TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Wednesday, June 13, 2012

MATUKIO MBALIMBALI KUTOKA MTANDAO WA GAZETI LA MAJIRA


Posted: 08 Jun 2012 12:48 AM PDT

Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli akikaribishwa na Mkurugenzi wa Kampuni ya Morco Textiles Erfon Aladdin Limited (kushoto) inayotengeneza na kusambaza vifaa mbalimbali vya matumizi ya nyumbani na ofisini kwenye banda la maonesho la kampuni hiyo mara baada ya uzinduzi wa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Bodi ya Makandarasi (CRB) Dar es Salaam jana. (Picha na Charles Lucas)
Posted: 08 Jun 2012 12:40 AM PDT

Posted: 08 Jun 2012 12:37 AM PDT

Na Stephano Samo, Manyara

VIONGOZI wa serikali za mitaa na halmashauri ya wilaya wametajwa kuwa ni chanzo cha migogoro inayotokea ndani ya jamii hapa nchini.

Hayo yalisemwa jana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Uwekezaji na Uwezeshaji ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Hanang mkoani Manyara Bi. Mary Nagu kwenye majumuisho ya ziara yake ya siku saba mjini hapa alipokuwa akizungumza na watendaji mbalimbali.

Bi. Nagu alisema, ni changamoto kwa watendaji wa vijiji na kata na watendaji wa halmashauri kutowajipika ipasavyo katika kuwahudumia wananchi badala yake wao ndiyo wamekuwa chanzo cha migogoro
wilayani hapo kwani hawatatui matatizo ya wananchi hivyo wanapaswa kubadili mwelekeo.

Mbunge huyo alisema kuwa, matatizo ya wananchi pindi yanapoachwa kutatuliwa kwa muda mrefu yanajenga usugu ambao ni kero ya kudumu.

Pia aliwaasa watendaji hao kuwa, ni lazima waache kukaa ofisini badala yake wawe na desturi ya kuwatembelea wananchi kwe nye makazi yao kwani kwa kufanya hivyo wataweza kubaini matatizo ya wananchi haraka na kuzitatua kero zinazowakabili haraka.

Akizungumzia migogoro ya wavamizi katika ardhi inayoendelea mjini hapa alisema, hatua za haraka zinapaswa kuchukuliwa ili kudhibiti hali hiyo.

Naye Mkuu wa wilaya hiyo Bi. Cristina Mdeme akizungumzia taharuki zilizojitokeza kwenye mgogoro wa uvamizi wa Mto Nyamuri baada ya wananchi zaidi ya 2,000 kufyeka miwa na migomba ya ndizi ya Bw.Sulemani amewataka wananchi hao kuacha hasira kwani serikali itachukua hatua haraka kutatua mgogoro huo.

Bi. Mdeme aliongeza kuwa ni marufuku kwa mtu yoyote kulima au kufanya shughuli yoyote kwenye vyanzo vya maji na si hapa Nyamuri bali maeneo yote ya wilayani na nchi nzima kwani maji ni uhai wa watu na viumbe vyote hai.

Akizungumzia Sensa ya Taifa ya Watu na Makazi pamoja na Katiba Mpya ya Tanzania Bi. Mdeme aliwataka wananchi wote hapa nchini washiriki kikamilifu kwenye kutoa maoni yao kwenye tume iliyoundwa  sambamba na ushiriki wa sensa.
Posted: 08 Jun 2012 12:49 AM PDT
Kutokana na umasikini uliokithiri wananchi wengi wamekua wakiishi katika nyumba zisizo bora kwa kukosa fedha za kulipa kodi.
Posted: 08 Jun 2012 12:25 AM PDT

Na Elizabeth Mayemba

SAKATA la mchezaji Kelvin Yondan limezidi kuchukua sura mpya, baada ya Klabu ya Simba kujibu mapigo na kuonesha mkataba waliomuongezea mchezaji huyo, huku wakidai huo uliooneshwa na watani zao Yanga ni feki.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa Klabu hiyo, Aden Rage alisema Yondan ni mchezaji halali wa Simba kwa kuwa mwaka jana aliongeza mkataba wa kuichezea timu hiyo miaka miwili.

"Mkataba ambao Yanga wameuonesha katika vyombo vya habari naufananisha kama karatasi la chooni (toilet paper), sisi ndio tuna mkataba halali wa mchezaji huyo ambaye aliusaini akiwa chini ya mwanasheria Alan Maduhu na pia TFF (Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania) wanautambua," alisema.

Alisema atawashitaki Yanga, Shirikisho la la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA), kwa kitendo chao cha kumsajili Yondan wakati bado ana makataba na klabu yake.

Mwenyekiti huyo alisema viongozi wa Yanga wamekuwa wakichanganya mara nyingi katika mambo ya soka kwani Ofisa Habari wa klabu hiyo juzi alitoa taarifa kwa vyombo vya habari akidai kuwa walimsajili Yondani Novemba mwaka jana huku picha ikionesha amesaini juzi.

Rage alisema ushahidi wa picha katika mitandao unaonesha Yondan alisainishwa juzi usiku, kwani picha aliyopiga akiwa Ahmed Seif wakati akisaini inaonesha amevaa fulana ya timu ya soka ya Taifa ya Tanzania, (Taifa Stars) yenye nembo ya wadhamini wapya bia ya Kilimanjaro, ambao waliingia mkataba wa kuidhamini timu hiyo mwezi uliopita.

"Kwanza kuna picha ambayo inaonesha Yondani akiwa katika jezi ya mazoezi ya timu ya Taifa yenye nembo ya bia ya Kilimanjaro na kumbukumbu zinaonesha mkataba kati ya TBL na TFF ni Juni 9 mwaka huu, hivyo kwa haraka haraka tukio hilo limefanyika kipindi cha chini ya mwezi mmoja ingawa taarifa za ushahidi zinaonesha tukio hilo lilitokea jana (juzi)," alisema.

Alisema kitendo walichofanya Yanga si cha kistaarabu kwani kinautia aibu mchezo wa soka, hivyo jana aliwaagiza mawakili wa klabu hiyo kukaa na kuandaa mashitaka ya kupeleka FIFA.

Rage pia alionesha nakala ya mkataba ambao Simba ilisaini na Yondani Desemba mwaka jana, ikionesha amepata fedha taslimu sh. milioni 25 kwa miaka miwili.

Alisema Yondani ni mchezaji halali wa Simba  aliye na mkataba hadi Mei 31, mwaka 2014, baada ya kuongeza mkataba na klabu yake, Desemba 23, mwaka jana kwani mkataba wa awali wa mchezaji huyo na Simba uliisha Mei 31, mwaka huu.

"Sheria za FIFA za hadhi na uhamisho wa wachezaji ziko wazi, katika kipengele cha 5 kifungu kidogo cha 2 kinasema kwamba mchezaji atasajiliwa kuichezea timu moja tu kwa wakati mmoja," alisema.
Posted: 08 Jun 2012 12:49 AM PDT
Mwenyekiti wa Simba,Aden Rage akiwaonyesha waandishi wa habari (hawapo pichani) picha ya Kelvin Yondan akisaini mkataba wa Yanga juzi. (Na mpiga picha Wetu)
Posted: 08 Jun 2012 12:15 AM PDT


Na Mwandishi Wetu

KAMPUNI ya Bia Tanzania (TBL), ambayo ni mdhamini mkuu wa timu ya Taifa (Taifa Stars) kupitia bia ya Kilimanjaro Premium Lager imesema ina imani na timu hiyo pamoja na kocha wake Kim Poulsen na imeahidi kuedelea kuipa nguvu, ili ifanikiwe zaidi.

Hayo yalisemwa Dar es Salaam jana na Meneja wa bia ya Kilimanjaro Premium Lager, George Kavishe wakati akitambulishwa rasmi kwa Taifa Stars na nahodha wa timu hiyo Juma Kaseja na Kocha Kim Poulsen na kupata chakula cha mchana na wachezaji.


Kavishe pia aliipongeza timu hiyo kwa kujitahidi wakati wa mechi yao na Ivory Coast Jumamosi iliyopita.

“Nimeelezwa kuwa mlicheza vizuri kwa kujituma na tulikosa nafasi nyingi za kufunga magoli,” alisema Kavishe.

Alisema kampuni yake inaamini huu ni mwanzo na timu hiyo ina nafasi ya kupata matokeo mazuri zaidi katika mechi zijazo, hasa hii ya Jumapili dhidi ya Gambia ya mchujo wa kufuzu kucheza Kombe la Dunia 2014.

“Lazima tuwafanye Watanzania wajione kama sehemu ya timu ya taifa, ili watushangilie wakati tunacheza na ifike wakati walie na sisi tunapolia na wacheke na sisi tunapocheka,” alisema.

Kavishe aliwataka wachezaji wawe karibu na wananchi, ili waweze kujiskia kama sehemu ya timu ya Taifa na kuongeza kuwa Watanzania wana matumaini makubwa na timu yao, hivyo ni jukumu laO kuendelea kuwapa imani na kujituma uwanjani.

Naye kocha Poulsen, aliishukuru TBL kwa udhamini wake mnono kupitia bia ya Kilimanajro Premium Lager na kuongeza kuwa timu haiwezi kuwa imara bila udhamini wa uhakika.

“Kwa sasa tunaweza kufanya mipango ya muda mrefu bila wasiwasi wowote kwa sababu udhamini ni wa uhakika,” alisema.

Posted: 08 Jun 2012 12:49 AM PDT
Meneja wa bia ya Kilimanjaro Premium Lager, George Kavishe akipeana mkono na beki wa Kilimanjaro Taifa Stars, Juma Nyoso wakati alipokutana na wachezaji wa timu hiyo jijini Dar es Salaam jana. Kulia ni nahodha wa timu hiyo, Juma Kaseja pamoja na Kocha Mkuu Kim Poulsen (wa pili kushoto). Na Mpigapicha Wetu


Posted: 08 Jun 2012 12:10 AM PDT


Na Peter Mwenda, Aliyekuwa Dodoma

MBUNGE wa Viti Maalum (CUF) Mkoa wa Dodoma Bi. Moza Said amedai kusikitishwa kupata taarifa kuwa mwanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Ula wilayani hapa Ali Majengo amefungwa jela miaka 20 kwa kosa la kuwalawiti watoto.

Akizungumza na Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Ula Bw. Omari Chuchi hivi karibuni, Mbunge huyo alitaka kujua kabla ya hukumu hiyo shule hiyo ilipokeaje taarifa hiyo wakati kesi ilipokuwa ikiendelea mahakamani.

"Nimesikitika sana kusikia mtoto wenu mmoja amefungwa kwa kosa la kulawiti, acheni kukimbia masomo na kwenda kujificha vichakani mkivuta bangi.

"Hii ni sifa mbaya kwa shule yenu mwanafunzi kukutwa na kosa kubwa kama hilo, mkuu wenu wa shule kaniambia mnatorokea nyumba za jirani na kufanya mambo ya kihuni, nimemwambia apambane na wanafunzi wenye tabia hizo," alisema Mbunge Moza.

Mkuu wa shule hiyo Bw. Chuchi alisema mbali ya wazazi kushindwa kuchangia fedha za kuendesha shule hiyo ada inayolipwa amekuwa akiingia mikataba na vijana waliomaliza kidato cha sita kufundisha shule hiyo.

Wakati huo huo imebainikia kuwa kuzorota kwa elimu katika shule za msingi na sekondari katika Wilaya ya Kondoa mkoani Dodoma hali hiyo imetokana na wanafunzi kushinda njaa wakati wanatumia siku nzima kwenda na kurudi shule.

Wakitoa malalamiko yao kwa Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Dodoma (CUF) Bi. Moza Said wanafunzi hao, walisema wanaondoka nyumbani saa 10 alfajiri bila kula kitu na wanashinda njaa wanapokuwa shuleni na wakirudi nyumbani saa mbili usiku wanakuwa wamezidiwa na njaa.

Mwalimu wa zamu wa shule ya Msingi Tumbelo Bi. Ramla Omari alisema ni kweli mahudhurio hafifu ya wanafunzi wa shule za msingi katika wilaya ya Kondoa kunatokana na njaa kwani wengi wao wanatoka katika vijiji vya jirani ambavyo havina shule ya msingi.
Posted: 08 Jun 2012 12:50 AM PDT
Posted: 08 Jun 2012 12:02 AM PDT

Na Peter Mwenda

MATREKTA madogo (Power tiller)  yameongeza ufanisi katika kilimo cha mazao wilayani Kondoa na kuongeza uzalishaji wa zao la alizeti na ufuta.

Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Kondoa, Bw. Nicolus Kombe aliambia majira kuwa matrekta madogo yanayonunuliwa na Halmashauri hiyo kutoka Kampuni ya Kubota yamekuwa imara kutokana na ardhi ya Wilaya ya Kondoa.

Alisema Halmashauri ya Wilaya ya  Kondoa mpaka sasa imekwisha nunua matrekta madogo 89 kuviuzia vikundi vidogo vidogo vya ushirika vya wakulima wadogo wamekopeshwa.

"Wakulima wadogo wilayani Kondoa wameongeza kiwango cha kilimo kutoka majembe ya mkono na sasa wanatumia matrekta ambayo yameongeza ufanisi wa usafiri, kufua umeme, kubeba mazao" alisema Mkurugenzi huyo.

Meneja Masoko wa kampuni ya Kubota, Bw. David alisema kampuni yake imekuwa ikitoa mikopo ya matrekta madogo katika wilaya mbalimbali nchini kupitia Halmashauri na maombi ya vikundi hivyo yanaongezeka siku hadi siku.

Mratibu wa kikundi cha Mshikamano chenye trekta moja alisema imekuwa mkombozi kwa wakulima wa wilaya ya Kondoa kwani mkulioma aliyekuwa akilima ekari mbiuli za alizeti sasa analima ekari 20.
Posted: 08 Jun 2012 12:50 AM PDT

Kaimu Mkurugenzi wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Bw. Raymond Mbilinyi akizungumza na Kaimu Mkurugenzi wa Kampuni ya Katani Limited, Juma Shamte (kushoto) mara baada ya uzinduzi wa tathmini ya kampuni bora 100 nchini Dar es Salaam jana. (Peter Twite)
Posted: 07 Jun 2012 11:59 PM PDT

Na Mwandishi Wetu

WAFANYABIASHARA wa Soko Kuu la wilayani hapa wamemlalamikia Diwani wa Kata ya Kondoa mjini Bw.Hamza Mafita wakidai ameshindwa kuwatetea wafanyabiashara kuhusu ushuru mkubwa wanaolipa.

Wakizungumza katika mkutano wa dharura katika soko hilo, wafanyabiashara hao walidai kuwa wanalipa ushuru wanaponunua bidhaa zao lakini bado wanatozwa wanapoingia sokoni na baadaye wanatozwa tena wanapoingiza mezani.


Wafanyabiashara hao pia walilalamika kuwa bidhaa zinapofika wilaya ya Kondoa watoza ushuru  hawazitambui risiti hizo na kulazimisha kulipa ushuru mwingine.

Alisema wafanyabiashara hao hawana sehemu ya kushusha mizigo na hivyo kuwalazimu kushusha nje ambako huongeza gharama nyingine ya kubeba bidhaa hizo kuingiza sokoni.

Bi. Farida Seif alisema aliwahi kugoma kulipa ushuru kwa sababu ya mizigo yake kuibiwa kutokana na ulinzi hafifu hivyo wezi kuingia kwa urahisi na kuiba mali za wafanyabiashara.

Mmoja wa wabeba mizigo sokoni hapo ambaye hakutaka kutaja jina lake alisema soko hilo linazidi kuharibika kwani linavuja na hakuna milango ya kuingia kwa gari ndani ya soko hilo.

Wafanyabiashara hao waliomba waandishi wa habari kusaidia kuibua kero zinazowakabili wananchi wa wilaya kongwe ya Kondoa ambayo mpaka sasa haina barabara ya lami.

Diwani wa Kondoa Mjini Bw. Mafita alipopigiwa simu kujibu malalamiko hayo alisema hayo si malalamiko ya kweli bali yanatokana na mambo ya kisiasa katika soko hilo wengi ni wafuasi wa Chama cha Wananchi (CUF).

Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Dodoma, Bi. Moza Said aliwaahidi wafanyabiashara hao kufutilia malalamiko yao kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Kondoa kupata ufumbuzi.
Posted: 08 Jun 2012 12:50 AM PDT
Mkurugenzi wa Kampuni ya King Promoters, Tom Chilala (kulia) akizungumza na waandhishi wa habari (hawapo pichani), kuhusu mashindano ya Redd's Miss Chang'ombe 2012 yatakayofanyika kesho katika Ukumbi wa Quality Center, Dar es Salaam. Katikati ni Meneja wa Redd's Victoria Kimaro na (kushoto) ni mratibu wa mashindano Teddy Cheddy. (Picha na Victor Mkumbo)


Posted: 07 Jun 2012 11:41 PM PDT


Na Victor Mkumbo

NAIBU Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Amos Makalla, anatarajia kuwa mgeni rasmi katika mashindano ya kumsaka Redd's Miss Chang'ombe 2012, yanayotarajiwa kufanyika kesho katika Ukumbi wa Quality Center.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Mratibu wa mashindano hayo, Teddy Chebby alisema Makala ndiye atakuwa mgeni rasmi ambapo atafuatana na baadhi ya Wabunge wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania.

Alisema mashindano mwaka huu, yatakuwa ya aina yake kutokana na maandalizi mazuri waliyoyafanya.

Teddy alisema jumla ya wanyange 14 watawania taji hilo, ambao kila mmoja amejitapa kuondoka na ushindi kutokana na maandalizi waliyoyafanya.

Alisema kuwa mshindi wa kwanza ataondoka na sh. 500,000, wa pili sh. 350,000, wa tatu atapewa sh. 250,000 wakati wa nne na watano wataondoka na sh. 200,000 kila mmoja na waliobakia watapata kifuta jasho cha sh. 100,000.

Mratibu huyo alisema mbali na warembo kujinadi ukumbini, pia kutakuwa na burudani kutoka kwa bendi ya Mapacha Watatu pamoja na msanii wa kizazi kipya, Naseeb Abdul 'Diamond'.

Aliwataja warembo watakaopanda jukwaani kesho kuwa ni Jesca Haule, Wensley Mabula, Frola Robert, Elizabeth Moshi, Latifa Mabewa, Debora Nyakisinda, Like Abraham, Catherine Masumbigana, Flora Kazungu, Clara Diu, Restituta Faustine, Mariam Ntakisuvya na Suzan Paulo.
Posted: 08 Jun 2012 12:50 AM PDT

Mtafiti Mshiriki wa Taasisi za Kidini Dkt.Comillus Kassala akichangia mada katika Kongamano la Kitaifa la Kiuchumi (TPN) lililofanyika Dar es Salaam juzi. (Picha na Prona Mumwi)
Posted: 07 Jun 2012 11:38 PM PDT


HOSPITALI ya Wilaya ya Makete mkoani Njombe imepokea msaada wa vifaa afya na tiba vyenye thamani ya sh. milioni 200.5 kutoka Shirika lilisilokuwa la kiserikali la Uboreshaji wa Maisha Vijijini la nchini Uingereza
(TRR).

Shirika hilo lenye wanachama sita ambao ni raia wa nchi hiyo wakishirikiana na Watanzania wazaliwa wa Wilaya ya Makete ambao wanaishi jijini Dare es Salaam mara kwa mara wamekuwa wakifanya shughuli za maendeleo katika wilaya hiyo.


Akikabidhi misaada hiyo mwakilishi wa Wanamakete hao Bi. Sophia Ng'wango alisema, misaada hiyo imetolewa kwa lengo la kusaidia sekta ya afya na kutatua kero mbalimbali ambazo zinaikabili sekta hiyo.

Alisema, Shirika la TRR lilianza shughuli za kuwasaidia watu wa Makete tangu mwaka 2006 ambapo lilitoa fedha ambazo zilisaidia watoto yatima katika Kituo cha Bulongwa, ujenzi wa bweni katika Shule ya Sekondari ya Mwakauta na kununua vitabu katika shule ya Usililo na kwamba kila mwaka tangu mwaka huo shirika limekuwa likitoa fedha kwa ajili ya kusaidia sekta mbalimbali.

Bi. Ng'wango alisema, katika kipindi ambacho wameanza mahusiano na wahisani hao tayari wananchi kadhaa wamenufaika na misaada ambapo hadi sasa kuna maeneo mengi ambayo yamenufaika na msaada huo na kwamba katika sekta za kifedha wametoa misaada ya fedha za kutunisha mfuko katika Saccos ya Bulongwa na Juhudu Saccos.

Alisema, pia Shirika la TRR linajihusisha na utatuzi wa kero ya huduma ya maji katika maeneo mbalimbali na kwamba vijiji vya Iniho, Bulongwa na Unyangogo Serikali ilipelekewa fedha na wananchi hao ili kupeleka huduma ya maji katika maeneo hayo.

Ofisa Tawala wa wilaya hiyo Bw. Joseph Chota aliwashukuru wahisani na kuomba kama kuna fursa nyingine ni vyema waangalie uwezekano wa kusaidia serikali katika ujenzi wa nyumba za watumishi pamoja na kujenga uzio wa hospitali kwani inapungukiwa na vitu mbalimbali muhimu ikiwa ni pamoja na  majokofu katika vyumba vya maiti.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Makete Bi. Imelda Ishuza alisema, ushirikiano unaoonesha na wananchi hao ni mfano wa kuigwa na kwamba serikali inapunguziwa mzigo wa majukumu na kwamba kama wananchi wengi wangelikuwa na moyo wa kujitolea kama hao matatizo katika wilaya hiyo hususan katika sekta mbalimbali yasingekuwepo.

Bi. Ishuza aliwashukuru wahisani hao na kuongeza kuwa serikali inathamini na kujali mchango wao na kwamba itasimamia kwa haki kuhakikisha kila mkilichotolewa kinatumika katika malengo ambayo yalikusudiwa na si vinginevyo.

Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa halmashauri hiyo Bw. Atilio Ng'ondeya kwa niaba ya wananchi aliomba uongozi wa hospitali hiyo kuhakikisha vifaa hivyo vinanufaisha wananchi wa eneo lililokusudiwa na kwamba vitumike kwa matumizi sahihi sawa na malengo yaliyokusudiwa.

ANCHOR

Wananchi kunufaika na mradi wa umeme

SHIRIKA lisilokuwa la kiserikali la CEFA linalojihusisha na masuala ya kijamii mkoani Njombe limezindua mradi wa kufua nishati ya umeme katika Kijiji cha Ikondo ambao unatarajia kugharimu zaidi ya sh. bilioni 3.5.

Aidha, shirika hilo linafadhiliwa na mashirika ya ulaya na kufanya kazi na kampuni ya CEFA ya mjini Njombe, Kampuni ya Matembwe iliyopo Lupembe wilayani humo.

Shirika hilo lilianzisha mradi wa ufuaji wa umeme zaidi ya miaka 25 iliyopita na kusambaza katika vijiji vya Matembwe, Barazani na Lupembe.

Akitambulisha mradi huo kwa viongozi wa vijiji, kata, tarafa, wilaya na halmashauri  katika ukumbi wa halmashauri ya wilaya hiyo hivi karibuni Meneja Mradi wa shirika hilo Bw. Giacono Spigarelli alisema, mradi wa Ikondo unatarajia kuzalisha nishati ya umeme zaidi ya 'Kw. 240'
ambapo awali ulikuwa unazalisha 'Kw 80' huku matumizi yakiwa makubwa kulinganisha na kiwango kinachozalishwa.

Bw. Spigarelli alisema, wananchi wanaohitaji huduma ya nishati hiyo ni wengi, ambapo mradi uliopo ulianza mwaka 2006 na kwamba mradi unaotambulishwa hivi sasa utanufaisha wananchi katika kata zaidi ya 10 ambapo wananchi wameshiriki kikamilifu katika kuandaa mpango wa kukamilisha madi huo unaotarajia kukamilika miaka minne ijayo.

Kwa upande wake Bw. Johannes Kamonga alisema, CEFA lilianza kushirikiana na MVC baada ya kubaini kuwa wanaweza kuendesha miradi ya umeme kutokana na wao kufanikisha kusimamia mradi wao wa umeme ambao ni wa muda mrefu, na kwamba kazi ya usanifu na mitambo itasimamiwa na MVC.

Alisema, Kampuni ya MVC imekuwa msitari wa mbele katika masuala ya nishati ya umeme kwa kuwa pamoja na kujihusisha na mausuala ya uzalishaji vifaranga, pia wana mradi wa umeme ambao unahudumia vijiji vya Tarafa ya Kata ya Lupembe.

Bw. Kamonga alisisitiza madiwani na viongozi wa vijiji kuhakikisha wanasimamia uandaaji wa miundombinu katika maeneo ya mradi ili mafundi waweza kurahisisha ufikaji katika mradi.

Naye Father Camirro Cariall alisema, kazi ya ubunifu w a miradi ya maendeleo imekuwa ikifanywa na yeye na kwamba kila anachokiona chema machoni pake ni chema kwa jamii, kwa ujumla kwani kazi ya 'umishionari' ni kuangalia matatizo ya wananchi na kuyatatua.

Akizindua mradi huo Kaimu mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya Bw. Steven Mkalimoto aliwashukuru wahisani na kuomba uharakishaji katika ujenzi wa mradi huo ili wananchi waanze kunufaika na mradi huo.

Alisema, sasa ni jukumu la viongozi kuhakikisha wanashirikiana na wahiisani hao ambao wanakuja kuangaza maisha ya wananchi ambao kimsingi hawana msaada hususan katika masuala ambayo ni nyeti na kuhakikisha nishati hiyo inafika katika, maeneo ya kutolea huduma za afya.

Alisiitiza ushirikiano na wahisani hao na kwamba, yapo amambo ambayo serikali inapaswa kushiriki moja kwa moja katika mradi huo, lakini nguvu za wananchi zitaharakisha kukamilika kwa mradi na kuleta tija.

Katika hafla hiyo fupi ya utambulisho wa mradi, wadau mbalimbali waliudhuria ambapo Diwani wa Kata ya Mtembwe Bw. Shaibu Masasi alisema, wananchi wameshiriki kikamilifu katika masuala ya maandalizi na kwamba ushirikishwaji ni muhimu katika mradi huo
Posted: 08 Jun 2012 12:51 AM PDT

Bondia wa timu ya Taifa ya ngumi, Haruna Swanga akifanya mazoezi ya kutafuta nguvu katika GYM ya Gymkhana, Dar es salaam jana (kulia) ni kocha wa timu hiyo David Yombayomba. (Picha na Rajabu Mhamila)

Posted: 07 Jun 2012 11:33 PM PDT


Na Elizabeth Mayemba

DROO ya mashindano ya vijana chini ya miaka 17 ya Copa Coca-Cola Ngazi ya Taifa ilichezeshwa jana na tayari ratiba ya mashindano hayo imetolewa.

Mashindano hayo yanatarajia kuanza kutimua vumbi Juni 24, mwaka huu katika viwanja vinne jijini Dar es Salaam, huku kila kundi likiwa na timu saba.


Akizungumza Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa mashindano hayo ya vijana Msafiri Mgoi, alisema wameamua kuchezesha droo hiyo ili isionekane kama wamepanga ratiba kwa kuzipendelea timu fulani.

"Kila mtu ameshuhudia droo jinsi ilivyochezeshwa, hivyo hakuna upendeleo wowote ni wajibu wa makocha kuleta wachezaji ambao watakidhi vigezo hasa suala la umri, na timu itakayokiuka vigezo kuna adhabu ambayo itatolewa," alisema Mgoi.

Alisema timu zote zinatakiwa kuwasilisha usajili kwa muda unaotakiwa na pia ana imani udanganyifu hautakuwepo katika suala zima la umri, ili mashindano hayo yafanyike kwa haki.

Mgoi alisema Kundi A lina timu za Kigoma, Lindi, Ilala, Arusha, Kusini Pemba, Rukwa na Ruvuma katika ambapo timu zitafungua dimba ni Kigoma na Lindi ambazo watacheza Uwanja wa Karume.

Alisema Kundi B lina timu za Morogoro, Manyara, Kaskazini Magharibi, Mjini Magharibi, Iringa, Mwanza na Tanga na timu zitakazofungua dimba ni Morogoro na Manyara kwenye Uwanja wa Kawe.

Mwenyekiti huyo alisema Kundi C lina timu za Temeke, Kinondoni, Mtwara, Mbeya, Kaskazini Unguja, Dodoma na Mara na watakaofungua dimba ni Temeke na Kinondoni kwenye Uwanja wa Nyumbu.

Alisema Kundi D lina timu za Kilimanjaro, Kusini Unguja, Pwani, Singida, Shinyanga, Kagera na Tabora, watakaofungua dimba ni Kilimanjaro na Kusini Unguja kwenye Uwanja wa Tamko.

No comments:

Post a Comment