FAINALI
ya pili ya kombe la shirikisho itapigwa leo katika dimba la Mazembe
mjini Lubumbashi baina ya wenyeji TP Mazembe dhidi ya CS Sfaxien ya
Tunisia.
Katika
mchezo wa leo washambuliaji wawili raia wa Tanzania Mbwana Ally Samatta
na Thomas Ulimwengu watakuwa wakiiongoza timu yao kutafuta ushindi
muhimu na wakihistoria kwao.
Samatta
anatarajiwa kuonesha makali yake zaidi huku ikizingatiwa kuwa ni
miongoni mwa wachezaji wanaowania tuzo ya CAF ya mchezaji bora wa Afrika
kwa wachezaji wanaocheza klabu za ndani.
Kama
mshambuliaji huyo atafunga leo na kuonesha kiwango cha juu, itamsaidia
kujiweka mazingira mazuri zaidi ya kubeba tuzo hiyo inayotolewa na
shirikisho la soka barani Afrika, CAF.
Mazembe
wanahitaji kushinda mabao 3-0 wakiwa katika dimba lao, kwani fainali ya
kwanza walifungwa mabao 2-0 na Watunisia hao dimba la Olympique de
Rades mjini Tunis.
Mabao hayo
yaliyoipa karaha Mazembe na mashabiki wake, yalifungwa na washambuliaji
wawili raia wa Gabon, Ibrahim Didier Ndong aliyefunga bao la kwanza
dakika ya 16 na mshambuliaji Taha Yassine Khenissi aliyefunga la pili
dakika ya 90.
Siku hiyo
Samatta na Ulimwengu wote walianza kikosi cha kwanza pamoja na mkali
Tressor Mputu Mabi, lakini bado mambo yalikuwa magumu zaidi kwani
Watunisia walionekana kuwa bora zaidi yao na kuweza kutumia nafasi
walizopata.
Thomas Ulimwengu naye mzigoni kama kawaida leo
Bingwa wa Kombe hilo atazawadiwa kitita cha dola za Kimarekani, 625 000, wakati mshindi wa pili atapata dola 432 000.
Mshindi
pia atamenyana na mabingwa wa Ligi ya Mabingwa, Al Ahly ya Misri
kuwania taji la Super Cup mechi itakayopigwa nchini Misri Februari 2014.
Wachezaji
waliokuwa wakiunda kikosi cha Simba SC mwaka 1993 walivalishwa Medali
za Fedha na Rais mstafu wa awamu ya pili, Alhaj Ali Hassan Mwinyi baada
ya kufungwa mabao 2-0 na Stellah Abidjan ya Ivory Coast mwaka 1993
katika fainali ya pili ya Kombe la CAF Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Awali, Simba ilitoa sare ugenini na kuwapa matumaini Watanzania kwamba taji la kwanza kubwa Afrika lingetua nchini mwaka 1993.
Baada
ya mchezo wa leo wa fainali, kesho, Samatta na Ulimwengu watakwea pipa
kuelekea jijini Nairobi Kenya kujiunga na kikosi cha timu ya Taifa ya
Tanzania bara, Kilimanjaro Stars kinachojiandaa na mchezo wa pili wa
kombe la CECAFA dhidi ya Somalia desemba 2 mwaka huu.
Mchezo
wa kwanza, Kili Stars walitoka sare ya bao 1-1 dhidi ya waliowahi kuwa
mabingwa wa soka barani Afrika, timu ya Taifa ya Zambia maarufu kwa jina
la Chipolopolo.
No comments:
Post a Comment