AWASILISHA VIELELEZO KWA WASULUHISHI WA MGOGORO
Na Penina Malundo
Rais
Jakaya Kikwete, amewasilisha utetezi wa Tanzania kwa jopo la Marais
wastaafu wanaotafuta ufumbuzi wa mpaka wa Ziwa Nyasa, kati ya Tanzania
na Malawi.
Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. Bernard Membe,
aliyasema hayo Dar es Salaam jana wakati akizungumza na waandishi wa
habari.
Alisema
utetezi huo uliwasilishwa kwa Rais mstaafu wa Msumbiji Joaquim Chissano
ambaye ndiye Mwenyekiti wa jopo hilo na Rais mstaafu wa Botswana, Bw.
Festus Mogae.
Awali,
viongozi hao wastaafu walifanya mkutano kama huo Blantyre, nchini
Malawi ambapo juzi walisikiliza hoja za upande wa pili juu ya mgogoro
huo.
"Katika
mkutano huu, Rais Kikwete alitoa maelezo mazuri pamoja na vielelezo
mbalimbali... utetezi wetu ulikuwa wa kisayansi hivyo hatuna hofu yoyote
juu ya hili," alisema.
Bw.
Membe alisema, leo anatarajia kwenda Maputo, nchini Msumbiji,
kuwasilisha maelezo yaliyotolewa na Rais Kikwete mbele ya marais hao
wastaafu.
Aliongeza
kuwa, jopo la Wanasheria wa kimataifa bado linaendelea na kazi ya
kufanya utafiti juu ya mgogoro huo kwani jambo hilo kwa kuliangalia ni
dogo lakini ni kubwa.
Alisema
kuwa mgogoro huu unaweza kuwa na tambo mbalimbali kati ya nchi moja na
nyingine ingawa tambo hizo zinaweza kuleta athari kubwa kwa nchi hizo
hivyo utafiti zaidi unahitajika.
No comments:
Post a Comment