TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Wednesday, January 22, 2014

Ratiba ya M4C- Operesheni Pamoja Daima, Ruvuma, Tabora na Tanga

Kama ambavyo jana umma wa Watanzania ulitaarifiwa kupitia kwenye mkutano wa Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Freeman Mbowe na wanahabari, Chama leo kinaanza operesheni ya takriban wiki mbili kwa nchi nzima (mijini na vijijini).

 Kuna jumla ya timu 6 zilizoko uwanja wa mapambano kuendesha M4C- Operesheni Pamoja Daima, ambazo zote zinaanza kazi leo katika maeneo zilizopangiwa. Timu tatu zitakuwa zikishambulia kutokea angani na timu tatu zitakuwa zikisonga mbele nchi kavu.
Timu hizi zinajumuisha viongozi wakuu wa Chama, watendaji kutoka Makao Makuu ya Chama, Wajumbe wa Kamati Kuu, Viongozi wa Kanda, Mikoa, Wilaya, Majimbo, Kata, Vijiji na Vitongoji pamoja na wabunge wote wa CHADEMA katika maeneo husika.

CHADEMA itatumia operesheni hii ya wiki mbili kuandaa umma wa Watanzania juu ya masuala kadhaa muhimu kwa hatma ya nchi yao;

1. Mjadala wa rasimu ya pili ya katiba mpya- Bunge Maalum la Katiba Mpya Wakati huu ambapo nchi Watanzania wanasubiri vikao vya Bunge Maalum la Katiba, pamoja na Tume ya Warioba kufanya kazi nzuri kwa kukusanya na kuzingatia  maoni ya watu (ambayo CCM wanayapinga wakiweka mbele maslahi ya chama  chao badala ya Watanzania wenye nchi yao), bado kuna masuala ambayo;

(a) yanahitaji msisitizo yaendelee kubakia kwenye rasimu

(b) yanahitaji kuboreshwa

(c) yanahitajika kuongezwa kwa sababu hayamo

2. Kuhusu uboreshwaji wa daftari la wapiga kura kwa ajili ya kura ya maoni kuamua Katiba Mpya na Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010.

Hii ni moja ya shughuli ya 'kufa na kupona' mwaka huu kwa sababu kuna mamilioni ya Watanzania hadi sasa Serikali ya CCM imewanyima haki yao ya kikatiba ya kufanya maamuzi yanayohusu maisha yao, maendeleo yao kupitia kura.

3. Uchaguzi wa ndani ya chama ambao hadi sasa unaendelea katika ngazi ya msingi nchi nzima hatimaye ngazi ya taifa.

4. Masuala ya Watanzania na umiliki wa rasilimali zao ambazo kwa sasa zinaonekana kuwanufaisha wageni, watawala na watu wenye mahusiano na watawala, pia hali ya ugumu wa maisha inayozidi kuwakabili wananchi ikiwa na uhusiano na uongozi mbovu unaokumbatia ufisadi na sera zilizoshindwa, yatapewa kipaumbele kikubwa katika ziara hii.

5. Bila kusahau kwamba 'all politics is local', hivyo chama kitatumia fursa hii kuzungumza na wananchi juu ya kero mbalimbali zinazowakabili na CHADEMA inaweza ku-offer nini. Na mengine kadha wa kadha yenye umuhimu kwa  maendeleo ya watu.

Ifuatayo ni ratiba ya leo na kesho kwa timu tatu za angani ambazo zinatumia usafiri wa helkopta 3;

Timu ya Katibu Mkuu, Dkt. Slaa;

Mbambabay, Mbinga, Peramiho, Namtumbo kisha kwa leo watamalizia Songea Mjini

Timu ya Makamu Mwenyekiti Zanzibar, Issa Saidi Mohamed

Nzega (Ndala), Igunga (Nkinga), Tabora Kaskazini (Mabama) na Tabora mjini

Timu ya Kamanda Tundu Lissu na John Heche

Lushoto, Korogwe, Muheza na Tanga mjini

* Tutawapatia updates kadri muda unavyokwenda. Accounts za CHADEMA mitandaoni ikihusisha pia 'vyombo' vya chama kama websites na blogs, ndizo zitakuwa vyanzo rasmi vya taarifa za uhakika kwa kila kinachoendelea field.

Tutashirikiana na mods pamoja na watu wengine wote hasa walioko fields kwenye timu zote 6 kuhakikisha Watanzania wanapata taarifa sahihi, za uhakika, kwa wakati, huku pia tukiomba uvumilivu wenu na subira inapolazimika, ili kupata vitu vizuri maana mikutano itafanyika maeneo ya vijijini na mijini.

Punde tutatoa ufafanuzi wa baadhi ya hoja za watu kama vile, kwa nini helkopta (tena idadi imeongezeka, hakuna chama cha siasa kiliwahi kufanya kama hivi kwenye operesheni kama hii), kwa nini PAMOJA DAIMA (wengine wanafikiri ni tofauti na M4C).

Haya karibuni kwa ajili ya M4C- PAMOJA DAIMA hii ndiyo habari yenyewe kwa sasa.

No comments:

Post a Comment