Na Rose Itono
Mhariri na Msanifu Mkuu Msaidizi wa gazeti la Uhuru, Dunia Mzobora,
amefariki dunia usiku wa kuamkia jana katika Hospitali ya Taifa ya
Muhimbili (MNH) kutokana na ugonjwa wa shinikizo la damu.
Akizungumza kwa
njia ya simu jana, Mhariri Mtendaji wa gazeti la Uhuru, Josia Mufungo,
alisema marehemu kabla ya mauti yake alikuwa kazini kama kawaida ambapo
saa mbili usiku alimaliza kazi zake na kurejea nyumbani.
Alisema
usiku wa saa sita walipata taarifa kutoka kwa familia yake kuwa Dunia
amezidiwa na kukimbizwa haraka hospitali kwa ajili ya matibabu.
"Marehemu
alikimbizwa Hospitali ya Agha Khan lakini walishindwa na kuamua
kumpeleka Muhimbili kwa matibabu zaidi na saa 12 za asubuhi alifariki",
alisema.
Mufungo
alisema marehemu alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa shinikizo la damu
kwa muda mrefu na kuongeza kuwa msiba wake utafanyika nyumbani kwake
Tabata Kimanga, ambapo anatarajiwa kuzikwa leo saa 7.00 za mchana na
shughuli zote za mazishi zitakuwa hapo hapo nyumbani kwake.
Alisema
marehemu ameacha mjane na watoto watano. Alijiunga na gazeti la Uhuru
mwaka 1989 kama mwandishi mwanafunzi ambapo baadaye alipanda hadi
kufikia nafasi aliyokuwepo
No comments:
Post a Comment