BARUA ZATOLEWA RASMI,WAPEWA SIKU 14
BAADA YA MAJIBU,KUJIELEZA KAMATI KUU
LISSU ADAI UTETEZI WAO ULIPOTOSHA UKWELI
Na Goodluck Hongo
Aliyekuwa
Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Bw.
Zitto Kabwe pamoja na wenzake, wameandaliwa mashtaka 11 kwa madai ya
kuandaa mapinduzi ya siri dhidi ya uongozi wa chama hicho kinyume cha
katiba.
Bw.
Kabwe na wenzake ambao ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya chama hicho, Dkt.
Kitila Mkumbo na Bw. Samson Mwigamba, aliyekuwa Mwenyekiti wa CHADEMA
jijini Arusha, jana walikabidhiwa barua rasmi ili wajieleze ndani ya
siku 14.
Mkurugenzi
wa Habari na Uenezi wa CHADEMA, Bw. John Mnyika, aliyasema hayo Dar es
Salaam jana wakati akizungumza na waandishi wa habari Makao Makuu ya
chama hicho.
Bw.
Mnyika ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Ubungo, Dar es Salaam, alisema
chama hicho kimeandaa mashtaka hayo baada ya Sekretarieti ya CHADEMA
kupitia maamuzi ya Kamati Kuu yaliyowavua nyadhifa za uongozi watuhumiwa
hao.
"Watuhumiwa
hawa watatakiwa kujieleza kwa maandishi ndani ya siku 14, baadaye
watajieleza mbele ya Kamati Kuu ambayo itatoa maamuzi ya hatua za
kuchukua," alisema Bw. Mnyika.
Alisema
mashtaka hayo yametokana na waraka wa siri ambao ulikamatwa na kutolewa
mbele ya Kamati Kuu unaowakashifu viongozi wakuu wa chama hicho.
"Wote
watatakiwa kujieleza kwa nini wasifukuzwe ndani ya chama chetu kwa
makosa waliyofanya... Kamati Kuu ya chama ndicho chombo chenye maamuzi
ya kuwaondoa viongozi au wanachama wanaokiuka Katiba.
"Waraka
uliochapishwa katika baadhi ya vyombo vya habari (si Majira) na
mitandao ya kijamii unaodaiwa kuwaponza Bw. Kabwe na wenzake si wenyewe
ni batili," alisema.
Aliongeza
kuwa, maamuzi yaliyofanywa na Kamati Kuu yalizingatia kanuni, sheria na
taratibu za chama kwa kufuata katiba, hivyo Bw. Kabwe na wenzake
hawakufukuzwa kwa sababu walizozitoa kwenye vyombo vya habari bali kwa
kuandika waraka wa kimapinduzi.
Msimamo wa CHADEMA
Bw.
Mnyika alisema, chama hicho hakipo tayari kuwavumilia viongozi na
wanachama wote ambao watakuwa kikwazo kwa chama hicho kufikia malengo
yake bila kujali cheo alichonacho.
"Wanatafuta
huruma kwa wananchi kutokana na makosa ambayo wameyafanya hasa la
kuandaa waraka wa siri, wao wenyewe walikiri kuhusika nao lakini
wanapotosha ukweli," alisema.
Alisema
Sekretarieti hiyo imepokea na kutoa mapendekezo mbalimbali ya
utekelezaji wa mikakati waliyojipangia ambayo ni Vuguvugu la Mabadiliko
(M4C) na "CHADEMA ni msingi".
Akizungumzia
uchomaji wa bendera za chama, ofisi, fulana na kuondoa mabango ya
CHADEMA, baada ya Bw. Kabwe na wenzake kuvuliwa nyadhifa za uongozi, Bw.
Mnyika alisema chama kimezisikia taarifa hizo.
"Uchunguzi
wa awali unaonesha kilichotokea ni kiini macho tu si wanachama wa chama
chetu waliofanya hivyo, viongozi wa maeneo husika wanaendelea na vikao,
usalama upo," alisema.
Tundu Lissu azungumza
Kwa
upande wake, Mwanasheria Mkuu wa CHADEMA, Bw. Tundu Lissu, alisema
watuhumiwa walifanya mkutano na vyombo vya habari kwa lengo la kupotosha
ukweli wa mambo juu ya mazingira halisi ya kuvuliwa nyadhifa zao.
"Hawakuondolewa
katika nyadhifa zao kwa sababu ya kuuza majimbo yetu ya uchaguzi mwaka
2010, si posho, wala uwepo wake kama Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya
Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), aliyeibua hoja ya kukaguliwa kwa
hesabu za vyama vya siasa.
"Amevuliwa nyadhifa hizo na wenzake kwa sababu ya kuandaa mapinduzi ndani ya chama kwa kukiuka maadili," alisema.
Akizungumzia
madai ya kugawanyika au kupasuka kwa chama hicho kama Bw. Kabwe
atafukuzwa uanacham, Bw. Lissu alisema kwa nyaraka alizoziona, Kabwe
alikuwepo katika kikao cha Kamati Kuu kilichomfukuza aliyekuwa Katibu
Mkuu wa chama hicho mwaka 2004, Dkt. Amaan Kabourou.
"Ka
bwe p i a a l i k uwe p o kwenye kikao cha Kamati Kuu kilichomfukuza
aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa chama hiki, marehemu Chacha Wangwe mwaka
2007; hivyo hata kikao kama hicho ndicho kilichowavua vyeo yeye na
wenzie hivyo Kamati Kuu isilaumiwe," alisema.
Bw.
Lissu alisema, madai ya Bw. Kabwe kudai alijitoa katika utiaji saini
katika masuala ya fedha ndani ya chama hicho kwanza hakuwahi kuwa mtiaji
saini ili kuidhinisha fedha, hivyo anashangaa kulizungumzia hilo wakati
hakuwahi kuwa mtiaji saini.
"Chama
kimepasuka mara nyingi tangu enzi ya Bw. Kabwe kuingia kwenye Kamati ya
Jaji Bomani, Chacha Wangwe, ugaidi wa Rwakatare hata sakata la mabomu
lakini tuliibuka upya, hadi sasa chama kinaendelea na mapambano yake,"
alisema.
Alipoulizwa
na waandishi kama viongozi hao wakiamua kuondoka, chama kimejipangaje,
alisema si vizuri kuwahukumu Bw. Kabwe na wenzake kwa sababu bado
hawajaanza kujitetea, lakini kugombea uongozi ndani ya chama si uhaini
wala dhambi.
Alibainisha
kuwa, sh. milioni 100 zilizotolewa na mfanyabiashara maarufu nchini,
Bw. Mustafa Sabodo, hesabu za matumizi yake zipo wazi na zilipelekwa
kwenye hesabu za chama hicho ili zikaguliwe na Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu
wa Hesabu za Serikali (CAG).
Aliongeza
kuwa, licha ya vyama vya siasa kuwa tayari kukaguliwa, CAG alishindwa
kukagua hesabu hizo kwa sababu ya ukosefu wa fedha, hivyo alivitaka
vyama husika kuwalipa wakaguzi ambao wangefanya ukaguzi huo jambo ambalo
walilipinga.
"Tuna
ushahidi wote kuhusu suala hili, hata Msajili mpya wa Vyama vya Siasa,
aliandika barua kwa CAG kuhusu kupinga vyama kuwalipa wakaguzi wa hesabu
kwani huo si utarabu wa Serikali, lakini tunamshangaa Kabwe kuzungumzia suala hili wakati analijua vizuri," alisema Bw. Lissu
No comments:
Post a Comment