TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Wednesday, January 22, 2014

NDUGU WAMFANYIA KITU MBAYA BIBI KIKONGWE WA MIAKA 100 BILA HURUMA...


Bibi kizee, Mwamini Abdallah
UONEVU! Bibi kizee, Mwamini Abdallah anayekadiriwa kuwa na umri  
wa zaidi ya miaka 100 (alikuwepo wakati wa Vita ya Kwanza ya 
Dunia ya 1914), anadai kunyang’anywa shamba na ndugu zake kisha kutelekezwa na kumsababishia kuishi kwa tabu.
 Akizungumza na waandishi wetu, bibi huyo anayeishi katika 
Kijiji cha Ngeleka-Usagara mkoani hapa alidai kwamba aliingia 
kwenye mgogoro wa mirathi na ndugu zake aliochangia nao baba 
mara baada ya mzazi  wake huyo kufariki dunia. 
Bibi huyo alisema kuwa mgogoro huo ulisababisha kufunguliwa kwa 
kesi Mahakama ya Mwanzo ya Misungwi na hukumu kuwapa haki ndugu 
zake hao na yeye kuambulia ardhi kidogo. 
Hata hivyo, aliiuza ardhi hiyo kidogo aliyopewa baada ya kukosa huduma za msingi  mara alipotengwa na ndugu zake.
 Waandishi wetu wamejionea hali ya bibi huyo ambaye analala 
chini akitandika na kujifunika magunia huku paa la ‘kibanda’ anachoishi likivuja. 
Kikongwe huyo anapata msaada kidogo kutoka kwa jirani yake 
Halima Said anayemchotea maji na kumpatia akiba kidogo ya chakula. 
Alisema kuwa hata kibanda hicho cha matope anachoishi kwa sasa alijengewa na mama mmoja aliyekuwa nesi maeneo hayo  lakini kwa
 sasa kipo hatarini kubomolewa kutokana na kujengwa kwenye 
hifadhi ya barabara inayotengenezwa kutoka Usagara kwenda Kisesa. 
“Nalelomba bhamunhu mnahmbilije naphandike hakulalaa niishiliwa,
alisema bibi huyo kwa Lugha ya Kisukuma akimaanisha ‘naombeni mnisaidie sehemu ya kulala na chakula.’  
Kufuatia ugumu wa maisha ya bibi huyo, mjukuu wake, Mariam John 
(15) ndiye anayemsaidia kwa kufanya kazi za ndani Mwanza mjini 
kwa ujira wa Sh. 20,000/= kwa mwezi, fedha ambazo pia hazikidhi mahitaji yao binafsi.  Kwa yeyote atakayeguswa na mateso 
anayopata  bibi huyu na anataka kutoa msaada wake, awasiliane 
na mwanaharakati wa kutetea haki za binadamu wa asasi ya
 FARIJIKA kwa namba 0787 040 261 au 075

No comments:

Post a Comment