TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Saturday, November 30, 2013

WAZIRI WA KILIMO YAMKUTA MAZITO, NI KUHUSU NAPE NAUYE.


3 - Copy
>> Amtaka aandae majibu kwa Kamati Kuu sio kumshambulia magazetini
>> Ahoji busara anayoidai itumike ni ipi?
>> Asisitiza kutetea wakulima ni msimamo wa Chama
>> Amkumbusha CCM ni chama cha wakulima
>> Ahoji busara ya kuachia ushirika kuwadhulumu wakulima.
>> Ahoji busara ya kulazimisha wakulima kutumia mbolea ya Minjingu inayoharibu mazao yao.
>
Katibu wa NEC itikadi na uenezi amemtaka
 Waziri wa kilimo, Chakula na Ushirika kuacha kumshambulia kwenye magazeti badala yake atumie muda huu kuandaa majibu ya kuwasilisha Kamati Kuu kwa hoja zilizoibuliwa na wakulima nchini.
Nape akihutubia mamia ya wananchi wa mji wa Vwawa wilayani Mbozi mkoani Mbeya alionyesha kukerwa na tabia ya hivi karibuni ya Waziri huyo kumshambulia Nape kwenye magazeti kwa maneno ya kejeli badala ya kujibu malalamiko ya wakulima.
 ” Katibu Mkuu tumezunguka wilaya nyingi sana nchini hakuna mahali hakuna malalamiko ya wakulima ambao ni 80% ya watanzania wote. Sasa tumemtaka waziri aje kwenye kamati kuu kueleza anatatuaje changamoto hizi, yeye amekazana kila kukicha kunishambulia kwenye magazeti. Nataka kumpa ushauri wa bure mheshimiwa sana waziri, anachofanya hanishambulii mimi anawashambulia wakulima kwasababu siongei yangu naongea malalamiko
 ya wakulima” alisisitiza Nape
 ”Nimemvumilia sana lakini sasa nimechoka, kila kukicha anatumia maneno ya kejeli na vijembe, kwanini hajifunzi busara ya Naibu wake Adam Malima? aliposikia wito wetu akasema yuko tayari kuja kujieleza kwenye Kamati Kuu kwakuwa chama ndiyo mwajiri wake hivyo atazingatia maamuzi ya chama, yeye waziri kila kukicha Nape Nape Nape, kumshambulia Nape hakuondoi kero za wakulima”! Alisema Nape
 ”Nimesikia leo anasema sina busara!!busara ipi anayohoji? Mie ninayewatetea wakulima wanaolalamika kulazimishwa kutumia mbolea ya Minjingu inayounguza mazao yao na yeye anayeleta mbolea hiyo na kulazimisha wakulima watumie nani anatumia busara hapa? Yeye anayepuuza malalamiko ya wakulima kuumizwa na baadhi ya maafisa ushirika na mimi ninayetaka hatua zichukuliwe dhidi ya maafisa wake nani anatumia busara??”
 ” mimi ninayemkumbusha kutembelea mkoa alioutangaza kuwa ghala la taifa la chakula ambao hajautembelea kwa miaka sasa licha ya kuwa waziri wa chakula na yeye ambaye hajatembelea nani anatumia busara?”
 ” mimi ninayemshauri asikilize kilio cha wakulima wa tumbaku,pamba na korosho badala ya kusikia kilio hicho miaka nenda miaka rudi na
 yeye nani anatumia busara?”
Katika ziara hiyo ya Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana ambaye ameongozana na  Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Dk.Asha-Rose Migiro na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Ndugu Nape Nnauye imekuwa na mafanikio makubwa  na imeongeza sana imani kwa wananchi wenye mapenzi mema na nchi hii.
Ziara hii imekuwa ya aina yake kwani Katibu Mkuu amepata fursa ya kusikia matatizo ya wananchi kuanzia wakulima ambao ndio asilimia 80%,walimu ambao ni zaidi ya asilimia 60% ya watumishi wa serikali,na kundi kubwa la vijana ambalo pamoja na kuwepo kwa taratibu za kufanya shughuli zao kwa kujiajiri bado wamekutana na vikwazo visivyo vya kawaida.
Uamuzi wa kuwaita Mawaziri kwenye kamati kuu ya chama ili watoe majibu kwa nini matatizo ya wananchi hasa wakulima hayashughulikiwi .
Wakulima wamelalamika sana kuhusu dhuluma  zinazofanywa na vyama vya ushirika na upatikanaji wa pembejeo kuwa wa tabu na cha ajabu Waziri wa Kilimo na watumishi wake wameziba masikio hata kutembelea wakulima kutaka kujua matatizo yao hawataki.

No comments:

Post a Comment