Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu ( Tamisemi), Hawa Ghasia ameingia matatani
baada ya Chama cha Walimu Wilaya za Mbozi na Momba mkoani Mbeya
kumchongea jambo kwa Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana.
CWT kilidai Ghasia alikataa
kusomewa risala ya walimu wenye kero akidai anazijua, hivyo hana haja ya
kusikiliza. Kutokana na kauli hiyo, Kinana aliomba asomewe taarifa
hiyo.
Msoma taarifa,Leonard Nyamiye
alisema walimu wanaidai Serikali zaidi ya Sh1 bilioni za mishahara
,uhamisho na mengine mengi. Mwalimu huyo alisema kutolipwa madeni hayo
kumewafanya waichukie sana CCM na Serikali.
Akizungumza Kinana alisema suala
la Ghasia atalifikisha kwa mwajiri wake. Kinana ambaye katika ziara
yake amekuwa akikutana na viongozi wa CWT kila wilaya, alikiri kusikia
kero za walimu siku nyingi. ”Nakumbuka mwaka 2010 Rais Kikwete alikaa na
CWT Taifa kwa saa tisa ili kumaliza tatizo, lakini kila baada ya mwaka
linajitokeza”, alisema.
Kinana alisema sasa CCM
italivalia njuga na kwamba itajadili chanzo cha tatizo katika kikao cha
NEC ijayo. Hata hivyo alidokeza kuwa amegundua kwamba walimu hawana
mwajiri mmoja na ndiyo maana wanasumbuliwa.
Alisema
walimu kwa sasa wanashughulikiwa na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya
Ufundi, Tamisemi, Tume ya Ajira na Hazina jambo ambalo ni kero.
No comments:
Post a Comment