Na Mwandishi Wetu, Nairobi
Timu
ya taifa ya Tanzania Bara (Kilimanjaro Stars) inayodhaminiwa na bia ya
Kilimanjaro jana imeshuka uwanjani kumenyana na Zambia, katika mechi ya
ufunguzi ya michuano ya Kombe la Chalenji.
Kilimanjaro
Stars na Zambia zimechuana kuwania pointi tatu katika mchezo
uliochezwa Uwanja wa Machakos ulioko nje kidogo ya jiji la Nairobi.
Timu
hiyo ya Tanzania Bara iliyopangwa Kundi B, ilihitaji ushindi ili kupata
pointi tatu ambazo zingeiweka katika nafasi nzuri kwenye michuano hiyo.
Akizungumzia mchezo huo wa jana, Kocha Mkuu wa Kili Stars, Kim Poulsen alisema timu yake imeshindwa kupata ushindi kutokana na wachezaji wengi kuwa wachovu wa safari,
Alisema
kikosi chake kimefanya mazoezi magumu, amb a y o bado wachezaji wanauguza viungo vyao, hata hivyo kulikuwa na upinzani mkubwa dhidi ya Zambia inayosifika kwa kutandaza soka ya kiwango
bora Afrika.
Kilimanjaro
Stars iliwategemea zaidi wachezaji kama Mrisho Ngasa, Amri Kiemba, Erasto
Nyoni, Kelvin Yondani, Said Morad, Athuman Idd na Salum Abubakar.
Pia, wamo Frank Domayo, Himid Mao, Haruna Chanongo, Ramadhan Singano ‘Messi’, Farid Mussa na Elias Maguli.
Katika
mechi ya ufunguzi iliyochezwa juzi mchana timu ya taifa ya Zanzibar
iliifunga Sudan Kusini mabao 2-1 katika mchezo mkali uliokuwa na
ushindani.
No comments:
Post a Comment