TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Wednesday, June 13, 2012

Kigogo CUF atimkia Chadema

Posted: 07 Jun 2012 01:35 AM PDT

Mkuu wa Wilaya ya Korogwe Mrisho Gambo (kushoto) akishiriki kupima afya yake wakati wa uzinduzi wa mafunzo ya siku 10 kuhusu njia bora ya maisha na kujikinga na kukabiliana na magonjwa sugu yasiyoambukiza iliyoratibiwa kwa pamoja na Mfuko wa Bima ya Afya wa Taifa (NHIF) na Shirika la Maendeleo la Ujerumani (GIZ)
Posted: 07 Jun 2012 12:29 AM PDT
Ndege mpya ya ATCL inayotumika sasa baada ya kutua uwanjani Dar es salaam hivi karibuni.
Posted: 07 Jun 2012 12:25 AM PDT

Rais Jakaya Kikwete (katikati) akiwa na marais wastaafu, Benjamin Mkapa (kushoto) na Ali Hassan Mwinyi wakati wa harambee ya kuchangia fedha za mpango wa Mkapa Fellows unaoratibiwa na Taasisi ya Mkapa HIV/AIDS iliyofanyika Dar es Salaam juzi. (Picha na Ikulu)
Posted: 07 Jun 2012 12:17 AM PDT

Katibu Msaidizi wa CCM  Wilaya ya Temeka, Bi. Anastazia Mwonga (kulia), akimkabidhi Bw. Yahaya Ndomondo, fomu za kugombea nafasi ya Katibu wa Siasa na Uenezi wa Wilaya ya Temeke, Dar es salaam juzi, kwa ajili ya uchaguzi  mkuu wa chama hicho. (Na Mpigapicha Wetu)
Posted: 07 Jun 2012 12:15 AM PDT


WALIMU wa Shule za Sekondari wilayani  Kahama mkoani Shinyanga ,wameanzisha kampeni ya kupiga vita tatizo la mimba kwa wanafunzi mashuleni.

Mpango huo ambao wanauitwa 'Rosebug'  kwa maana 'ua waridi changa lazima litunzwe na kulindwa', lengo lake ni kuwaokoa watoto na tatizo la kupata ujauzito wakiwa shuleni.

Kampeni hiyo ilizinduliwa juzi katika Sekondari ya Nyihogo mjini Kahama na kuzihusisha shule 15 za Tarafa ya Kahama Mjini, ambapo kulitolewa elimu ya kuwataka watoto kuachana na vitendo vya zinaa vinavyosababisha mimba shuleni.

Tunaunga mkono mpango huo kwani tunatambua athari za mimba mashuleni. Ujauzito kwa wanafunzi kwa kiasi kikubwa unaathiri mipango ya wazazi wanafunzi kwa ujumla, ndiyo maana Serikali imekuwa mstari wa mbele kupambana na mafataki.

Tatizo hilo limekuwa likisababisha kila mwaka maelfu ya wanafunzi wa kike kuacha masomo kutokana na kupata ujauzito.

Tatizo hilo si tu linawasikitisha wazazi waliotumia fedha zao nyingi  kuwasomesha watoto wao, bali pia wanakuwa wameongezewa mzigo wa malezi ya mtoto.

Hali hii  huwakatisha tamaa wazazi na ndio sababu baadhi yao  wanahofu kuwaendeleza watoto wao wa kike kielimu.

Zipo sababu nyingi ambazo zimekuwa zikiwafanya mabinti wengi wajikute wakipata ujauzito na miongoni mwake ni kutokana na kutojua njia dhabiti za kujikinga na ujauzito na baadhi ya wazazi wanakaa mbali na watoto wao, hivyo kutopata fursa ya kuwapa elimu ya kujikinga na mimba za utotoni.

Wengine wanadhani jukumu hilo ni la walimu. Hali hiyo ndiyo inachangia kuongezeka kwa mimba kwa wanafunzi kutokana na watoto wetu kukosa malezi ya pamoja. Tunatambua kuwa zipo njia za kila aina ambazo zinaweza kumaliza tatizo hili iwapo kila mmoja ataelewa kuwa tatizo hilo ni kubwa.

Kinachotakiwa ni wazazi na walezi kwa pamoja ndani ya jamii ni kuzungumza kauli ya kutokomeza ujauzito kwa wanafunzi wa kike. Hii inawezekana iwapo kila mmoja wetu anatahakikisha mtoto wa jirani yake analindwa.

Hata hivyo tuna imani kama jitihada za pamoja zitaunganishwa kufanya kampeni kama hiyo, tatizo hili  litaweza kupungua kwa kiasi kikubwa kama  siyo kutokomezwa kabisa.

Tunachukua fursa kuwaomba walimu  na wazazi katika wilaya nyingine nchini nao kupanga mkakati kama huo ili kukabiliana na janga hilo.
Posted: 07 Jun 2012 12:14 AM PDT

Meneja Maendeleo ya Biashara wa Kampuni ya Simgas Tanzania Ltd, Bw. Tayeb Noorbhai (kulia) akizungumza na baadhi ya wateja jinsi ya kutumia gesi550 itokanayo na mabaki ya vyakula na takataka waliotembelea banda la kampuni hiyo Dar es Salaam jana, inayotumika kwa matumizi ya nyumbani ambayo pia huzarisha mbolea, wakati wa Maonesho ya Nishati Jadilifu. (Picha na Charles Lucas)
Posted: 07 Jun 2012 12:12 AM PDT

Na Zahoro Mlanzi

KLABU ya Simba, imepanga kufanya ziara katika mikoa ya Kanda ya Ziwa kuanzia Juni 16 na 17 mwaka huu yenye lengo la kusherehekea kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara.

Mbali na hilo, Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), kupitia bia ya Kilimanjaro Lager, imepanga kuikabidhi timu hiyo basi jipya la kisasa siku ya Simba Day, ambayo hufanyika kila mwaka Agosti 8.

Akizungumza Dar es Salaam jana wakati wa kutangaza rasmi ziara hiyo, Mwenyekiti wa klabu hiyo, Ismail Rage alisema ziara hiyo ni maalumu kwa ajili ya kupeleka kombe walilotwaa kwa mashabiki wao wa Kanda ya Ziwa.

"Tutaanzia Shinyanga Juni 16 ambapo tutacheza na Toto African na kisha kwenda Mwanza nako tutacheza na timu moja kutoka Uganda, ambapo mazungumzo yanaendelea na ikiwa tayari tutaitangaza," alisema Rage.

Alisema mashabiki wa mikoa hiyo watapata fursa ya kufurahia mafanikio ya timu yao kwa msimu uliopita na watashuhudia ushirikiano uliopo kati yao na TBL.

Naye Meneja wa bia ya Kilimanjaro, George Kavishe alisema wanaishukuru timu hiyo kwa kuendelea kuwaunganisha pamoja Watanzania kwa mafanikio wanayoyapata na pia kutekeleza yanayopaswa kufanywa katika mkataba wao.

Posted: 07 Jun 2012 12:11 AM PDT
Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA), Juma Pinto (kulia), akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana (hawapo pichani), kuhusu tuzo za Mwanamichezo Bora wa mwaka zitakazotolewa Juni 14 mwaka huu. Katikati ni Meneja Mawasiliano wa SBL, Imani Lwinga na kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa TASWA, Maulid Kitenge. (Picha na Victor Mkumbo)
Posted: 06 Jun 2012 11:53 PM PDT

Na Goodluck Hongo, Lindi

CHAMA cha Wananchi (CUF), kimepata pigo baada ya Bw. Mohamed Madebe aliyekuwa meneja kampeni wa Mbunge wa Jimbo la Lindi Mjini, Bw. Salum Barwany, kukihama chama hicho na kukimbilia CHADEMA.

Uamuzi huo aliutangaza jana katika mkutano wa hadhara maarufu kwa jina la Okoa Mikoa ya Kusini uliofanyika Lindi Mjini.


Bw. Madebe alisema ameamua kukihama cha hicho kutokana na chama cha CUF kupoteza mwelekeo na kuyumbayumba.

"Nimeamua kukihama CUF kwa utashi wangu wenyewe bila ya kushurutishwa na mtu kwani hivi sasa chama hiki kimekuwa kikipoteza mwelekeo na kutokuwa na sifa kama awali, " alisema.

Aliwaomba wananchi wengine kumfuata, kwani CHADEMA inaoneka kuwa ni chama ambacho kimeonesha nia ya kubadilisha maisha ya umaskini kwa wananchi.

Katika mkutano huo, Mwenyekiti wa CHADEMA, Bw. Freeman Mbowe, alisema chama hicho kitaendelea na operesheni yake katika maeneo mbalimbali ili kuwaamsha wananchi waliolala na kunyanyukia CHADEMA.
Posted: 06 Jun 2012 11:51 PM PDT

Posted: 06 Jun 2012 11:50 PM PDT

Na Mwandishi Wetu

TIMU ya Taifa (Kilimanjaro Taifa Stars), imepanda katika viwango vinavyotolewa kila mwezi na Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA), kutoka nafasi ya 145 mpaka 139.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Ofisa Habari wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Boniface Wambura ilieleza kwamba Tanzania imepanda kwa nafasi sita kwenye orodha hiyo inayoongozwa na Hispania.


Alisema timu hiyo ambayo kwa sasa inadhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager, ilikuwa namba 145 hivi sasa imefika nafasi ya 139 ikiwa na pointi 214.

"Mei 26, mwaka huu Taifa Stars ilicheza mechi ya kirafiki na Malawi na kutoka suluhu. Malawi yenye pointi 324 imeporomoka kwa nafasi tano kutoka ya 102 hadi 107," ilieleza sehemu ya taarifa hiyo.

Alisema Ivory Coast ambayo katika mechi yake ya mwisho Juni 2, mwaka huu iliifunga Taifa Stars mabao 2-0 imeporomoka kwa nafasi moja kutoka ya 15 hadi 16 ikiwa na pointi 943. Hata hivyo ndiyo inayoongoza kwa upande wa nchi za Afrika katika viwango hivyo.

Wakati huohuo, timu ya Taifa ya Hispania imeendelea kuongoza ikifuatiwa na Uruguay, Ujerumani, Uholanzi, Brazil, England, Argentina, Croatia, Denmark na Ureno.

Zingine ni Chile ambayo ipo nafasi ya 11 ikifuatiwa na Italia, Urusi, Ufaransa, Ugiriki, Ivory Coast, Sweden, Jamhuri ya Ireland, Mexico na Colombia.

Posted: 06 Jun 2012 11:48 PM PDT
Mwendesha Pikipiki ya abiria 'Bodaboda', (aliyesimama kushoto), akiwa ameshika nyonga, haamini kilichotokea, huku akimwangalia Polisi wa Kikosi cha Usalama Barabarani, aliyekuwa akimwandikia faini, baada ya kukutwa na makosa ya usalama barabarani eneo la Karume, Manispaa ya Ilala Dar es Salaam juzi. (Picha na Heri Shaaban)
Posted: 06 Jun 2012 11:44 PM PDT

Na Zahoro Mlanzi

NI zali limedondoka, ndivyo utakavyothubutu kusema baada ya Mawakala watatu kutoka nchi mbalimbali kumuhitaji mshambuliaji wa timu ya Taifa ya Uganda 'The Cranes' na Simba, Emmanuel Okwi akacheze soka la kulipwa Ulaya.

Lakini klabu ya Simba, imeweka wazi kwamba ipo tayari kumwachia nyota huyo kama wakiwa wameweka kitita cha euro 500,000 na si vinginevyo.


Akizungumza Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa klabu hiyo, Ismail Aden Rage alisema wamepokea ofa kutoka kwa mawakala watatu ambao wanafanya kazi na wakala Ali Selehe wa Zanzibar kwamba wanamuhitaji mshambuliaji huyo.

"Mawakala hao wanataka Okwi akacheze soka la kulipwa katika nchi za Seribia, England au Australia lakini kati ya hao wakala anayetaka Okwi akacheze Australia ndiye ambaye tunaendelea kufanya naye mazungumzo.

"Tayari ameshatuma maelezo ya awali ambayo yanapitiwa na mwanasheria wake na wanamuhitaji kipindi hiki, lakini hao wengine bado hawajaweka wazi ni lini wanamuhitaji," alisema.

Alisema watakuwa tayari kumruhusu Okwi kwenda popote kwa zaidi ya euro 500,000 kwani wachezaji wao kwa sasa wapo juu kiuchezaji, hivyo dau hilo ni kwa Okwi na ikitokea kwa mwingine watazungumza nao.

Aliongeza kuwa ukiachana na Okwi, pia kuna wachezaji wengine watatu wa timu yake ya vijana (U-20), wakati wowote wanakwenda nchini Ujerumani kufanya majaribio ya kucheza soka la kulipwa.

Mbali na hilo, pia alijibu maswali kuhusu usajili hususani wa mchezaji Kelvin Yondani ambaye inadaiwa amesaini na Yanga pia, ambapo alisema: "Yondani ni mali yetu na ameshasaini mkataba mwingine, hivyo wanaosema kasaini sehemu nyingine hilo ni la kwao."

Alisema si hilo tu, wanajua vitu vingi vinazungumzwa kuhusu kocha wao, Milovan Cirkovic lakini alithibitisha kwamba wameshamalizana naye na kwamba muda si mrefu atarejea nchini kuendelea kuinoa timu hiyo katika mashindano ya Kombe la Kagame.
DUA
Posted: 06 Jun 2012 11:43 PM PDT

Wachezaji wa timu ya Taifa (Taifa Stars), wakiomba dua mara baada ya kumaliza mazoezi yao ya kujiandaa na mechi dhidi ya Gambia itakayofanyika Jumapili katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Mazoezi hayo yalifanyika jana kwenye Uwanja wa Karume. (Picha na Rajabu Mhamila)
Posted: 06 Jun 2012 11:41 PM PDT


Na Elizabeth Mayemba

JUMLA ya wagombea 28 wa Klabu ya Yanga wamejitokeza kuwania nafasi za uongozi katika kinyang'anyiro cha Uchaguzi Mdogo uliopangwa kufanyika Julai 15, mwaka mhuu.

Akizungumza Dar es Salaam jana Katibu wa Kamati ya Uchaguzi ya klabu hiyo
Francis Kaswahili, alisema awali walijitokeza wagombea 33 lakini wanne hawakurudisa fomu.


Aliwataja wagombea wanaowania nafasi ya Uenyekiti kuwa ni Yusuf Manji, John Jambele, Edgar Jambele na Sarah Ramadhan, nafasi ya Umakamu ni Ayoub Nyenzi, Ally Mayai, Yono Kevela na Clement Sanga.

Kaswahili aliwataja wanaowania ujumbe kuwa ni Abdallah Binkleb, Mussa Katabalo, Ramadhan Kampira, Lameck Nyambaya, Mohammed Mbaraka, Ramadhan Said, Edgar Fongo, Beda Tindwa na Ahmed Gao.

Wengine ni George Manyama, Aaron Nyanda, Omary Ndula, Shaaban Katwila, Jumanne Mwamenya, Peter Haule, Justine Baruti, Abdallah Mbaraka, Jamal Kisongo, Gaudisius Ishengoma na Yono Kevela.

Alisema ambao hawakurudisha fomu ni Muhingo Rweyemamu, Mzamiru Katunzi, Eliakim Mmaswi waliokuwa wanawania ujumbe na Isaack Chanja Makamu Mwenyekiti.

Kaswahili alisema Kamati ya Uchaguzi ya Yanga na ile ya TFF, kesho watapitia majina ya wagombea wote na yale yaliyokidhi vigezo yatatangazwa tena.

No comments:

Post a Comment