Na Mwandishi Maalum
Waziri
Mkuu, Mizengo Pinda, amewataka maofisa mipango miji nchini kurekebisha
utendaji wao wa kazi ili waweze kubadili taswira mbaya iliyojengeka
miongoni mwa jamii dhidi yao.
Alitoa
kauli hiyo jana wakati akifungua Mkutano wa Kwanza wa Wataalam wa
Mipango miji waliosajiliwa na Bodi ya Usajili wa Wataalam wa Mipango
miji ulioanza jana jijini Dar es Salaam.
“Taswira
ya utendaji kazi katika taaluma ya mipango miji na katika sekta ya
ardhi kwa ujumla miongoni mwa wananchi na Serikali sio nzuri sana.
Watafiti wanatueleza kuwa kati ya asilimia 60 na 80 ya makazi kwenye miji yetu hapa nchini yamejengwa kiholela.
Na kwa kiwango hicho hicho wakazi wa mijini wako kwenye makazi hayo na wanaishi kiholela,î alisema.
“Wako
wanaosema ninyi ndiyo chanzo cha hiyo migogoro, wako wanaosema ninyi
kwa rushwa ndiyo wenyewe, mimi sishangai madai haya ila ninawasihi muwe
na roho ngumu katika kushinda vishawishi hivi,” alisisitiza.
Aliwataka
wajadili masuala yanayohusu migogoro ya ardhi baina ya wafugaji na
wakulima, baina ya mipaka ya vijiji, baina ya wilaya, baina ya
wanavijiji na hifadhi za Taifa au maeneo ya uchimbaji madini na kujadili
njia za kutatua migogoro hiyo ili kuwa na mipamgo endelevu.
Aliwataka
waangalie suala la ukuaji wa miji iliyokaribu na Jiji la Dar es Salaam
kwa kuangalia dhana ya miji mikubwa kubeba vijiji vinavyoizunguka na
hasa kuangalia uwezekano wa kupunguza mrundikano wa watu katika jiji
hilo.
“Miji
ya Kibaha, Mkuranga na Bagamoyo inatumikaje kusaidia kupunguza
msongamano katika jiji la Dar es Salaam,” Waziri Mkuu alihoji.
Alisema
wataalamu wa mipango miji wanapaswa kuwa na maono makubwa ya baadaye
kama kweli wanataka kupunguza majanga katika siku za usoni.
“Angalieni
utafiti wa gesi unaoendelea pale Mtwara na mjipange, angalieni mpango
wa ujenzi wa bandari ya Bagamoyo na kuunganisha na reli ya kati,
angalieni Lindi na upatikanaji wa Liquified Naturala Gas (LNG), pangeni
miji kwa siku za baadaye siyo sasa,” alisisitiza.
Aliwataka
wanataaluma hao wasimamie vyema taaluma yao kwani katika miaka 37
ijayo, (mwaka 2050) inakadiriwa kwamba nusu ya watu wote watakuwa
wakiishi mijini. “ Kuweni wakweli, tumieni weledi wenu la sivyo katika
miaka 37 ijayo kama wanavyosema watafiti, itakuwa balaa tupu,î alisema.
Mapema
akimkaribisha Waziri Mkuu kuzungumza na wataalamu hao kutoka mikoa yote
hapa nchini, Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Makazi, Prof. Anna
Tibaijuka, alisema maofisa mipango miji wanakabiliwa na changamoto ya
kufikiri na kubuni aina ya miji ambayo itakidhi mahitaji ya jamii ya
baadaye.
Alisema
hata hivyo maofisa hao wamekuwa wakikabiliwa na changamoto ya kushindwa
kutoa maamuzi au ushauri wa kitaalamu kwa kuhofia kuadhibiwa na
madiwani.
Wizara
ya Fedha. " Kwa nafasi yake ndiye alikuwa akishiriki kuandaa bajeti ya
upinzani bungeni, kuwasilisha bajeti ya wizara ya fedha akiwa waziri
kivuli, lakini kwa kuvuliwa wadhifa wake maana yake haaminiki tena,"
alisema mmoja wa watoa habari ndani ya chama hicho kwa sharti la jina
lake kutochapishwa gazetini.
Hata
hivyo, juhudi za kumpata Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa CHADEMA,
John Mnyika, ili kuweza kuzungumzia suala hilo ziligonga mwamba kutokana
na simu yake ya kiganjani kutopokelewa.
Wakati
huo huo, Jeshi la Polisi Makao Makuu jijini Dar es Salaam leo
linatarajia kufanya mahojiano na Katibu wa CHADEMA mkoa wa Dar es
Salaam, Henry Kileo, baada ya mahojiano hayo kukwama kufanyika jana
kutokana na malalamiko yanayodaiwa kuwasilishwa na Mbunge wa Kigoma
Kaskazini, Zitto Kabwe.
Mahojiano
hayo yalikuwa yafanyike Makao Makuu ya Jeshi la Polisi jijini Dar es
Salaam jana mchana, lakini yaliahirishwa muda mfupi baada ya Kileo
kuwasili akiwa na mwanasheria wake na makada wengine wa CHADEMA.
Baada
ya kufika maofisa wa Polisi walifanya mazungumzo na mwanasheria wake,
lakini baada ya muda walikubaliana yafanyike leo saa tano.
Akizungumza
na gazeti hili jana, Kileo, alisema awali mahojiano yalitakiwa
yafanyike jana saa nane mchana, lakini walichelewa kufika makao makuu ya
polisi kutokana na wakili wake kuchelewa kwani alikuwa na kesi makao
makuu ya Polisi.
Kileo,
alipoulizwa anatakiwa polisi kwa ajili ya makosa gani, alisema hana
taarifa kwa undani, kwani alipigiwa simu na ofisa aliyejitambulisha kwa
jina la Mbutta na kumwambia kuwa anatakiwa kufika makao makuu ya Polisi
kwa mahojiano kutokana na malalamiko ambayo Zitto, ameyafikisha.
"Niliambiwa
nahitajika kujibu tuhuma ambazo Zitto amezifikisha Polisi, lakini
sikuelezwa ni tuhuma gani hizo," alisema Kileo. Alipoulizwa ni kwa nini
Zitto apeleke shtaka hilo Makao Makuu ya Polisi, badala ya vituo vingine
kama ilivyo kawaida, Kilewo alijibu; "Mimi sijui labda wapigie polisi
ili muwaulize swali hilo."
Gazeti
moja (sio Majira) jana lilichapisha habari inayoeleza kuwa Zitto,
amemfungulia mashtaka Kileo akimtuhumu kusambaza waraka katika mitandao
ya kijamii unaomhusisha na mipango ya kufanya mapinduzi ya chama hicho.
No comments:
Post a Comment