TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Saturday, June 11, 2016

BoT yatoa Sh. Milioni 273 kuchangia ununuzi wa madawati nchini.


Fedha hizo zilikabidhiwa leo kupitia hundi ya mfano kwa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa baada ya matembezi ya hisani yaliyolenga kuchangia madawati, yaliyoanzia Ofisi za BOT hadi kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.Akizungumza kabla ya kukabidhi fedha hizo, Gavana wa BOT Prof. Benno Ndulu alisema lengo la mchango huo ni kuunga mkono juhudi za Serikali ya Awamu ya Tano katika kuongeza ubora wa elimu kupitia upatikanaji wa madawati kwa shule za msingi na sekondari nchini.

“Tunatambua kwamba changamoto hiyo (uhaba wa madawati) ni kubwa, lakini tunaamini mchango wetu utasaidia kupunguza makali ya tatizo hilo na kuongeza idadi ya watoto wetu ambao wanasoma wakiwa wamekaa kwenye madawati” alisema Gavana Prof. Ndulu.

Alitaja mikoa hiyo na fedha zilizochangwa na wafanyakazi wa BOT wa matawi ya mikoa hiyo kuwa ni Makao Makuu Dar es Salaam waliochangia Shilingi Milioni 22, Mwanza (Milioni 1.24), Chuo cha Benki Mwanza (680,000) Arusha (Milioni 1.23) Mbeya (Milioni 1.186), Mtwara (850,000) na Dodoma (Milioni 1.18).

Alisema taasisi zilizochangia fedha hizo ni Benki ya India Shilingi Milioni 5, Benki ya Habib (Milioni 5), Benki ya Exim (Milioni 5), Benki ya UBA (United Bank for Africa, Milioni 2), Tanzania Mortgage Refinance (Milioni 2), China Community Bank (Milioni 2) na NIC Bank aliyotoa Milioni 1.

Kwa upande wa kampuni za simu zilizotoa fedha ni kampuni ya Vodacom iliyotoa Dola za Kimarekani 10,000, kampuni ya Tigo Dola za Kimarekani 10,000 na kampuni ya Selcom iliyotoa Dola za Kimarekani 5,000.

Akizungumza baada ya kupokea hundi ya mfano, Waziri Mkuu Majaliwa alisisitiza fedha hizo zitumike kama zilivyokusudiwa na yeyote atakayetumia fedha hizo kinyume na malengo achukuliwe hatua mara moja.Katika kuthamini sekta ya elimu nchini, Gavana Prof. Ndulu alisema benki hiyo ilianzisha Mfuko wa Udhamini wa Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere ambapo hadi sasa umetoa ufadhili kwa wanafunzi 22 kusoma shahada za kwanza na za uzamivu katika vyuo vikuu hapa nchini katika masomo ya sayansi, hisabati, uchumi, fedha, uhasibu na TEHAMA.

No comments:

Post a Comment