Na Mwandishi Wetu
Rais
Jakaya Kikwete, amemtumia salamu za rambirambi Makamu Mwenyekiti wa
Chama Cha Mapinduzi (CCM), Philip Mangula, kufuatia kifo cha mtoto wake,
Peter Philip Mangula, kilichotokea juzi katika Hospitali ya Taifa ya
Muhimbili (MNH) alikokuwa amepelekwa kwa matibabu akisumbuliwa na
ugonjwa wa shinikizo la damu.
"Nimeshtushwa,
nimesikitishwa na kuhuzunishwa sana kutokana na taarifa za kifo cha
mwanao (Peter Philip Mangula)," alisema kwa masikitiko Rais Kikwete
katika salamu zake.
Rais
Kikwete aliongeza kusema kuwa; nasikitishwa zaidi na taarifa za kifo
hiki kwa kuzingatia kwamba ni katika kipindi kifupi kilichopita, Mangula
alimpoteza binti yake, Neema Nemela Mangula aliyefariki dunia kutokana
na ajali ya gari, hivyo ni dhahiri kwamba kifo cha kijana wake huyu
kimeongeza machungu na simanzi kwa familia ya Mangula na kimesababisha
pengo kubwa kwa wanafamilia kwa ujumla.
"Kutokana
na taarifa hizo za kusikitisha, ninakutumia wewe salamu zangu za
rambirambi na pole nyingi kwako wewe binafsi na kwa familia yako yote
kwa ujumla kwa kupotelewa na mtoto wako."
Alisema
anamuomba Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema mjalie yeye na familia yake
moyo wa uvumilivu na ujasiri ili kuhimili machungu ya kuondokewa na
kijana wao.
No comments:
Post a Comment