…………………………………………………………………..
Dar es Salaam. Utafiti
uliofanywa hivi karibuni na Taasisi ya Twaweza unaonyesha kuwa licha ya
kuwapo sababu nyingine zinazochangia kutokea kwa ajali za kuporomoka kwa
majengo, rushwa inaonekana kuwa chanzo kikuu cha kukithiri kwa hali
hiyo.
Ripoti ya utafiti huo inaeleza
kuwa rushwa imekuwa ikichangia kwa kiasi kikuba majengo mengi kujengwa
chini ya kiwango, hali inayochangia kutokea kwa majanga mbalimbali
yanayogharimu maisha ya Watanzania.
Utafiti huo umekuja kufuatia
tukio la Machi 29 mwaka huu ambapo jengo la ghorofa 36 katika Mtaa wa
Indira gandhi liliporomoka na kusababisha vifo na wengine kadhaa
kujeruhiwa.
Akiwasilisha ripoti hiyo, mmoja
wa watafiti kutoka katika mradi wa Sikiliza, Dk Thomas Maqway alisema
licha ya serikali kusisitiza kuchukua hatua mbalimbali lakini utafiti
huo unaonyesha kuwa wananchi hawana imani na mfumo wa kisheria katika
kuwawajibisha na kuwaadhibu wanaohusika kusababisha ajali zinazotokana
na majengo kuporomoka.
Alisema hali hiyo inatokana na
mfumo wa rushwa unaonekana kutawala katika ujengaji wa majengo kuanzia
ukandarasi, usanifu, vifaa, ujenzi hadi kwenye ukaguzi wa majengo
katika jiji ji la Dar es Salaam.
“Asilimia
78 ya wahojiwa walioshiriki katika utafiti huu wanataja rushwa ndiyo
sababu ya kuendelea kutokea kwa hali hii, hivyo hata uwajibishwaji wa
wahusika hawana imani.
No comments:
Post a Comment