TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Friday, January 24, 2014

Snoop Dogg avuta Bangi za kufuru katika moja ya hoteli maarufu Australia

article-2544251-1ADC0EAB00000578-483_634x593
.aweka picha kadhaa kwenye mtandao wa Instagram
Na. MOblog Tanzania, Kwa msaada wa mtandao
Rapa maarufu nchini Marekani ametoa kali ya mwaka baada ya kupost picha kadhaa kwenye mtandao kuonyesha akivuta bangi kwenye moja ya hoteli Queensland Gold Coast maarufu kama Palazzo Versace nchini Australia.
Vyombo vya habari nchini Australia vimeripoti kuwa rapa huyo maarufu duniani alikwenda kufanya tamasha la mwaka la muziki lakini akaiishia kufanya vituko hotelini kwa kuvuta bangi siku nzima na kugonga vichwa vya habari vya Australia.
article-2544251-1AE333C100000578-841_634x512 
Rapa huyo mwenye umri wa miaka 42 aliweka picha nyingi akionyesha anavuta bangi kwa kwenda mbele na kwenye meza yake aliweka bangi nyingi kwenye bakuli tayari kuvuta lakini wachambuzi wa mambo wamesema ni kinyume cha sheria za Australia kuvuta bangi .
Nyota huyo ambaye anaonekana haguswi nchini marekani (untouchable) jina lake halisi ni Calvin Cordozar aka snoop dogg dogg akiwa amevaa shati la superman na rasta akivuta bangi kwenye moja ya hoteli hiyo maarufu nchini Australia.
Polisi nchini Australia wamethibitisha kwamba rapa huyo amevunja sheria za Australia kwa kuvuta bangi na kupiga picha na kuweka kwenye mitandao ya kijamii  na wanasubiri jinsi ya kumhoji kwa upepelezi zaidi.
article-2544251-1AE333C900000578-281_634x645
Afisa huyo wa Jeshi la Polisi nchini Australia amesema  ‘Hata kama sisi hatuna uwezo wa kupata mabaki ya bangi katika chumba cha hoteli, tunaweza kufanya upekuzi katika chumba chake kujiridhisha na tuhuma zake hizo,” amesema
Waziri uhamiaji wa Australia,  Scott Morrison ametishia kufuta visa ya rapa huyo maarufu kwa kukiuka sheria za nchi yao kwa kuvuta bangi na kuweka picha kwenye mitandao ya kijamii.

No comments:

Post a Comment