TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Thursday, January 23, 2014

MAMA KIKWETE ASISITIZA KUPUNGUZA MAAMBUKIZI KUTOKA KWA MAMA KWENDA KWA MTOTO

IMG_0452  

Na Magreth Kinabo – Maelezo


 Mke wa Rais Mama Salma   Kikwete amewataka  Watanzania  kuongeza juhudi za kuzuia maambukizi ya Virusi
Vya Ukimwi(VVU)  kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto ili  katika  Tanzania iweze kuwa na kizazi kisichokuwa na VVU na ugonjwa wa Ukimwi.
 Kauli hiyo imetolewa leo na Mama Kikwete  ambaye pia  ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA)  wakati akifungua mkutano wa kitaifa wa  wadau wa kuzuia maambukizi ya VVU kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto.
Aidha mama Kikwete aliwataka Watanzania kuchangia sh. 100 katika kupambana na tatizo kwa mchango  utawapa nguvu wadau wengine kuwaunga mkono.
 Aliwataka wadau wamaendeleo kuendele kuunga mkno katika juhudi za kuondokana na tatizo hilo.
 “ Lazima juhudi za makusudi zifanyike bila kuchoka kwa maeneo yote Serikali, NGO’s, taasisi za dini mashirika ya kiraia na watu binafsi . Hii itasaidia kunusuru kizazi chetu na kuwa na nguvu kazi iliyobora, kizazi kisichokuwa na maambukizi na VVU na Ukimwi,” alisema Mama Kikwete huku akisisitiza Tanzania bila Ukimwi inawezekana.
 Aliongeza kuwa mikakati imara na endelevu ni lazima iwepo kama vile kutoa huduma za kuzuia maambukizi ya VVU na Ukimwi kwa kushirikisha jamii na kutoa tiba kikamilifu zinaweza kupunguza maambukizi hayo.
 Alisema asilimia 98 ya  wakina mama wajawazito wanahudhuria kiliniki angalau mara moja  na asilimia 43 mara nne  wakati wa ujauzito kati ya hao, asilimia 81 wanapimwa VVU.
Aliwataka wakina mama wajazito kuhudhuria kiliniki wakati wa  ujauzito kuanzia siku ya kwanza hadi watakapoajifungua  ili idadi ya wanahudhuria kiliniki  iweze kufikia  asilimia 100.
 Naye Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Seif Rashid alisema hivi sasa Tanzania imefanikiwa kupunguza maambukizi hayo kwa asilimia 15 mwaka 2012  kutoka asilimia  19  mwaka 2011  na lengo ni kufikia asilimia 5 ifikapo mwaka 2015.
 Alisema asilimia 90 ya wakina mama wajawazito wamepimwa VVU kati yao asilimia 64 wamegundulika wanaishi na VVU , pia asilimia 55 ya watoto wanapatiwa dawa za kupunguza makali ya ugonjwa huo.(ARV’s).
 Kaimu Mkurugenzi wa Kinga kutoka wizara hiyo , Dk .Neema  Rusibamayilla alisema  alisema awamu ya pili ya kupambana na tatizo hilo itaanza Januari mwaka huu katika mikoa  mingine 16.
 Mratibu wa huduma hiyo kutoka Malawi, Dk. Michael Eliya alisema  ni muhimu kuweza katika  utoaji wa huduma, kuboresha miundombinu ,ikiwemo rasilimali fedha na watu katika kufanikisha malengo hayo.
======================================================

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI, MHE. PEREIRA SILIMA AELEZEA MAFANIKIO YA WIZARA YA MAMBO YA NDANI YALIYOFIKIWA NA SERIKALI YA AWAMU YA NNE, JIJINI DAR

1 
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Pereira Silima(katikati) akitoa taarifa ya Mafanikio ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi katika kipindi cha Serikali ya Awamu ya Nne kwa Waandishi wa Habari(hawapo pichani) leo Januari 21, 2014 katika Ukumbi wa Mikutano, Makao Makuu ya Jeshi la Polisi, Jijini Dar es as Salaam(kulia) ni Kamishna wa Utawala wa Jeshi la Polisi, Clodwing Mtweve(Kushoto) ni Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Habari na Maelezo, Bw. Assah Mwambeni.
image 

Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza Nchini, John Casmir Minja akiwa pamoja na Viongozi Wengine Wakuu wa Idara zilizo chini ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi wakati Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Pereira Silima akitoa taarifa rasmi ya Mafanikio ya Wizara ya Mambo ya Ndani katika kipindi cha Serikali ya Awamu ya Nne(wa pili kulia) ni Kamishna Mkuu wa Idara ya Uhamiaji, Sylivester Ambokile(kushoto) ni Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Nchini, Pius Nyambacha. image_1 
Baadhi ya Wakurugenzi mbalimbali wa Idara za Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi wakifuatilia kwa makini taarifa ya Mafanikio ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi katika kipindi cha Serikali ya Awamu ya Nne iliyotolewa na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Prereira Silima kwa Waandishi wa Habari leo Januari 21, 2014 katika Ukumbi wa Mikutano, Makao Makuu ya Jeshi la Polisi, Jijini Dar es Salaam(Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).

No comments:

Post a Comment