Na Suleiman Abeid, Shinyanga
Wanachama
wa vikundi vya wajasiriamali wadogo katika kata ya Kitangili Manispaa
ya Shinyanga wametakiwa kuepuka kuingiza siasa katika vikundi vinginevyo
vitasambaratika
Tahadhari
hiyo ilitolewa juzi na diwani wa viti maalumu (CCM) manispaa ya
Shinyanga, Mariamu Nyangaka, alipokuwa akizungumza na viongozi wa vikund
imbalimbali vya wajasiriamali waliokutana kwa ajili ya kuanzisha Chama
cha Ushirika wa Akiba na Mikopo (SACCOS ).
Nyangaka
alisema viongozi wa vikundi vya wajasiriamali pamoja na wanachama wao
kwa ujumla wanatakiwa kuhakikisha wanaendesha shughuli zao bila kuingiza
au kutanguliza itikadi ya vyama vya siasa katika vikundi vyao kitu
ambacho kinaweza kusababisha mgawanyiko miongoni mwao.
Alisema
wapo baadhi ya wanasiasa wanaotumia wajasiriamali wadogo kufikia
malengo yao waliyojipangia huku wengine wakidiriki hata kuwazuia wafuasi
wa vyama vyao wasishirikiane na watu ambao si wafuasi wa vyama vyao vya
siasa hata kama shughuli zao zinapaswa kuendeshwa kwa ushirikiano wa
pamoja.
"Ndugu
zangu mkakati ambao mnataka kuuanzisha ni mkakati mzuri utawasaidia
kuendesha shughuli zenu kwa ufanisi mkubwa, mtakapokuwa na SACCOS yenu
itawasaidia kuweza kupata mitaji ya kuendesha biashara zenu kupitia
mikopo mtakayokopa yenye masharti nafuu tofauti na inayotolewa na benki
zetu nyingi nchini,"alisema.
"Lakini
naomba mjihadhari na siasa katika vikundi vyenu, mkimruhusu mdudu huyu
kuwa miongoni mwenu eleweni wazi hamtadumu kwa kipindi kirefu,
hakikisheni mnaendesha shughuli zenu bila kuchanganya na itikadi za
kisiasa na wakemeeni wale wote watakaoonesha dalili za kuingiza siasa
ndani ya vikundi," alisema Nyangaka.
Kwa
upande wake ofisa ushirika kutoka manispaa ya Shinyanga, Athumani,
alisema serikali kwa kipindi kirefu imekuwa ikihimiza umuhimu wa
wananchi kujiundia vyama vyao vya ushirika wa akiba na mikopo (SACCOS)
kwa vile ni rahisi zaidi kusaidiwa na asasi mbalimbali za kifedha.
Alisema kupitia SACCOS watu wengi wamefanikiwa katika biashara zao na
baadhi wameweza kujenga nyumba za makazi huku wengine wakisomesha watoto
wao bila matatizo. Alisema jambo la msingi ni uaminifu wa viongozi wa
SACCOS zinazoanzishwa kwa kuhakikisha zinakuwa na wanachama waadilifu na
wenye kuzingatia sheria za uendeshaji wa ushirika huo.
Katika
hatua nyingine, viongozi hao wa vikundi vya wajasiriamali wadogo
wameunda uongozi wa muda utakaosimamia taratibu za uanzishwaji wa
ushirika wa akiba na mikopo.
Alisema
utaundwa na vikundi vyote vilivyopo katika kata ya Kitangili na
kuhakikisha SACCOS hiyo inasajiliwa kisheria ili iweze kuanza kazi mara
moja.
Viongozi
wa muda waliochaguliwa Elias Joseph (Mwenyekiti), Richard Maige
(mwenyekiti msaidizi), Patrick Kileo (katibu), Masunga Elias (katibu
msaidizi) ambapo Timothy Kakiri, alichaguliwa kuwa mweka hazina.
No comments:
Post a Comment