TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Wednesday, June 8, 2016

MKUTANO MKUU WA MTANDAO WA MASHIRIKA YA WAZEE TANZANIA WAZINDULIWA


a
Mheshimiwa Ummy Mwalimu (Mb.) Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Mtandao wa Mashirika ya Wazee Tanzania.
Mheshimiwa Ummy Mwalimu (Mb.) Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto akihutubia wazee walioshiriki katika Mkutano Mkuu wa Mtandao wa Mashirika ya Wazee Tanzania

Akihutubia katika uzinduzi wa Mkutano huo Mheshimiwa Waziri Ummy alizitaka Halmashauri kuhakikisha wanatekeleza wajibu wao wa kutoa vitambulisho kwa wazee ili kuwezesha utambuzi wa wazee waliopo katika Halmashauri zao hususan katika utoaji huduma na mahitaji mbalimbali.

Mfano wa kitambulisho kinachotolewa kwa wazee wa Halmashauri ya Wilaya ya Kasuru.

Waziri Ummy alisisitiza kuwa Halmashauri zinatakiwa kutekeleza kwa vitendo kaulimbiu ya “Mzee Kwanza” hususan katika utoaji wa huduma za afya ambapo kila kituo cha Afya cha Umma kinatakiwa kiwe na chumba na watumishi maalum wa kuhudumia wazee. Pia ameziagiza Halmashauri zote nchini kuhakikisha wanakuwa na regista ya Wazee kwa kuainisha pia ujuzi wa wazee hao.

Mheshimiwa Waziri Ummy alieleza kuwa Serikali inatarajia kuwasilisha muswada wa sheria ya Wazee Bungeni Mwezi Septemba mwaka huu. Pia, aliwahakikishia wazee kuwa tatizo la upatikanaji wa dawa kwa wazee litapatiwa ufumbuzi kwa kiasi kikubwa kuanzia mwezi Julai 2016

No comments:

Post a Comment