TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Friday, June 10, 2016

UZINDUZI WA HOTEL YA KISASA KUSILE RESTAURANT AND LODGE MJINI MBINGAULIOFANYIKA NA MWENGE WA UHURU 2016.

MPALULEBLOGS:
Mkurugenzi wa kampuni ya Ovans Construction Company Limited, ambao ni wamiliki wa Kusile Restaurant and Lodge, Valence Urio upande wa kulia akiwa ameshika Mwenge wa Uhuru mara baada ya Kiongozi wa mbio za Mwenge George Mbijima kufungua rasmi hoteli hiyo iliyopo Mbinga mjini mkoani Ruvuma. Ni Hoteli ya kisasa iliyopo Mbinga mjini mkoani Ruvuma ikiwa ni Hotel ya kwanza na ya kisasa katika wilaya hiyo

Msimamizi wa hoteli ya Kusile Restaurant and Lodge, Mary Thomas upande wa kushoto akisoma taarifa ya maendeleo juu ya ujenzi wa hoteli hiyo ya kisasa kwa Kiongozi wa mbio za Mwenge, George Mbijima wa pili kutoka kulia. Wa pili kutoka kushoto ni mmiliki wa hoteli hiyo, Verena Urio. Mradi huu umefanikiwa pia kuwawezesha wakulima wadogo wadogo 10 kuanzisha kilimo cha mboga mboga maalumu ambazo hazipatikani Mbinga, hivyo kutengeneza soko la uhakika kwa mboga mboga hizo na zile za kawaida pia imefanikiwa kutengeneza ajira 22 ambapo kati ya hizo wanawake wapo 16 na wanaume sita.
Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa, George Mbijimi akiondoa kitambaa ikiwa ni ishara ya ufunguzi rasmi wa hoteli ya kisasa ya Kusile Restaurant and Lodge iliyopo Mbinga mjini mkoani Ruvuma. Ambapo Kiongozi huyo wa mbio za Mwenge, aliwataka watoa huduma katika hoteli hiyo wahakikishe kwamba wanatoa huduma zinazolingana na hadhi ya jengo hilo, ili biashara wanazozifanya ziweze kuwa endelevu.Hata hivyo Mbijima amewapongeza wamiliki wa jengo hilo la biashara, kwa ubunifu walioufanya ambao utasaidia kupunguza uhaba wa nyumba ya kisasa ya kulala wageni na kuweza kupata huduma bora ya chakula.
Mkurugenzi wa kampuni ya Ovans Construction Company Limited, ambao ni wamiliki wa Kusile Restaurant and Lodge, Valence Urio akimwelekeza kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa 2016 George Mbijima
Mkurugenzi wa Kusile Restaurant and Lodge akisalimiana na kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa 2016 George Mbijima. Hotel hiyo ipo mkabara na stand kuu ya Mabasi mjini Mbinga.Kwa maelezo zaidi unaweza kuwasiliana nao 067 609 660/ 0784 609 660. (picha zote na ruvumahabari.blogspot.com

No comments:

Post a Comment