PDT


Darlin Said na Radhia Adam

TAASISI ya Mawasiliano (TCRA), imeliomba Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) kuhamasisha wasanii kuongeza na kuboresha vipindi vyao, ili viweze kuleta maendeleo ya nchi katika tasnia ya sanaa na utamaduni.

Ombi hilo limetolwea na Mhandisi Mwandamizi wa masafa TCRA, Joel Chacha katika kongamano lililohusu teknolojia ya dijitali na faida zake kwenye sekta ya sanaa na wasanii, lililowasilishwa kwenye jukwaa la sanaa liliofanyika Dar es Salaam jana.


Chacha alisema katika mabadiliko ya utangazaji kutoka analogi kwenda dijitali sekta ya sanaa na wasanii nchini, watafaidika kwa kutangaza kazi zao za usanii na kuutangaza utamaduni wa Mtanzania ndani na nje ya nchi.

"Kupitia mabadiliko haya ya sanaa, Tanzania itapata soko kwa njia iliyo rahisi na kuwatangaza wasanii nje ya mipaka yetu, pamoja na kuutangaza utamaduni wetu na pia wasanii watapata ajira mbalimbali kutokana na kuongezeka kwa kampuni za sanaa," alisema.

Mbali na faida hizo, baadhi ya wasanii waliohudhuria kongamano hilo wameulalamikia mfumo huo mpya kutokana na changamoto watakazokumbana nazo ikiwemo upoteaji wa kazi zao za filamu na utamaduni wa Mtanzania.

"Kupitia mfumo wa dijitali, ambao unalenga kutumia ving'amuzi itakuwa rahisi kwa mtu wa nje ya nchi kuiba sanaa zetu kwa kunyonya kazi zetu na kwenda kutumia katika nchi zao," alifafanua Surchyang Raphael ambaye ni msanii na Mwenyekiti wa TASA, Ilala.

Naye msanii kutoka kundi la Kashkash, Amos Beda aliulalamikia mfumo huo kwa kusema kwamba mfumo huo ni wa gharama kwa mwananchi wa kawaida kuweza kuumudu katika kununua king'amuzi na kulipia gharama za uendeshaji.

Wakizungumza katika changamoto za mfumo wa dijitali wasanii hao, waliiomba TCRA kusimamia kudhibiti mfumuko wa bei ya ving'amuzi na pia kudhibiti uingiaji wa aina tofauti za ving'amuzi, ili iwe rahisi kwa mwananchi kumiliki king'amuzi kiurahisi zaidi ambacho kitaonesha chaneli zote.

Mfumo wa digitali ulizinduliwa rasmi Agosti mwaka jana na Rais Jakaya Kikwete, ambao ulienda sambamba na uzinduzi wa nembo ya dijitali kwa ambao utekelezaji wake unatarajiwa kuanza rasmi Januari 2013.
Posted: 12 Jun 2012 12:17 AM PDT

Posted: 12 Jun 2012 12:16 AM PDT


Na Elizabeth Mayemba

KAMATI ya Uchaguzi ya Yanga, jana ilitangaza majina ya wagombea wa uchaguzi mdogo wa klabu hiyo ya kujaza nafasi za waliojiuzulu baada ya kupitia vyeti vyao, hivyo yatabandikwa ubaoni keshokutwa ili kutoa nafasi kwa wale wenye pingamizi.

Uchaguzi huo unatarajiwa kufanyika Julai 15, mwaka huu.

Akizungumza Dar es Salaam jana Katibu wa kamati hiyo, Francis Kaswahili alisema kati ya majina 29 ya walioomba kugombea nafasi mbalimbali za uongozi, Abdallah Sharia ambaye ni mkazi wa Zanzibar vyeti vyake hakuwasilisha hivyo ametakiwa kufanya hivyo kabla ya usaili, baada ya mwenyewe kuiomba kamati.

Kaswahili alisema mgombea Mohammed Mbaraka, yeye ameondolewa katika kinyang'anyiro hicho kwa kuwa hana sifa.

Kwa upande wa wanaogombea nafasi ya Mwenyekiti wote wanne wamepita, ambao ni Yusuf Manji, John Jambele, Edgar Chibura na Sarah Ramadhan kwa nafasi ya Makamu Mwenyekiti waliopita ni Ayoub Nyenzi, Clement Sanga, Yono Kevela na Ally Mayai.

Wajumbe waliopita ni Lameck Nyambaya, Ramadhani Kampira, Mohamed Mbaraka 'Binkleb', Ramadhan Said, Edgar Fongo, Ahmed Gao, Beda Tindwa, Jumanne Mwamenywa na George Manyama.

Wengine ni Gadeuncius Ishengoma, Haron Nyanda, Omary Ndula, Shaban Katwila, Justine Baruti, Jamal Kisongo, Peter Haule na Stanley Kevela 'Yono'ambaye pia anagombea nafasi ya Makamu Mwenyekiti.

Kaswahili alisema pingamizi kwa walioomba kugombea uongozi litaanza kutolewa Juni 14 hadi 18, mwaka huu na baada ya hapo Kamati za Yanga na TFF zitakaa kupitia pingamizi hizo.

"Tunatoa hadhari kwa wale wote ambao wataleta pingamizi zao wawe na ushahidi wa kutosha, kinyume na hapo hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao," alisema Kaswahili.
Posted: 12 Jun 2012 12:13 AM PDT
Mkuu wa Chuo cha Aseki Dodoma, Bw. Omari Kiputiputi akizungumza katika mahafali ya kwanza ya chuo hicho yaliyofanyika hivi karubuni, ambapo wahitimu mbalimbali walitunikiwa vyeti katika fani za biashara, kushoto ni Mwenyekiti wa bodi ya mitihani ya chuo hicho, Balozi Job Lusinde na Mwenyekitu wa Bodi ya Wakurugenzi wa chuo hicho,Dk. Richard Mushi. (Picha na Mpiga Picha wetu)
Posted: 11 Jun 2012 11:58 PM PDT

Na Willbroad Mathias

ILI Tanzania iwe na maendeleo endelevu lazima kujenga utamaduni wa kujiendeleza kimasomo hasa katika fani za biashara na ujasiriamali.

Kwa kufanya hivyo, watakuwa wamejirahisishia mazingira ya kumudu ushindani unaolikabili soko la ajira ndani na nje ya nchi. Hakuna njia ya mkato zaidi ya watu kuwekeza katika sekta ya elimu.

Changamoto hiyo ndiyo imewafanya watanzania wengi kuwekeza katika elimu.

Mkuu wa Chuo Cha Biashara cha Aseki cha mkoani Dodoma,  Bw. Omari Kiputiputi, wakati akizungumzia maendeleo ya elimu na changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta hiyo pamoja na umuhimu wa ujasiriamali.

Bw. Kiputiputi anasema ni mhitimu wa Shahada ya Elimu ya Chuo kikuu cha Dar es Salaam mwaka 1979 na pia ana Shahada ya pili ya usimamizi wa biashara akiwa amebobea zaidi upande wa masoko MBA aliyopata mwaka 1998.

Anasema baada ya kuhitimu shahada ya ualimu wa masomo ya sayansi mwaka 1979 katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam aliajiriwa na Chuo cha Biashara Dar es Salaam CBE na kufanya kazi katika chuo hicho kwa miaka 31 ambapo alistaafu kwa mujibu wa sheria mwaka 2010.

Anasema, miaka 10 ya mwisho licha ya kuendelea na kazi ya ufundishaji alipewa dhamana ya kuwa Makamu Mkuu wa Chuo cha CBE Dodoma.

Bw.Kiputiputi anasema, akiwa katika nafasi hiyo alikikuta kikiwa na wanafunzi 183, lakini hadi anaondoka aliacha wanafunzi zaidi ya 4,000.

"Uwezo wa kampasi ile ni wanafunzi 200 tu, lakini tuliweza kufanya yote haya kutokana na stadi za kijasiriamali," anasema.

"Nilipokea kampasi ile ikiwa inaendesha programu moja tu ya stashada katika fani tatu tu yaani uhasibu, uendeshaji biashara na uboharia, lakini nimeiacha kampasi ikiwa inaendesha programe tatu, cheti, stashahada na shahada katika fani tano za uhasibu, uendeshaji biashara, masoko, uboharia na TETAMA yaani Teknolojia ya Taarifa na Mawasiliano," anasema.

Anasema kwa kuwa alifanya kazi kwa bidii, utiifu, ubunifu na uadilifu mkubwa, alipostaafu mwajiri wake alimpa zawadi nyingi, ikiwemo cheti cha utumishi uliotukuka hivyo anawahimiza watanzania kujituma zaidi katika kufanya kazi.

Bw.Kiputiputi anasema, hata hivyo akiwa bado yupo kazini wazo lake kubwa lilikuwa ni kuanzisha chuo chake binafsi ili aweze kuwasaidia watanzania kufaidi matunda ya elimu yake.

Anasema kuwa hata hivyo ndoto zake zilikamilika mwaka jana baada ya kufanikiwa  kuanzisha chuo chake binafsi  cha Biashara cha Aseki cha mkoani Dodoma, ambapo anaahidi kutoa wahitimu bora wanaoweza kujiajiri wenyewe au hata kuajiriwa kila pembe ya dunia.

Anasema  kozi zinazofundishwa kuwa ni pamoja na cheti cha uhasibu, cheti cha uendeshaji wa biashara na cheti cha manunuzi na ugavi.

Bw. Kiputiputi anasema kwa upande wa stashahada wanatoa katika uendeshaji wa biashara, stashahada katika uhasibu na stashahada ya manunuzi na ugavi.

Anaongeza kuwa mwanafunzi yeyote aliyemaliza kozi ya cheti NTA 4 inayoendana na fani hizo kutoka kwenye chuo chochote kilichosajiliwa na NACTE au aliyemaliza kidato cha sita na kupata angalau 'pass' moja au 'subsidiary' pass mbili anaweza kujiunga na kozi ya stashahada.


“Tunajitahidi chuo hiki kiwe cha kipekee hapa nchini kwa kutoa wahitimu bora katika menejimenti, ujasiriamali na ujuzi kupitia mafunzo, utafiti, utumishi wa umma na huduma za kijamii katika kanda hii na hata nje ya mipaka ifikapo mwaka 2020,” anasema.

Anasema chuo kitahakikisha kinawaandaa wanafunzi katika misingi bora ya uendeshaji bora wa biashara wenye mafanikio makubwa kwa kuwatumia wanataaluma waliobobea katika gani husika.

Bw. Kiputiputi anasema chuo kimepata usajili kamili kutoka NACTE na hiyo inamaanisha kwamba mtu yeyote atakayesoma kwenye chuo hicho na kufanikiwa kupata cheti kitatambuliwa rasmi nchini na duniani kote.

Anasema ili kufikia malengo hayo wamedhamiria kutoa elimu ya kiwango cha juu na kwa gharama ambazo watanzania wengi wataweza kuzimudu katika kozi za usimamizi wa biashara, uhasibu na fedha, masoko, ugavi na manunuzi, masomo ya  kompyuta na kozi zingine zinazoendana na masomo hayo.

Anafafanua kuwa, iwapo wahitimu watapata mafunzo ya kiwango cha hali ya juu itarahisisha kupata maendeleo endelevu, kwani nchi itakuwa na wataalamu wa kutosha katika fani mbalimbali kama zinazotolewa na chuo hicho.

Ili Aseki ifikie malengo hayo, anasema wamepanga kufanya kazi kwa ushirikiano kama timu moja, kwa kuzingatia weledi wa taaluma, uadilifu, ubunifu, huduma kwa wateja na uwajibikaji wa pamoja.

Bw. Kiputiputi anawaomba watanzania kuchangamkia fursa ya kuanzishwa kwa chuo hicho kwa kuwa elimu ni ufunguo wa maisha pia hazina pekee kwa urithi wa baadaye.

Anasema wazazi au walezi ambao wana vijana waliomaliza kidato cha nne na kukosa sifa ya kuendelea na masomo ya kidato cha tano wasikate tamaa ili mradi tu wawe wamefaulu na kupata angalau alama tatu za D, hivyo wanaweza kujiunga na chuo hicho.

“Akija hapa sisi licha ya kumpa stadi muhimu za maisha tutampa pia sifa za kuweza kujiunga na chuo kikuu chochote nchini ndani ya miaka mitatu, tutampa stadi za kuweza kujiajiri yeye mwenyewe au kuajiriwa baada miaka hiyo mitatu ya kwanza endapo atashindwa au ataamua kutoendelea na masomo zaidi,” anasema, Bw. Kiputiputi.

Anasisitiza kuwa, “Tumepania kuwa kituo kilichotukuka, yaani kituo bora kwa kutoa elimu, mafunzo na stadi katika nyanja za biashara, uendeshaji na ujasiliamali kupitia mafunzo, utafiti, huduma kwa umma na shughuli za nje ya chuo katika kanda hadi kufikia mwaka 2020.”

Bw. Kiputiputi anasema walimu wote wa chuo hicho wana angalau shahada ya kwanza na stashahada ya juu, hivyo wahitimu wa chuo hicho wanakuwa na viwango vya elimu inayokubalika katika fani mbalimbali nchini.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Baraza la Chuo hicho, Dkt. Richard Mushi, anawahimiza watanzania kuwa na utamaduni wa kuanzisha miradi kwa ubia kwani ndiyo njia pekee ya kuanzisha miradi mkubwa.

Anasema wengi hawapendi kuanzisha miradi ya ubia kwa kutoaminiana, lakini aliwatoa hofu kuwa walioanzisha chuo cha ASEKI kwa ubia wamefanikiwa na chuo kinazidi kusonga mbele siku hadi siku.

“Waanzilishi wa chuo hiki wanastahili pongezi. Baraza linaona fahari kuongoza chuo hiki kwani licha ya kuanzishwa na watu binafsi, chuo kimetimiza masharti yote ya msingi ya kuandikishwa yaliyowekwa na Baraza la Vyuo vya Elimu ya Ufundi NACTE na ndiyo maana kimepata usajili kamili,” anasema Dkt. Mushi.

Anasema baraza la chuo limedhamiria kuona wakufunzi wa chuo hicho wanapata elimu ya ngazi ya juu zaidi ili waweze kumudu majukumu yao ipasavyo na wawe na viwango vinavyokubalika popote.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Baraza la Mitihani, Bw. Balozi Job Lusinde anasema Baraza lake limepania kuhakikisha linasimamia viwango vya juu vya taalum ili wahitimu watakaotoka Aseki wawe watu wa kupigiwa mfano.
Posted: 12 Jun 2012 12:14 AM PDT
Meneja Mawasiliano wa Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL), Imani Lwinga (kushoto)akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) jana kuhusu tuzo za Chama Cha Waandishi wa Habari za Michezo (TASWA) ambazo zitafanyika kesho. Katikati ni Mwenyekiti wa TASWA Juma Pinto na kulia ni Katibu Mkuu wa chama hicho, Amir Mhando.(Picha na Victor Mkumbo)
Posted: 11 Jun 2012 11:52 PM PDT

Na Zahoro Mlanzi

BENDI ya muziki wa dansi ya Extra Bongo 'Wazee wa kizigo', inatarajia kunogesha tuzo ya Mwanamichezo Bora 2011 wa Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA) zitakazofanyika Alhamisi kwenye Ukumbi wa Diomond Jubilee, Dar es Salaam.

Akizungumza Dar es Salaam jana na waandishi wa habari, Meneja Mawasiliano wa Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) ambao ndiyo wadhamini wa tuzo hiyo, Imani Lwinga alisema bendi hiyo itakasindika utoaji wa tuzo hizo kwa kutua burudani ya aina yake.

Alisema ana uhakika bendi hiyo itakonga nyoyo za wanahabari pamoja na watu mbalimbali watakaokuwepo siku hiyo.

"Tunatangaza rasmi kwamba bendi ya Extra Bongo ambayo ipo chini ya Ali Choki, ndiyo itakayotoa burudani siku hiyo, hivyo tunaomba wanamichezo, waandishi wa habari na wageni watakaoalikwa kujitokeza kwa wingi kuja kushuhudia tukio hilo kubwa kwa wanamichezo," alisema Lwinga.

Naye Mwenyekiti wa chama hicho, Juma Pinto aliishukuru kampuni hiyo kwa kuzidi kutekeleza waliyoahidi na kwamba kuhusu mgeni rasmi, watatangaza siku chache zijazo.

Mbali na hilo, alisema wanajipanga kuhakikisha wanajenga uhusiano na waandishi wa habari za michezo kwa Ukanda wa Afrika Mashariki, ambapo kwa mwaka jana walipata mwaliko wa kwenda kushuhudia tuzo katika nchi za Rwanda na Burundi.

Alisema kwa mwaka huu walipanga pia kuzialika baadhi ya nchi za ukanda huo, lakini walifanya jitihada za kuwapa ikashindikana kutokana na kubanwa na ratiba zingine.

Mwanamichezo bora kwa mwaka huu, anatarajiwa kupewa dola za Marekani 8,000 (sh. milioni 12 za Tanzania).

Pia kutakuwa na zawadi ya sh. milioni moja kwa kila mshindi wa kila mchezo.
Posted: 11 Jun 2012 11:50 PM PDT


Na Elizabeth Mayemba

TAWI la Chelsea nchini, limeandaa sherehe za kuipongeza timu ya Chelsea ambayo imenyakua ubingwa wa Klabu Bingwa Ulaya na Kombe la FA.

Akizungumza Dar es Salaam jana Katibu Mkuu wa Chelsea Tawi la Dar es Salaam, Cliford Ndimbo alisema sherehe hizo zimepangwa kufanyika Msasani Beach, Dar es Salaam Juni 24, mwaka huu.

"Tumeamua kuanzisha tawi letu la Chelsea hapa nchini, hivyo tumeona ni vyema tuipongeze timu yetu kwa vikombe hivyo ambavyo wamevipata, tunaamini sherehe zetu zitafana sana," alisema Ndimbo.

Alisema pia katika kunogesha sherehe hizo wamewaalika na wapenzi wa Manchester United na wale wa Arsenal, ambapo kutakuwa na mechi kati ya wapenzi wa Chelsea ambao watacheza na timu zote mbili na zawadi mbalimbali zitatolewa kwa washindi.

Ndimbo alisema wapo katika harakati za kusajili rasmi tawi lao, ili lijulikane kote duniani na wanaamini watapata wanachama wa kutosha katika kuliendeleza tawi lao.

Alisema kiingilio katika sherehe hizo ni sh. 10,000 kwa kila mtu, pia watoto nao watapata fursa ya kuhudhuria ambapo mwisho wao itakuwa ni saa 12 jioni.

No comments:

Post a Comment