- HATIMA YA NAFASI ZA ZITTO KUJULIKANA KARIBUNI
- ALIYEMLALAMIKIA KUHOJIWA POLISI MAKAO MAKUU LEO
Kiongozi
wa Kambi Rasmi Upinzani Bungeni na Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman
Mbowe, anatazamiwa kufanya mabadiliko kwa Baraza lake la Mawaziri
Kivuli, wakati wowote katika kipindi cha Mkutano ujao wa Bunge ili
kutekeleza maagizo ya Kamati Kuu iliyokutana hivi karibuni na kumvua
wadhifa wake Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe.
Zitto
amevuliwa wadhifa wake wa Naibu Katibu Mkuu kutokana na kile
kinachodaiwa anahusika kuandaa waraka wa kufanya mapinduzi ya viongozi
ndani ya chama hicho.
Kwa
mujibu wa vyanzo vya habari kutoka ndani ya chama hicho vililiambia
gazeti hili kuwa Kamati Kuu ambayo ndiyo inasimamia Kambi Rasmi ya
Upinzani Bungeni, hivyo mara baada ya kutangaza kumvua Zitto, wadhifa
wake (unaibu katibu mkuu) ilielekezwa uanze mchakato wa kumuondoa kwenye
nafasi zake.
Bungeni, Zitto ni Naibu Kiongozi wa Kambi Rasmi akiwa msaidizi wa Mbowe na Waziri Kivuli wa
Wizara
ya Fedha. " Kwa nafasi yake ndiye alikuwa akishiriki kuandaa bajeti ya
upinzani bungeni, kuwasilisha bajeti ya wizara ya fedha akiwa waziri
kivuli, lakini kwa kuvuliwa wadhifa wake maana yake haaminiki tena,"
alisema mmoja wa watoa habari ndani ya chama hicho kwa sharti la jina
lake kutochapishwa gazetini.
Hata
hivyo, juhudi za kumpata Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa CHADEMA,
John Mnyika, ili kuweza kuzungumzia suala hilo ziligonga mwamba kutokana
na simu yake ya kiganjani kutopokelewa.
Wakati
huo huo, Jeshi la Polisi Makao Makuu jijini Dar es Salaam leo
linatarajia kufanya mahojiano na Katibu wa CHADEMA mkoa wa Dar es
Salaam, Henry Kileo, baada ya mahojiano hayo kukwama kufanyika jana
kutokana na malalamiko yanayodaiwa kuwasilishwa na Mbunge wa Kigoma
Kaskazini, Zitto Kabwe.
Mahojiano
hayo yalikuwa yafanyike Makao Makuu ya Jeshi la Polisi jijini Dar es
Salaam jana mchana, lakini yaliahirishwa muda mfupi baada ya Kileo
kuwasili akiwa na mwanasheria wake na makada wengine wa CHADEMA.
Baada
ya kufika maofisa wa Polisi walifanya mazungumzo na mwanasheria wake,
lakini baada ya muda walikubaliana yafanyike leo saa tano.
Akizungumza
na gazeti hili jana, Kileo, alisema awali mahojiano yalitakiwa
yafanyike jana saa nane mchana, lakini walichelewa kufika makao makuu ya
polisi kutokana na wakili wake kuchelewa kwani alikuwa na kesi makao
makuu ya Polisi.
Kileo,
alipoulizwa anatakiwa polisi kwa ajili ya makosa gani, alisema hana
taarifa kwa undani, kwani alipigiwa simu na ofisa aliyejitambulisha kwa
jina la Mbutta na kumwambia kuwa anatakiwa kufika makao makuu ya Polisi
kwa mahojiano kutokana na malalamiko ambayo Zitto, ameyafikisha.
"Niliambiwa
nahitajika kujibu tuhuma ambazo Zitto amezifikisha Polisi, lakini
sikuelezwa ni tuhuma gani hizo," alisema Kileo. Alipoulizwa ni kwa nini
Zitto apeleke shtaka hilo Makao Makuu ya Polisi, badala ya vituo vingine
kama ilivyo kawaida, Kilewo alijibu; "Mimi sijui labda wapigie polisi
ili muwaulize swali hilo."
Gazeti
moja (sio Majira) jana lilichapisha habari inayoeleza kuwa Zitto,
amemfungulia mashtaka Kileo akimtuhumu kusambaza waraka katika mitandao
ya kijamii unaomhusisha na mipango ya kufanya mapinduzi ya chama hicho
No comments:
Post a Comment