Na Prosper Mgimwa, Katavi
Mahakama ya Wilaya ya Mpanda Mkoa wa Katavi imemuhukumu, Leonald
Wiliamu (19), mkazi wa Kijiji cha Mwese Namba Moja Wilaya ya Mpanda
kifungo cha maisha jela kwa tuhuma ya kumlawiti mtoto wa kiume mwenye
umri wa miaka saba (jina tunalo).
Hukumu hiyo ilitolewa na Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya
Mpanda, Chiganga Ntengwa, baada ya mahakama kutokuwa na mashaka na
ushahidi uliotolewa mahakamani wa mashtaka.
Katika
kesi hiyo ambayo ilikuwa na washtakiwa wawili mshtakiwa mwingine
alikuwa na umri wa 17 ambaye alihukumiwa adhabu kuchapwa viboko vinne
kutokana na kuwa na umri chini ya miaka 18.
Washtakiwa hao walidaiwa kutenda kosa hilo la kumlawiti mtoto huyo
Julai 31, mwaka huu saa mbili usiku nyumbani kwao. Watuhumiwa hao
walikuwa wameajiriwa kufanya kazi ya kuchunga mifugo kwa baba mzazi wa
mtoto huyo.
Akisoma hukumu hiyo, Hakimu Chiganga alisema baada ya kusikiliza
mwenendo mzima wa kesi, mahakama iliwaona washtakiwa wanakabiliwa na
kosa hilo la kulawiti.
Washtakiwa kabla ya kusomewa hukumu walipewa nafasi ya kujitetea,
ambapo waliiomba mahakama iwaachie huru kutokana kwa kile walichodai
kuwa walisingiziwa kutenda kosa hilo na baba wa mtoto huyo kwa kuwa
walikuwa wakimdai mshahara kwa muda mrefu.
Akisoma hukumu hiyo, Ntengwa alisema Wiliamu anahukumiwa kifungo cha
maisha jela baada ya kupatikana na hatia ya kumlawiti mtoto huyo na
mwenzake, Yohane anachapwa viboko vinne
No comments:
Post a Comment