Siku moja baada ya gazeti hili kuripoti habari za watoto wanadaiwa
kutekwa na kufichwa katika handaki lililopo kwenye msitu wa Mabwepande,
Wilaya ya Kinondoni, Dar es Salaam, ambalo ndani yake kuna jengo kubwa
lenye vyumba, Jeshi la Polisi limeanza uchunguzi mkali, anaripoti Masau Bwire.
Chanzo
chetu cha habari kimedokeza kuwa, uchunguzi huo unafanywa na Jeshi la
Polisi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi
mkoani Pwani.
"Polisi
wapo katika uchunguzi mkali tangu leo (jana), asubuhi, si vyema kuzitoa
taarifa mapema kabla uchunguzi haujakamilika, tunaweza kuharibu
upelelezi na wahusika kukimbia.
"
Watoto wal i o j i o k o a w a m e p e l e k w a h o s p i t a l i
kuchunguzwa afya zao baada ya kuhojiwa na kutoa picha kamili ya eneo
lenye handaki, hivyo uchunguzi ukikamilika mtaambiwa," kilisema chanzo
hicho kwa sharti la kutotajwa jina lake.
Utekaji
watoto wanaodaiwa kuwa zaidi ya 60 katika handaki hilo, unadaiwa
kufanywa na raia wa kigeni (Wazungu), wakishirikiana na Watanzania
ambapo watoto hao hufungiwa katika vyumba hivyo, kuteswa, kulawitiwa na
kubakwa.
Watoto
waliodai kutoroka kwenye handaki hilo ni Emmanuel Robert (11) anayesoma
darasa la tano Shule ya Msingi Maendeleo iliyopo Tabata, Segerea, Dar
es Salaam na mdogo wake Godianus Robert (8), anayesoma darasa la tatu
shuleni hapo.
Watoto
hao walidai kutekwa na Wazungu wawili asubuhi ya Septemba 2 mwaka huu,
wakati wakienda shuleni na kufanikiwa kutoroka katika jengo hilo
Septemba 23 mwaka huu.
Wakiwa
wamechoka na afya zao kuzorota katika Kituo kidogo cha Polisi, Kibaha
Maili Moja, mkoani Pwani, watoto hao walisema ndani ya jengo hilo kuna
watoto wengi wa kike na kiume.
Wa
l i s e m a w a t o t o h a o wanafanyishwa kazi na kuteswa kwa
kutandikwa fimbo, kuchomwa moto na kupigwa shoti ya umeme hasa
wanapowaulizia wazazi wao ambapo baadhi yao hubakwa na kulawitiwa.
Akizungumza na Majira,
Emmanuel alisema baada ya kutekwa yeye na mdogo wake, walifungwa na
vitambaa vyeusi usoni hadi walipofikishwa ndani ya jumba hilo la mateso.
Aliiomba Serikali kufanya jitihada za hali na mali ili kuwaokoa watoto wengine waliopo katika jengo hilo.
Mama
mzazi wa watoto hao, Martha Godianus (29), ambaye anafanya shughuli za
mama lishe, njia panda ya Barakuda, Tabata Manispaa ya Ilala, alisema
amehangaika zaidi ya miezi mitatu kuwatafuta watoto hao bila mafanikio.
Juzi Kamanda wa Polisi mkoani Pwani, Ulrich Matei alikiri kupata taarifa
za tukio hilo na kuanza kuzifanyia kazi
No comments:
Post a Comment