TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Thursday, January 23, 2014

BARUA KWA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, JAKAYA MRISHO KIKWETE

Rais Dk. Jakaya Mrisho Kikwete.
KWA: MHE. RAIS WA JAMHURI YA  MUUNGANO WA TANZANIA, JAKAYA MRISHO KIKWETE
Ndugu,
YAH: UNYANYASAJI ULIOPITILIZA WA BODI YA MIKOPO KWA WANAFUNZI WASOMAO CHINA
Tafadhali rejea mada iliyotajwa hapo juu.
Mheshimiwa Rais, awali ya yote, tunapenda kuchukua fursa hii kukupa pole na majukumu yako ya kila siku na kukutakia heri ya Mwaka Mpya.
Mheshimiwa, tunaandika  barua hii ya  wazi kwako tukiomba  kutatuliwa  matatizo  yetu  makuu   mawili. Tumefikia hatua hii  baada  ya  kushindwa  kupata  suluhisho la  matatizo  haya kwa  watendaji  walio  chini  yako  ambao ni Bodi ya  Mikopo (HESLB)  na Ubalozi wa Tanzania  nchini China (kupitia mwambata  wa  wanafunzi).
1.    Ucheleweshwaji  uliopitiliza  wa pesa  za  kujikimu.
2.    Kiwango  kidogo cha  pesa ya  kusafirishia na kutolea  mizigo.
UCHELEWESHWAJI ULIOPITILIZA WA PESA ZA KUJIKIMU:
 Kwa  masikitiko  makubwa tunapenda kuwasilisha tatizo   la ucheleweshwaji uliopitiliza wa  pesa  za  kujikimu kwa  wanafunzi  tunaoendelea na masomo yetu nchini China. Kwa mujibu  wa  utaratibu  wa Bodi  ya Mikopo ni kwamba pesa  hii ya  kujikimu  inayozungumziwa ilipaswa iwe  imemfikia  kila mwanafunzi  kwa  mwaka  wa  masomo  kila  uanzapo  mwezi wa  tisa (Septemba).  Lakini katika   hali ya kusikitisha,  pesa  hii  bado haijatufikia   hadi  sasa  mwezi Januari.
Tumejaribu  kuchukua  hatua  nyingi  za  awali ikiwemo  kuwasiliana  na  ubalozi wtu  kwa kupitia  mwambata  wa  wanafunzi  wasomao  China (ushahidi    upo ) pia tumefanya  mawasiliano  na Bodi  ya  Mikopo moja  kwa  moja  bila  mafanikio yoyote (ushahidi  upo ushahidi ) zaidi ya  kuambulia  majibu yasiyo  na  kichwa  wala  miguu (ushahidi upo ).
Licha ya sisi kuwa wavumilivu kwa miezi zaidi ya mitano sasa, bado tunaendelea kupewa majibu mepesi ya kwamba tuendelee kuwa na amani na wavumilivu kwamba pesa zitakuja tu lakini haijulikani ni lini, mwezi gani na nini hasa chanzo cha kucheleweshwa mikopo hiyo?
Ikizingatiwa   kuwa  kuna baadhi  ya  wanafunzi  wanatarajia  kuhitimu mwezi  wa  saba (Julai) licha  ya  kwamba  wanahitaji  pesa  ya kujikimu  ila  pia  watahitaji pesa  kwa ajili  ya  kusafirishia  mizigo yao pindi watakapomaliza  muda  wao wa masomo  nchini China.  
KIWANGO KIDOGO CHA PESA YA KUSAFIRISHA MIZIGO:
Moja ya  changamoto  kubwa  ambayo imekuwa ikitukabili  wanafunzi  tusomao  China na  hasa  wakati  wa  kuhitimu  masomo  yetu ni  usafirishaji  wa  mizigo (vitu  mbalimbali  vikiwemo  vifaa  vya  utafiti, vitabu  na  vitu  binafsi).
Kwa wanafunzi waliohitimu  kabla ya mwaka 2013  walikuwa wanapewa pesa  ya kusafirishia mizigo kuanzia Dola za Kimarekani 3,000  hadi  3,500  lakini baadaye Bodi ya Mikopo iliamua kupunguza pesa hiyo  kufikia Dola za Kimarekani 1,200. 
Ukweli ni kwamba gharama  za usafirishaji wa mizigo kutoka China kwenda Tanzania zimeongezeka kwa kasi sana na  pesa hii  kwa  uhalisia  haitoshi hata  kidogo.
Kwa mshangao mkubwa na bila kushirikishwa  kwa wanafunzi  tusomao  China ambao  ndiyo  wanufaikaji, Bodi ya Mikopo iliamua kupunguza pesa hiyo kwa zaidi ya asilimia 100 hadi kufikia Dola za Kimarekani 1,200, pamoja na kwamba kiasi kilichoombwa baada  ya  utafiti  wa  kina  juu  ya gharama za  usafirishaji  na  utoaji  mizigo viliambatanishwa.
Kiasi hicho kusema ukweli hakikidhi gharama za usafirishaji wa mizigo ya wahitimu kutoka sehemu mbalimbali za China kwenda nyumbani Tanzania.
Mfano mwaka jana wanafunzi walishindwa kusafirisha baadhi ya vitu vyao kutokana na gharama kuwa kubwa sana na ambao waliweza kuongeza pesa kutoka mfukoni mwao na kusafirisha walishindwa kuvitoa pale bandarini Dar es Salaam.
HITIMISHO:
Kutokana na matatizo haya na mengine mengi ambayo tunashindwa kuyaeleza hapa, suala hili limesababisha usumbufu mkubwa kwa wanafunzi katika shughuli zao za kimasomo.  Hii  ni  pamoja  na  baadhi  ya  tafiti zao kushindwa  kufanyika ipasavyo.
Ombi letu kwa Mh.  Rais ni kwamba tunaomba tupatiwe ufumbuzi wa matatizo   yetu haraka kwa sababu tumeshavumilia  vya  kutosha.  Tunaomba pesa ya kujikimu  iwe inatumwa  kwa wakati na pia  pesa ya kusafirishia mizigo ipatiwe ufumbuzi.
Aidha irejeshwe kama ilivyokuwa awali au ikiwezekana iongezwe ili kukidhi  gharama za usafirishaji na utoaji  mizigo  Tanzania.  
Mheshimiwa Rais, ni wazi kuwa tumehuzunishwa na kusikitishwa sana na udhalilishaji, uonevu na unyanyaswaji tunaofanyiwa kutokana na kutowajibika kwa baadhi ya watendaji wa Bodi ya Mikopo na ubalozi  wetu ama kwa kutambua au kutotambua wajibu wao.
Tunaamini suala letu utalipa uzito unaostahili.
Tunatanguliza shukrani zetu za dhati na pia tunakutakia mafanikio mema katika shughuli zako za ujenzi wa taifa.
Wako wanafunzi  wa Tanzania walio China.

No comments:

Post a Comment