TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Thursday, November 28, 2013

PINDA AWASHUKIA MAOFISA MIPANGO


Na Mwandishi Maalum

 Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, amewataka maofisa mipango miji nchini kurekebisha utendaji wao wa kazi ili waweze kubadili taswira mbaya iliyojengeka miongoni mwa jamii dhidi yao.

Alitoa kauli hiyo jana wakati akifungua Mkutano wa Kwanza wa Wataalam wa Mipango miji waliosajiliwa na Bodi ya Usajili wa Wataalam wa Mipango miji ulioanza jana jijini Dar es Salaam.
“Taswira ya utendaji kazi katika taaluma ya mipango miji na katika sekta ya ardhi kwa ujumla miongoni mwa wananchi na Serikali sio nzuri sana. 
 
 Watafiti wanatueleza kuwa kati ya asilimia 60 na 80 ya makazi kwenye miji yetu hapa nchini yamejengwa kiholela.
Na kwa kiwango hicho hicho wakazi wa mijini wako kwenye makazi hayo na wanaishi kiholela,î alisema. 
 
“Wako wanaosema ninyi ndiyo chanzo cha hiyo migogoro, wako wanaosema ninyi kwa rushwa ndiyo wenyewe, mimi sishangai madai haya ila ninawasihi muwe na roho ngumu katika kushinda vishawishi hivi,” alisisitiza. 
 
Aliwataka wajadili masuala yanayohusu migogoro ya ardhi baina ya wafugaji na wakulima, baina ya mipaka ya vijiji, baina ya wilaya, baina ya wanavijiji na hifadhi za Taifa au maeneo ya uchimbaji madini na kujadili njia za kutatua migogoro hiyo ili kuwa na mipamgo endelevu. 
 
Aliwataka waangalie suala la ukuaji wa miji iliyokaribu na Jiji la Dar es Salaam kwa kuangalia dhana ya miji mikubwa kubeba vijiji vinavyoizunguka na hasa kuangalia uwezekano wa kupunguza mrundikano wa watu katika jiji hilo. 
 
“Miji ya Kibaha, Mkuranga na Bagamoyo inatumikaje kusaidia kupunguza msongamano katika jiji la Dar es Salaam,” Waziri Mkuu alihoji.
Alisema wataalamu wa mipango miji wanapaswa kuwa na maono makubwa ya baadaye kama kweli wanataka kupunguza majanga katika siku za usoni. 
 
“Angalieni utafiti wa gesi unaoendelea pale Mtwara na mjipange, angalieni mpango wa ujenzi wa bandari ya Bagamoyo na kuunganisha na reli ya kati, angalieni Lindi na upatikanaji wa Liquified Naturala Gas (LNG), pangeni miji kwa siku za baadaye siyo sasa,” alisisitiza. 
 
Aliwataka wanataaluma hao wasimamie vyema taaluma yao kwani katika miaka 37 ijayo, (mwaka 2050) inakadiriwa kwamba nusu ya watu wote watakuwa wakiishi mijini. “ Kuweni wakweli, tumieni weledi wenu la sivyo katika miaka 37 ijayo kama wanavyosema watafiti, itakuwa balaa tupu,î alisema.
 
Mapema akimkaribisha Waziri Mkuu kuzungumza na wataalamu hao kutoka mikoa yote hapa nchini, Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Makazi, Prof. Anna Tibaijuka, alisema maofisa mipango miji wanakabiliwa na changamoto ya kufikiri na kubuni aina ya miji ambayo itakidhi mahitaji ya jamii ya baadaye. 
 
Alisema hata hivyo maofisa hao wamekuwa wakikabiliwa na changamoto ya kushindwa kutoa maamuzi au ushauri wa kitaalamu kwa kuhofia kuadhibiwa na madiwani.
Wizara ya Fedha. " Kwa nafasi yake ndiye alikuwa akishiriki kuandaa bajeti ya upinzani bungeni, kuwasilisha bajeti ya wizara ya fedha akiwa waziri kivuli, lakini kwa kuvuliwa wadhifa wake maana yake haaminiki tena," alisema mmoja wa watoa habari ndani ya chama hicho kwa sharti la jina lake kutochapishwa gazetini.
 
Hata hivyo, juhudi za kumpata Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa CHADEMA, John Mnyika, ili kuweza kuzungumzia suala hilo ziligonga mwamba kutokana na simu yake ya kiganjani kutopokelewa.
Wakati huo huo, Jeshi la Polisi Makao Makuu jijini Dar es Salaam leo linatarajia kufanya mahojiano na Katibu wa CHADEMA mkoa wa Dar es Salaam, Henry Kileo, baada ya mahojiano hayo kukwama kufanyika jana kutokana na malalamiko yanayodaiwa kuwasilishwa na Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe. 
 
Mahojiano hayo yalikuwa yafanyike Makao Makuu ya Jeshi la Polisi jijini Dar es Salaam jana mchana, lakini yaliahirishwa muda mfupi baada ya Kileo kuwasili akiwa na mwanasheria wake na makada wengine wa CHADEMA.
Baada ya kufika maofisa wa Polisi walifanya mazungumzo na mwanasheria wake, lakini baada ya muda walikubaliana yafanyike leo saa tano.
 
Akizungumza na gazeti hili jana, Kileo, alisema awali mahojiano yalitakiwa yafanyike jana saa nane mchana, lakini walichelewa kufika makao makuu ya polisi kutokana na wakili wake kuchelewa kwani alikuwa na kesi makao makuu ya Polisi. 
 
Kileo, alipoulizwa anatakiwa polisi kwa ajili ya makosa gani, alisema hana taarifa kwa undani, kwani alipigiwa simu na ofisa aliyejitambulisha kwa jina la Mbutta na kumwambia kuwa anatakiwa kufika makao makuu ya Polisi kwa mahojiano kutokana na malalamiko ambayo Zitto, ameyafikisha. 
 
"Niliambiwa nahitajika kujibu tuhuma ambazo Zitto amezifikisha Polisi, lakini sikuelezwa ni tuhuma gani hizo," alisema Kileo. Alipoulizwa ni kwa nini Zitto apeleke shtaka hilo Makao Makuu ya Polisi, badala ya vituo vingine kama ilivyo kawaida, Kilewo alijibu; "Mimi sijui labda wapigie polisi ili muwaulize swali hilo."
Gazeti moja (sio Majira) jana lilichapisha habari inayoeleza kuwa Zitto, amemfungulia mashtaka Kileo akimtuhumu kusambaza waraka katika mitandao ya kijamii unaomhusisha na mipango ya kufanya mapinduzi ya chama hicho.

MBOWE KUPANGUA ‘MAWAZIRI’ WAKE!

  • HATIMA YA NAFASI ZA ZITTO KUJULIKANA KARIBUNI
  • ALIYEMLALAMIKIA KUHOJIWA POLISI MAKAO MAKUU LEO
Na Goodluck Hongo
   Kiongozi wa Kambi Rasmi Upinzani Bungeni na Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe, anatazamiwa kufanya mabadiliko kwa Baraza lake la Mawaziri Kivuli, wakati wowote katika kipindi cha Mkutano ujao wa Bunge ili kutekeleza maagizo ya Kamati Kuu iliyokutana hivi karibuni na kumvua wadhifa wake Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe.

Zitto amevuliwa wadhifa wake wa Naibu Katibu Mkuu kutokana na kile kinachodaiwa anahusika kuandaa waraka wa kufanya mapinduzi ya viongozi ndani ya chama hicho.
Kwa mujibu wa vyanzo vya habari kutoka ndani ya chama hicho vililiambia gazeti hili kuwa Kamati Kuu ambayo ndiyo inasimamia Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, hivyo mara baada ya kutangaza kumvua Zitto, wadhifa wake (unaibu katibu mkuu) ilielekezwa uanze mchakato wa kumuondoa kwenye nafasi zake.
Bungeni, Zitto ni Naibu Kiongozi wa Kambi Rasmi akiwa msaidizi wa Mbowe na Waziri Kivuli wa
 Wizara ya Fedha. " Kwa nafasi yake ndiye alikuwa akishiriki kuandaa bajeti ya upinzani bungeni, kuwasilisha bajeti ya wizara ya fedha akiwa waziri kivuli, lakini kwa kuvuliwa wadhifa wake maana yake haaminiki tena," alisema mmoja wa watoa habari ndani ya chama hicho kwa sharti la jina lake kutochapishwa gazetini.
Hata hivyo, juhudi za kumpata Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa CHADEMA, John Mnyika, ili kuweza kuzungumzia suala hilo ziligonga mwamba kutokana na simu yake ya kiganjani kutopokelewa.
Wakati huo huo, Jeshi la Polisi Makao Makuu jijini Dar es Salaam leo linatarajia kufanya mahojiano na Katibu wa CHADEMA mkoa wa Dar es Salaam, Henry Kileo, baada ya mahojiano hayo kukwama kufanyika jana kutokana na malalamiko yanayodaiwa kuwasilishwa na Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe.
Mahojiano hayo yalikuwa yafanyike Makao Makuu ya Jeshi la Polisi jijini Dar es Salaam jana mchana, lakini yaliahirishwa muda mfupi baada ya Kileo kuwasili akiwa na mwanasheria wake na makada wengine wa CHADEMA.
Baada ya kufika maofisa wa Polisi walifanya mazungumzo na mwanasheria wake, lakini baada ya muda walikubaliana yafanyike leo saa tano.
Akizungumza na gazeti hili jana, Kileo, alisema awali mahojiano yalitakiwa yafanyike jana saa nane mchana, lakini walichelewa kufika makao makuu ya polisi kutokana na wakili wake kuchelewa kwani alikuwa na kesi makao makuu ya Polisi.
Kileo, alipoulizwa anatakiwa polisi kwa ajili ya makosa gani, alisema hana taarifa kwa undani, kwani alipigiwa simu na ofisa aliyejitambulisha kwa jina la Mbutta na kumwambia kuwa anatakiwa kufika makao makuu ya Polisi kwa mahojiano kutokana na malalamiko ambayo Zitto, ameyafikisha.
"Niliambiwa nahitajika kujibu tuhuma ambazo Zitto amezifikisha Polisi, lakini sikuelezwa ni tuhuma gani hizo," alisema Kileo. Alipoulizwa ni kwa nini Zitto apeleke shtaka hilo Makao Makuu ya Polisi, badala ya vituo vingine kama ilivyo kawaida, Kilewo alijibu; "Mimi sijui labda wapigie polisi ili muwaulize swali hilo."
Gazeti moja (sio Majira) jana lilichapisha habari inayoeleza kuwa Zitto, amemfungulia mashtaka Kileo akimtuhumu kusambaza waraka katika mitandao ya kijamii unaomhusisha na mipango ya kufanya mapinduzi ya chama hicho

WAJASIRIAMALI WAONYWA KUHUSU SIASA


 Na Suleiman Abeid, Shinyanga

Wanachama wa vikundi vya wajasiriamali wadogo katika kata ya Kitangili Manispaa ya Shinyanga wametakiwa kuepuka kuingiza siasa katika vikundi vinginevyo vitasambaratika
.
Tahadhari hiyo ilitolewa juzi na diwani wa viti maalumu (CCM) manispaa ya Shinyanga, Mariamu Nyangaka, alipokuwa akizungumza na viongozi wa vikund imbalimbali vya wajasiriamali waliokutana kwa ajili ya kuanzisha Chama cha Ushirika wa Akiba na Mikopo (SACCOS ).
Nyangaka alisema viongozi wa vikundi vya wajasiriamali pamoja na wanachama wao kwa ujumla wanatakiwa kuhakikisha wanaendesha shughuli zao bila kuingiza au kutanguliza itikadi ya vyama vya siasa katika vikundi vyao kitu ambacho kinaweza kusababisha mgawanyiko miongoni mwao.
Alisema wapo baadhi ya wanasiasa wanaotumia wajasiriamali wadogo kufikia malengo yao waliyojipangia huku wengine wakidiriki hata kuwazuia wafuasi wa vyama vyao wasishirikiane na watu ambao si wafuasi wa vyama vyao vya siasa hata kama shughuli zao zinapaswa kuendeshwa kwa ushirikiano wa pamoja.
"Ndugu zangu mkakati ambao mnataka kuuanzisha ni mkakati mzuri utawasaidia kuendesha shughuli zenu kwa ufanisi mkubwa, mtakapokuwa na SACCOS yenu itawasaidia kuweza kupata mitaji ya kuendesha biashara zenu kupitia mikopo mtakayokopa yenye masharti nafuu tofauti na inayotolewa na benki zetu nyingi nchini,"alisema.
"Lakini naomba mjihadhari na siasa katika vikundi vyenu, mkimruhusu mdudu huyu kuwa miongoni mwenu eleweni wazi hamtadumu kwa kipindi kirefu, hakikisheni mnaendesha shughuli zenu bila kuchanganya na itikadi za kisiasa na wakemeeni wale wote watakaoonesha dalili za kuingiza siasa ndani ya vikundi," alisema Nyangaka.
Kwa upande wake ofisa ushirika kutoka manispaa ya Shinyanga, Athumani, alisema serikali kwa kipindi kirefu imekuwa ikihimiza umuhimu wa wananchi kujiundia vyama vyao vya ushirika wa akiba na mikopo (SACCOS) kwa vile ni rahisi zaidi kusaidiwa na asasi mbalimbali za kifedha. Alisema kupitia SACCOS watu wengi wamefanikiwa katika biashara zao na baadhi wameweza kujenga nyumba za makazi huku wengine wakisomesha watoto wao bila matatizo. Alisema jambo la msingi ni uaminifu wa viongozi wa SACCOS zinazoanzishwa kwa kuhakikisha zinakuwa na wanachama waadilifu na wenye kuzingatia sheria za uendeshaji wa ushirika huo.
Katika hatua nyingine, viongozi hao wa vikundi vya wajasiriamali wadogo wameunda uongozi wa muda utakaosimamia taratibu za uanzishwaji wa ushirika wa akiba na mikopo.
Alisema utaundwa na vikundi vyote vilivyopo katika kata ya Kitangili na kuhakikisha SACCOS hiyo inasajiliwa kisheria ili iweze kuanza kazi mara moja.
Viongozi wa muda waliochaguliwa Elias Joseph (Mwenyekiti), Richard Maige (mwenyekiti msaidizi), Patrick Kileo (katibu), Masunga Elias (katibu msaidizi) ambapo Timothy Kakiri, alichaguliwa kuwa mweka hazina.

HOSEAH AULA SHIRIKISHO LA RUSHWA DUNIANI


Na Mwandi shi Maalumu, Panama 
 
 Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU), Dkt. Edward Hoseah, amechaguliwa kuwa Makamu wa Rais wa Shirikisho la Taasisi za Kuzuia na Kupambana na Rushwa Duniani (IAACA).

Dkt. Hoseah alichaguliwa na wajumbe 460 wa Mkutano Mkuu wa saba wa shirikisho hilo kutoka nchi mbalimbali uliofanyika Panama, Amerika ya Kati kuanzia Novemba 22-24, mwaka huu.
Wajumbe wa mkutano huo ni pamoja na wakuu wa taasisi 98 za Kuzuia na Kupambana na Rushwa Duniani ambapo kaulimbiu ya mkutano huo inasema, "Utawala wa Sheria na Rushwa: Changamoto na Fursa Zilizopo".
Kabla ya kuchaguliwa katika nafasi hiyo, Dkt. Hoseah alikuwa Mjumbe wa Kamati Kuu ya Utendaji katika shirikisho hilo ambapo kutokana na uteuzi huo, anakuwa Mwafrika wa kwanza kushika wadhifa huo mkubwa katika mapambano dhidi ya rushwa duniani.
Uchaguzi huo ni heshima kubwa kwa Tanzania na Bara la Afrika pia ni fursa nzuri kwa Dkt. Hoseah kuonesha uwezo wake wa kuongoza mapambano dhidi ya rushwa kimataifa. Nyadhifa nyingine za kimataifa ambazo Dkt. Hoseah amewahi kuzishikilia ni pamoja na Rais wa
 Kwanza wa Shirikisho la Taasisi za Kuzuia na Kupambana na Rushwa Afrika Mashariki (2007-2008), Rais wa kwanza wa Jukwaa la Taasisi za Kuzuia na Kupambana na Rushwa katika nchi za SADC (SAFAC-2010-2011).
Nyingine ni Mwenyekiti wa Bodi ya Umoja wa Afrika ya Ushauri wa Masuala ya Rushwa (AU-ABC 2011-2012).
IAACA linajumuisha taasisi 298 pamoja na wanachama zaidi ya 2,000 kutoka katika asasi mbalimbali zisizo za kiserikali na lilianzishwa Aprili 19, 2006, Makao Makuu yapo Peking, China.
Lengo la kuanzishwa kwa shirikisho hilo ni kuziwezesha nchi wanachama kutekeleza Mkataba wa Umoja wa Mataifa Dhidi ya Rushwa uliopitishwa na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Desemba 30, 2003.

TZ KUTUNZA NYARAKA ZA MAUAJI YA KIMBARI



 Na Penina Malundo 
 
  Tanzania imeingia mkataba na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa (UN), kwa ajili ya ujenzi wa jengo la kutunzia nyaraka zinazohusiana na kesi za mauaji ya kimbari nchini Rwanda.

  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. Bernard Membe, aliyasema hayo Dar es Salaam jana wakati akizungumza na waandishi wa habari. 
 
  Alisema jengo hilo litagharimu dola za Marekani milioni tano sawa na sh. bilioni nane za Tanzania na litajengwa mjini Arusha katika eneo la Lakilaki. 
 
  "Jengo hili litaweza kuhifadhi nyaraka hizo muhimu pamoja na vielelezo mbalimbali vya kesi za kimbari...mafaili yote ya kiutendaji na kiufundi yatahifadhiwa humo," alisema. 
 
  Bw. Membe alisema, nchi tatu ambazo ni Tanzania, Kenya na Rwanda, ziliomba ujenzi wa jengo hilo katika nchi zao ambapo baraza hilo, limeridhia jengo hilo kujengwa Tanzania. 
 
  Mkurugenzi Mkuu wa Masuala ya Sheria kutoka Umoja wa Mataifa, Miguel de Serpa Soares, alisema baraza hilo limeridhia ujenzi huo ufanyike nchini kutokana na mahusiano mazuri yaliyopo. kati yao na Tanzania.

JK ‘AFUNGUKA’ MGOGORO ZIWA NYASA

  •  AWASILISHA VIELELEZO KWA WASULUHISHI WA MGOGORO

Na Penina Malundo 
 
  Rais Jakaya Kikwete, amewasilisha utetezi wa Tanzania kwa jopo la Marais wastaafu wanaotafuta ufumbuzi wa mpaka wa Ziwa Nyasa, kati ya Tanzania na Malawi.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. Bernard Membe, aliyasema hayo Dar es Salaam jana wakati akizungumza na waandishi wa habari. 
 
Alisema utetezi huo uliwasilishwa kwa Rais mstaafu wa Msumbiji Joaquim Chissano ambaye ndiye Mwenyekiti wa jopo hilo na Rais mstaafu wa Botswana, Bw. Festus Mogae.
Awali, viongozi hao wastaafu walifanya mkutano kama huo Blantyre, nchini Malawi ambapo juzi walisikiliza hoja za upande wa pili juu ya mgogoro huo. 
 
"Katika mkutano huu, Rais Kikwete alitoa maelezo mazuri pamoja na vielelezo mbalimbali... utetezi wetu ulikuwa wa kisayansi hivyo hatuna hofu yoyote juu ya hili," alisema.
Bw. Membe alisema, leo anatarajia kwenda Maputo, nchini Msumbiji, kuwasilisha maelezo yaliyotolewa na Rais Kikwete mbele ya marais hao wastaafu. 
 
Aliongeza kuwa, jopo la Wanasheria wa kimataifa bado linaendelea na kazi ya kufanya utafiti juu ya mgogoro huo kwani jambo hilo kwa kuliangalia ni dogo lakini ni kubwa. 
 
Alisema kuwa mgogoro huu unaweza kuwa na tambo mbalimbali kati ya nchi moja na nyingine ingawa tambo hizo zinaweza kuleta athari kubwa kwa nchi hizo hivyo utafiti zaidi unahitajika.

ZITTO KUJIBU MASHTAKA 11

  •  BARUA ZATOLEWA RASMI,WAPEWA SIKU 14

  • BAADA YA MAJIBU,KUJIELEZA KAMATI KUU

  • LISSU ADAI UTETEZI WAO ULIPOTOSHA UKWELI

 Na Goodluck Hongo
Aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Bw. Zitto Kabwe pamoja na wenzake, wameandaliwa mashtaka 11 kwa madai ya kuandaa mapinduzi ya siri dhidi ya uongozi wa chama hicho kinyume cha katiba.

Bw. Kabwe na wenzake ambao ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya chama hicho, Dkt. Kitila Mkumbo na Bw. Samson Mwigamba, aliyekuwa Mwenyekiti wa CHADEMA jijini Arusha, jana walikabidhiwa barua rasmi ili wajieleze ndani ya siku 14.
Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa CHADEMA, Bw. John Mnyika, aliyasema hayo Dar es Salaam jana wakati akizungumza na waandishi wa habari Makao Makuu ya chama hicho.
Bw. Mnyika ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Ubungo, Dar es Salaam, alisema chama hicho kimeandaa mashtaka hayo baada ya Sekretarieti ya CHADEMA kupitia maamuzi ya Kamati Kuu yaliyowavua nyadhifa za uongozi watuhumiwa hao.
 "Watuhumiwa hawa watatakiwa kujieleza kwa maandishi ndani ya siku 14, baadaye watajieleza mbele ya Kamati Kuu ambayo itatoa maamuzi ya hatua za kuchukua," alisema Bw. Mnyika.
Alisema mashtaka hayo yametokana na waraka wa siri ambao ulikamatwa na kutolewa mbele ya Kamati Kuu unaowakashifu viongozi wakuu wa chama hicho.
"Wote watatakiwa kujieleza kwa nini wasifukuzwe ndani ya chama chetu kwa makosa waliyofanya... Kamati Kuu ya chama ndicho chombo chenye maamuzi ya kuwaondoa viongozi au wanachama wanaokiuka Katiba.
"Waraka uliochapishwa katika baadhi ya vyombo vya habari (si Majira) na mitandao ya kijamii unaodaiwa kuwaponza Bw. Kabwe na wenzake si wenyewe ni batili," alisema.
Aliongeza kuwa, maamuzi yaliyofanywa na Kamati Kuu yalizingatia kanuni, sheria na taratibu za chama kwa kufuata katiba, hivyo Bw. Kabwe na wenzake hawakufukuzwa kwa sababu walizozitoa kwenye vyombo vya habari bali kwa kuandika waraka wa kimapinduzi.
Msimamo wa CHADEMA
Bw. Mnyika alisema, chama hicho hakipo tayari kuwavumilia viongozi na wanachama wote ambao watakuwa kikwazo kwa chama hicho kufikia malengo yake bila kujali cheo alichonacho.
"Wanatafuta huruma kwa wananchi kutokana na makosa ambayo wameyafanya hasa la kuandaa waraka wa siri, wao wenyewe walikiri kuhusika nao lakini wanapotosha ukweli," alisema.
Alisema Sekretarieti hiyo imepokea na kutoa mapendekezo mbalimbali ya utekelezaji wa mikakati waliyojipangia ambayo ni Vuguvugu la Mabadiliko (M4C) na "CHADEMA ni msingi".
Akizungumzia uchomaji wa bendera za chama, ofisi, fulana na kuondoa mabango ya CHADEMA, baada ya Bw. Kabwe na wenzake kuvuliwa nyadhifa za uongozi, Bw. Mnyika alisema chama kimezisikia taarifa hizo.
"Uchunguzi wa awali unaonesha kilichotokea ni kiini macho tu si wanachama wa chama chetu waliofanya hivyo, viongozi wa maeneo husika wanaendelea na vikao, usalama upo," alisema.
Tundu Lissu azungumza
Kwa upande wake, Mwanasheria Mkuu wa CHADEMA, Bw. Tundu Lissu, alisema watuhumiwa walifanya mkutano na vyombo vya habari kwa lengo la kupotosha ukweli wa mambo juu ya mazingira halisi ya kuvuliwa nyadhifa zao.
"Hawakuondolewa katika nyadhifa zao kwa sababu ya kuuza majimbo yetu ya uchaguzi mwaka 2010, si posho, wala uwepo wake kama Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), aliyeibua hoja ya kukaguliwa kwa hesabu za vyama vya siasa.
"Amevuliwa nyadhifa hizo na wenzake kwa sababu ya kuandaa mapinduzi ndani ya chama kwa kukiuka maadili," alisema.
Akizungumzia madai ya kugawanyika au kupasuka kwa chama hicho kama Bw. Kabwe atafukuzwa uanacham, Bw. Lissu alisema kwa nyaraka alizoziona, Kabwe alikuwepo katika kikao cha Kamati Kuu kilichomfukuza aliyekuwa Katibu Mkuu wa chama hicho mwaka 2004, Dkt. Amaan Kabourou.
"Ka bwe p i a a l i k uwe p o kwenye kikao cha Kamati Kuu kilichomfukuza aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa chama hiki, marehemu Chacha Wangwe mwaka 2007; hivyo hata kikao kama hicho ndicho kilichowavua vyeo yeye na wenzie hivyo Kamati Kuu isilaumiwe," alisema.
Bw. Lissu alisema, madai ya Bw. Kabwe kudai alijitoa katika utiaji saini katika masuala ya fedha ndani ya chama hicho kwanza hakuwahi kuwa mtiaji saini ili kuidhinisha fedha, hivyo anashangaa kulizungumzia hilo wakati hakuwahi kuwa mtiaji saini.
"Chama kimepasuka mara nyingi tangu enzi ya Bw. Kabwe kuingia kwenye Kamati ya Jaji Bomani, Chacha Wangwe, ugaidi wa Rwakatare hata sakata la mabomu lakini tuliibuka upya, hadi sasa chama kinaendelea na mapambano yake," alisema.
Alipoulizwa na waandishi kama viongozi hao wakiamua kuondoka, chama kimejipangaje, alisema si vizuri kuwahukumu Bw. Kabwe na wenzake kwa sababu bado hawajaanza kujitetea, lakini kugombea uongozi ndani ya chama si uhaini wala dhambi.
Alibainisha kuwa, sh. milioni 100 zilizotolewa na mfanyabiashara maarufu nchini, Bw. Mustafa Sabodo, hesabu za matumizi yake zipo wazi na zilipelekwa kwenye hesabu za chama hicho ili zikaguliwe na Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).
Aliongeza kuwa, licha ya vyama vya siasa kuwa tayari kukaguliwa, CAG alishindwa kukagua hesabu hizo kwa sababu ya ukosefu wa fedha, hivyo alivitaka vyama husika kuwalipa wakaguzi ambao wangefanya ukaguzi huo jambo ambalo walilipinga.
"Tuna ushahidi wote kuhusu suala hili, hata Msajili mpya wa Vyama vya Siasa, aliandika barua kwa CAG kuhusu kupinga vyama kuwalipa wakaguzi wa hesabu  kwani huo si utarabu wa Serikali, lakini tunamshangaa Kabwe kuzungumzia suala hili wakati analijua vizuri," alisema Bw. Lissu

Tuesday, November 26, 2013

AMKA WORKSHOP LEO MANGO GARDEN KINONDONI DAR ES SALAAM.

 Mkurugenzi wa Chief Promotion Amon Mkoga wa pili kulia, akifafanua jambo kuhusiana na Semina ya Wasanii inayofanyika leo kwenye ukumbi wa Mango Garden kinondoni jijini Dar es Salaam, ikihusisha wasanii mbalimbali kwa lengo la kujifunza haki miliki ya kazi zao. wengine ni wasanii wa kundi la MABAGA FRESH, Christopher Mwingira-aka DJ SNOX, na Jumanne Omary aka JB Mkuu wa Majaji, wa pili kushoto ni Mkuu wa Mpango wa Uchangiaji wa Hiari Mfuko wa Penshen wa PSPF, Matilda Nyallu.

 Mkurugenzi wa Chief Promotion Amon Mkoga wa pili kulia, akifafanua jambo
Baadhi ya Waandishi wa Habari wakifuatilia kwa makini Hafla hiyo,
Mkuu wa Mpango wa Uchangiaji wa Hiari Mfuko wa Penshen wa PSPF, Matilda Nyallu.akifafanua jambo kuhusiana na Semina ya Wasanii inayofanyika leo kwenye ukumbi wa Mango Garden kinondoni jijini Dar es Salaam, ikihusisha wasanii mbalimbali kwa lengo la kujifunza haki miliki ya kazi zao.

Wasanii wa kundi la MABAGA FRESH, Christopher Mwingira-aka DJ SNOX, na Jumanne Omary aka JB Mkuu wa Majaji,Wakifafanua jambo
 baadhi ya wandishi wa habari wakiuliza jambo
hapa wakiwa katika picha ya pamoja muda mfupi baada ya kumaliza mkutano na waandishi wa habari.(Picha kwa Hissani ya Miss Demokrasia Tanzania).