Na Mwandi shi Maalumu, Panama
Mkurugenzi
Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU),
Dkt. Edward Hoseah, amechaguliwa kuwa Makamu wa Rais wa Shirikisho la
Taasisi za Kuzuia na Kupambana na Rushwa Duniani (IAACA).
Dkt.
Hoseah alichaguliwa na wajumbe 460 wa Mkutano Mkuu wa saba wa
shirikisho hilo kutoka nchi mbalimbali uliofanyika Panama, Amerika ya
Kati kuanzia Novemba 22-24, mwaka huu.
Wajumbe
wa mkutano huo ni pamoja na wakuu wa taasisi 98 za Kuzuia na Kupambana
na Rushwa Duniani ambapo kaulimbiu ya mkutano huo inasema, "Utawala wa
Sheria na Rushwa: Changamoto na Fursa Zilizopo".
Kabla
ya kuchaguliwa katika nafasi hiyo, Dkt. Hoseah alikuwa Mjumbe wa Kamati
Kuu ya Utendaji katika shirikisho hilo ambapo kutokana na uteuzi huo,
anakuwa Mwafrika wa kwanza kushika wadhifa huo mkubwa katika mapambano
dhidi ya rushwa duniani.
Uchaguzi
huo ni heshima kubwa kwa Tanzania na Bara la Afrika pia ni fursa nzuri
kwa Dkt. Hoseah kuonesha uwezo wake wa kuongoza mapambano dhidi ya
rushwa kimataifa. Nyadhifa nyingine za kimataifa ambazo Dkt. Hoseah
amewahi kuzishikilia ni pamoja na Rais wa
Kwanza
wa Shirikisho la Taasisi za Kuzuia na Kupambana na Rushwa Afrika
Mashariki (2007-2008), Rais wa kwanza wa Jukwaa la Taasisi za Kuzuia na
Kupambana na Rushwa katika nchi za SADC (SAFAC-2010-2011).
Nyingine ni Mwenyekiti wa Bodi ya Umoja wa Afrika ya Ushauri wa Masuala ya Rushwa (AU-ABC 2011-2012).
IAACA
linajumuisha taasisi 298 pamoja na wanachama zaidi ya 2,000 kutoka
katika asasi mbalimbali zisizo za kiserikali na lilianzishwa Aprili 19,
2006, Makao Makuu yapo Peking, China.
Lengo
la kuanzishwa kwa shirikisho hilo ni kuziwezesha nchi wanachama
kutekeleza Mkataba wa Umoja wa Mataifa Dhidi ya Rushwa uliopitishwa na
Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Desemba 30, 2003.
No comments:
Post a Comment