Na Penina Malundo
Tanzania
imeingia mkataba na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa (UN), kwa
ajili ya ujenzi wa jengo la kutunzia nyaraka zinazohusiana na kesi za
mauaji ya kimbari nchini Rwanda.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. Bernard Membe,
aliyasema hayo Dar es Salaam jana wakati akizungumza na waandishi wa
habari.
Alisema jengo hilo litagharimu dola za Marekani milioni tano sawa na
sh. bilioni nane za Tanzania na litajengwa mjini Arusha katika eneo la
Lakilaki.
"Jengo hili litaweza kuhifadhi nyaraka hizo muhimu pamoja na vielelezo
mbalimbali vya kesi za kimbari...mafaili yote ya kiutendaji na kiufundi
yatahifadhiwa humo," alisema.
Bw. Membe alisema, nchi tatu ambazo ni Tanzania, Kenya na Rwanda,
ziliomba ujenzi wa jengo hilo katika nchi zao ambapo baraza hilo,
limeridhia jengo hilo kujengwa Tanzania.
Mkurugenzi Mkuu wa Masuala ya Sheria kutoka Umoja wa Mataifa, Miguel de
Serpa Soares, alisema baraza hilo limeridhia ujenzi huo ufanyike nchini
kutokana na mahusiano mazuri yaliyopo. kati yao na Tanzania.
No comments:
Post a Comment