Asteria Muhozya, Dar es Salaam
Nchi za Zambia, Tanzania na Kenya zimesaini Mkataba wa Makubaliano
kuonesha dhamira ya Serikali ya nchi hizo kujenga miundombinu ya pamoja
ya kusafirisha umeme (ZTK) na kufanya biashara ya kuuziana umeme wa
ziada baina ya nchi hizo na nchi nyingine barani Afrika. Akiongea katika
hafla hiyo Waziri wa Nishati na Madini, Tanzania Profesa Sospeter
Muhongo ameeleza kuwa, mradi huo wa pamoja unalenga kuondoa tatizo la
upungufu wa nishati ya umeme baina ya nchi hizo na nchi nyingine barani
Afrika jambo ambalo litachangia katika kukuza uchumi wa mataifa hayo.
Naye, Waziri wa Migodi, Nishati na Maendeleo ya Maji wa Zambia ,
Christopher Yaruma ameeleza kuwa, utekelezaji wa mradi huo sio tu
utaziwezesha nchi hizo kufanya biashara bali pia utafungua fursa za
uwekezaji na kusaidia katika kuondoa umaskini miongoni mwa nchi
wanachama kutokana kuzitumia fursa mbalimbali zinazotokana na nishati ya
umeme. Kwa upande wake Waziri wa Nishati na Petroli Kenya, Davis
Chirchir amewataka washirika wa maendeleo kusaidia katika kuwezesha
utekelezaji wa mradi huo wa kujenga miundombinu ya pamoja ya kusafirisha
umeme baina ya nchi hizo kutokana na manufaa yake kwa bara la Afrika na
kuongeza kuwa, kutokana na uwepo wa rasilimali asilia za kutosha katika
nchi hizo hakuna sababu ya kuwepo tatizo la nishati katika nchi hizo na
barani Afrika. Naye, Katibu Mkuu Msaidizi wa Jumuiya ya Soko la pamoja
la nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika anayeshughulikia miradi
(COMESA), Dkt. Kipyego Cheluget amezipongeza nchi hizo kwa kuuendeleza
utekelezaji wa mradi huo ambao umechukua kipindi kirefu na kuueleza
kuwa, ni miongoni mwa miradi 16 ya kipaumbele na kimaendeleo kwa Afrika.
Aidha, kwa upande wao Washirika wa maendeleo waliohudhuria hafla hiyo,
wameonesha kufurahishwa kwao na dhamira ya nchi hizo na kuahidi
kushirikana na nchi hizo kuhakikisha mradi huo unatekelezwa. Miongoni
mwa washirika wa maendeleo waliohudhuria ni pamoja na uwakilishi wa
Umoja wa Ulaya, Benki ya Dunia, Ubalozi wa Norway, Shirika la Maendeleo
la Japani (JICA), African Development Bank(AfDB) na Ubalozi wa Ufaransa.
TAN
Bayport
Kikoa
Myway entertainment
FORE PLAN CLINIC
MPINGA CUP 2016
Mashujaa Fm 89.3, Lindi
Wednesday, October 1, 2014
TANZANIA, ZAMBIA, NA KENYA ZASAINI MKATABA KUJENGA MIUNDOMBINU YA UMEME.
PROFESA SOSPETER MUHONGO ASAINI MKATABA WA MRADI WA KUUZIANA UMEME KATIA YA ZAMBIA, TANZANIA NA KENYA.
Katika utiaji saini Mkataba huo,
Profesa Muhongo alisema kuwa mchakato wa kuandaa Mkataba wa mradi huo
ulikwishafanyika tangu mwaka 2001 ambapo ulikuwa na vipengele ambavyo
kwasasa Mawaziri wa Nishati toka nchi zote tatu wameupitia na umefanyiwa
marekebisho.
Profesa Muhonga alisema kuwa
katika marekebisho hayo wamebadili kipengele kilichokuwa kinaeleza juu
ya uwepo wa Ofisi moja itakayosimamia mradi huo katika nchi zote tatu,
na badala yake wamekubaliana kuwa kila nchi ijisimamie yenyewe badala ya
kuwa na Ofisi moja pekee itakayosimamia mradi huo.
“Kwa upande wa Tanzania ujenzi
wa mradi huu umeshaanza kazi na mpaka hivi sasa asilimia 90 ya vifaa vya
ujenzi wa mradi vimeshawasili katika eneo la ujenzi,”alisema Profesa
Muhongo.
Akizungumzia maeneo ambayo mradi
huo utapita kwa upande wa Tanzania, Profesa Muhongo alisema kuwa, mradi
huo utapita maeneo ya mikoa ya Singida- Arusha-Namanga, na
Namanga-Isinya kwa Kenya, kwa upande wa Zambia utapita Mbeya–Iringa na
Iringa-Singida-Shinyanga. Ambapo unatarajia kusambaza umeme wa kuanzia
400kV.
Naye Katibu Mkuu wa Nishati
nchini Kenya, Mhandisi Joseph Njoroge alisema kuwa muungano huo wan chi
tatu utasaidia kupunguza tatizo la umeme katika nchi zote na Afrika kwa
ujumla kwani utapunguza gharama ya umeme pamoja na kuongeza ukuaji wa
uchumi katika uzalishaji.
Aidha aliongeza kuwa Serikali
yake itahakikisha kuwa Mkataba huo ndani ya siku Thelathini zijazo kabla
ya mkutano ujao kuanza, Mwanasheria Mkuu wa Kenya atakuwa umekwisha
usaini.
Kwa upande wake Waziri wa
Nishati na Madini nchini Zambia, Mh. Christopher Yaruma alisema kuwa
nchi yake imeshasaini Mkataba wa kuonyesha dhamira ya kuuziana umeme na
nchi ya Malawi, Namibia na Botswana.
Utiaji saini wa Mkataba huo
ulihusisha wadau mbalimbali wa maendeleo na wafadhili ikiwemo JICA,
COMESA, EU, Korea, Benki ya Dunia, AFD, Ufaransa na Mabalozi wa nchi
mbalimbali, ambapo wadau hao wameonyesha nia ya dhati katika kuendelea
kuisaidia Serikali hususani katika sekta ya Nishati.
Sambamba na hilo, mkutano wa
mwendelezo wa mradi huo badaa ya kuwa umesainiwa na viongozi wa Sheria
katika nchi husika unatarajiwa tena kufanyika mwanzoni mwa mwezi wa Kumi
na moja nchini Lusaka, Zambia.
PROGRAMU YA KUFUNDISHA HISABATI KWA KUTUMIA SIMU ZA MKONONI YAZINDULIWA DAR ES SALAAM
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mawasiliano Sayansi na Teknolojia, John Mgodo akizungumza katika uzinduzi huo.
Mtaalamu wa mradi huo kutoka Kampuni ya Nokia, Riita Vanska. (Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)
Meneja
Mkuu wa Tigo, Diego Gutierrez akizungumza katika uzinduzi huo. Kampuni
ya Tigo, Nokia na Microsoft ndio wadau mpango huo.
Meneja Mawasiliano wa Microsoft Mobile Devices, Lilian Nganda akitoa neno la ukaribisho kwa wageni waalikwa.
Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Sayansi na
Teknolojia Dk.Hassan Mshinda akizungumza katika
uzinduzi huo.
Viongozi mbalimbali wakiwa meza kuu wakati wa uzinduzi huo.
Naibu
Katibu Mkuu Wizara ya Mawasiliano Sayansi na Teknolojia, John Mgodo
(katikati), akiangalia simu wakati akiwaelekeza namna ya kutumia simu
wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Azania, Peter Riima (kushoto) na
Mrashani Katebeleza, wakati wa uzinduzi wa Programu ya kuwawezesha
wanafunzi kujifunza somo la hisabati kwa kutumia simu za mkononi na
vifaa vingine vya kielektroniki Dar es Salaam leo. Kulia ni Meneja Mkuu
wa Tigo, Diego Gutierrez.
Hapa uzinduzi huo ukifanyika.
‘ Ni kama anasema’ Niacheni nipo kazini nachukua tukio hili nikawahabarishe wengine, chezea mimi nyiee
Wadau mbalimbali na wanahabari wakiwa kwenye
hafla hiyo ya uzinduzi.
Wadau na wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana wa Jangwani wakiwa kwenye uzinduzi huo.
Dotto Mwaibale
WANAFUNZI
nchini wametakiwa kutumia mitandao hasa ya simu za mikononi kwa ajili
ya kujifunzia masomo mbalimbali badala ya kutumia katika matumizi
yasiofaa.
Mwito
huo umetolewa na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mawasiliano Sayansi na
Teknolojia, John Mgodo wakati wa uzinduzi wa Programu ya kuwawezesha
wanafunzi kujifunza somo la hisabati kwa kutumia simu za mkononi na
vifaa vingine vya kielektroniki uliofanyika Dar es Salaam leo.
Alisema
progamu hiyo imefika wakati muafaka na itawasaidia wanafunzi kujifunza
somo hilo muhimu katika ulimwengu wa sayansi na teknolojia.
Alisema
programu hiyo imeletwa nchini na Kampuni ya Nokia, Tigo kwa
kushirikiana na Microsoft, ambapo serikali kupitia Tume ya Taifa ya
Sayansi na Teknolojia (Costech) inasimamia kwa karibu mpango huo.
Alisema
Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi katika programu hiyo imesaidia
kupata mahudhui ya kihisabati jambo litakalo wasaidia wanafunzi kuwa
makini kitaaluma.
Alisema
matumizi hayo ya simu katika kujifunza hisabati yatakuwa yakifanyika
katika muda wa ziada baada ya masomo kwa vile licha ya wanafunzi
kumiliki simu lakini hawaruhusiwi kuwa nazo mashuleni.
Mgodo alisema mpango huo kwa sasa upo katika majaribio ukifanikiwa wanaweza kuuingiza katika mitaala ya taifa.
Mtaalamu
wa mradi huo kutoka Kampuni ya Nokia, Riita Vanska alisema mpango huo
umekuwa ukiongeza weredi kwa wanafunzi katika somo la hisabati na ni
muhimu katika kipindi hiki cha maendeleo ya Sayansi na Teknolojia.
Mkurugenzi
Mkuu wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia Dk.Hassan Mshinda
alisema tume hiyo ilifanyamchakato na kuukubali mpango huo ambao ni
muhimu hasa katika kipindi hiki ambacho taifa linaupungufu mkubwa wa
wataalamu wa sayansi wanaotokana na kufaulu kwa somo la hisabati.
“Mradi huu tuliona unafaa kwani utasaidia kuongeza wanasayansi hivyo tuliupokea kwa mikono miwili” alisema Dk.Mshinda.
Serikali Mkoani Tanga yachukua Tahadhari Mlipuko wa Ugonjwa wa Ebola
SERIKALI imetoa rai kwa wananchi
kutoa taarifa kwa mgonjwa yeyote mwenye dalili ya ugonjwa wa Ebora ili
aweze kupati msaada wa kitabibu hali ambayo itapunguza maambuzi kwa watu
wengi .
Rai hiyo imetolewa na Mkuu wa
Wilya ya Tanga wakati akifungua kikao cha maelekezo huhusu ugonjwa
hatari wa Ebola na dhana ya ushirikiano baina ya Sekta binafsi na Sekta
ya Umma kwa madaktari na wauguzi kutoka serikalini na sekta binafsi
kilichofanyika leo katika ukumbi wa Rodasaksa Hospiali ya Mkoa wa Tanga
(Bombo).
Kikao hicho ni moja ya jitihada
ambazo zinachukuliwa na Mkoa wa Tanga katika kutoa uelewa wa ugonjwa
huo hatari ambao sasa umekuwa tishio katika baadhi ya maeneo ya Afrika.
Vile vile ametoa wito kwa sekta ya umma na sekta binafsi kuweka nguvu
zao pamoja katika kuhakikisha wanachi wanapata huduma bora za afya.
Akielezea mkakati wa Mkoa dhidi ya
jinsi gani Mkoa umejiandaa endapo atapatikana mgonjwa wa Ebola katika
Mkoa wa Tanga, Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tanga Dr Asha Mahita
amesema kuwa tayari maeneo mbalimbali yenye vifaa maalumu yametengwa ili
kutoa huduma ya kitabibu kwa wagonjwa wa aina hiyo. Maeneo hayo ni
pamoja na eneo la Masiwani lilipo jengo la Hospitali ya Wilaya ya Tanga
na kituo kingine kipo Mpakani Horohoro.
Serikali pia imekuchukua tahadhali
katika maeneo ya mpakani hasa eneo la Horohoro mpaka wa Tanzania na
Kenye na uwanja wa ndege kwa kuweka kifaa maalumu cha kuweza kupima na
kutambua msafiri mwenye maambukizi ya Ugonjwa wa Ebola. Hatua ambayo
imefikiwa baada ya kusikia kuwepo mlipuko wa ugonjwa huo katika nchi za
jirani na hasa Afrika.
Akifafanua dhana ya ushirikiano
kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi katika kutoa huduma za afya,
Dr.Samweli Ogillo ambaye ni Mtendaji Mkuu kutoka chama cha Watoa huduma
Binafsi Nchini ( APHFTA)amesema ni jambo la msingi iwapo Serikali na
Sekta binafsi zitaweka nguvu ya pamoja ili kudhibiti na kuzuia ebola
kuingia nchini kwa sababu upande mmoja peke yake hauwezi.
Hadi sasa hakuna mgonjwa yeyote
mwenye dalili ya ugonjwa wa Ebola ambaye ameripotiwa kupatikana katika
nchi ya Tanzania. Historia inaonyesha mwaka 2012 Mwezi wa Julai
ulitokea mlipuko wa ugonjwa wa Ebola magharibi mwa Uganda eneo linaitwa
Kabaale ambapo zaidi ya watu 14 walipoteza maisha.
Ebola ni ugonjwa hatari
unaosababishwa na virusi vijulikanavyo kwa lugha ya kitaalamu “Ebola
Virusi na husambaa kwa haraka sana . Dalili zake ni pamoja na homa kali
inayoambatana na kutokwa damu katika matundu yote ya mwili kama pua,
njia ya haja kubwa na ndogo, mdomoni, machoni kutapika na kuharisha
damu. Stori & Picha na Monica Laurent, Afisa Habari Tanga
RAIS KIKWETE AREJEA NCHINI KUTOKA MAREKANI KWENYE MKUTANO WA 69 WA UMOJA WA MATAIFA
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Saidi
Meck Sadik baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa
Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Septemba 30, 2014 akitokea
Marekani alikohudhuria Mkutano wa 69 wa Umoja wa Mataifa.
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la
Wananchi Tanzania (JWTZ), Luteni Jenerali Samuel Ndomba mara baada ya
kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini
Dar es salaam leo Septemba 30, 2014 akitokea Marekani alikohudhuria
Mkutano wa 69 wa Umoja wa Mataifa.
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na IGP Ernest Mangu, Mnadhimu Mkuu wa
Jeshi la Ulinzi la Wananchi Tanzania (JWTZ), Luteni Jenerali Samuel
Ndomba na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Saidi Meck Sadik baada ya
kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini
Dar es salaam leo Septemba 30, 2014 akitokea Marekani alikohudhuria
Mkutano wa 69 wa Umoja wa Mataifa.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete
akilakiwa na wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama baada ya kuwasili
katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es
salaam leo Septemba 30, 2014 akitokea Marekani alikohudhuria Mkutano wa
69 wa Umoja wa Mataifa.
PICHA NA IKULU
Wazee walalamikia kunyanyapaliwa na wahuduma wa Afya
Wazee wakiwa kwenye kongamano la
wazee kwenye ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Mpanda kujadili
changamoto zinazowakabili wakati wa kupatiwa matibabu.
Na Kibada Kibada-Katavi.
Wahudumu wa Afya wameendelea
kuwanyanyapaa wazee wawapo hospitalini kupata huduma ya Afya kwa
kuwaacha wakae asubuhi hadi jioni ,huku wenyewe wakifanya kazi zao
nyingine.
Pia wakitibiwa na Daktari mara
nyingi huambiwa wakatafute dawa madukani hata kama zipo hospitalini na
ukiuliza kwa nini hujibu hawahitaji usumbufu.
Hayo yameelezwa na Katibu wa
Shirika la Wazee saidia lenye makao yake Wilayani Kasulu Mkoani
Cotlida Kokupima wakati akiwasilisha salamu za wazee kutoka Mkoani
kigoma kwenye kongamano la wazee lililofanyika Mjini Mpanda Mkoa wa
Katavi.
Bibi Kokupima ameeleza
changamoto zinazowakabiliwa wazee katika maeneo mbalimbali zikiwemo na
manyanyaso hayo wanayofanyiwa wazee wakiwa katika Zahanati,Vituo vya
Afya Pamoja na Kwenye Hospitali mbalimbali hapa nchini.
Changamoto hizo ni kuwa wakienda
kutibiwa na wakishaandikiwa dawa wanaambiwa hazipo waende wakanunue
madukani wakati mwingine wanakuwa hawana hela matokeo yake wanarudi
nyumbani kulala bila kupata dawa na mwisho ni kufa.
Changamoto ya usafiri kutoka
nyumba hadi kufika kwenye huduma za jamii hasa matibabu kwa wazee wenye
umri mkubwa ni taabu,hawana uwezo wa kuzifuata dawa dukani hata kama
watakuwa na fedha.
Kwa Upande wake mwakilishi wa
shirika la Afya la Wazee Duniani Athman Daniel ameeleza kuwa shirika
lake kwa kusaidiana na wadau mbalimbali na wazee limeweza kuchangia
kuisukuma serikali kuona uwezekano wa kuwapatia wazee malipo ya uzeeni
na mchakato unaenda vizuri na wakati wowote suala hilo litafanikiwa.
Akizungumzia Halmashauri ya
Mpanda amesifu juhudi zilizofanywa katika kuwahudumia wazee kwa kutenga
chumba cha kiliniki ya wazee na wanapatiwa huduma hapo.
Kauli mbiu ya mwaka huu ni “WAZEE WASIACHWE NYUMA TUJENGE JAMII SHIRIKISHI KUPITISHA SHERIA YAO.
NYUSI AKUTANA NA WANAMSUMBIJI WA ZANZIBAR
Mgombea
wa Urais wa Msumbiji kupitia chama cha FRELIMO Mh.Filipe Nyusi akipokea
zawadi kutoka kwa Jumuiya ya watu wa Msumbiji wanaoishi Zanzibar.
Mgombea
wa Urais wa Msumbiji kupitia chama cha FRELIMO Mh.Filipe Nyusi
akizungumza na Wananchi wa Msumbiji wanaoishi Tanzania ambapo alitumia
fursa hiyo kuwaomba wampigie kura kwani amekuja na mikakati mizuri ya
kuboresha uchumi ambapo amedhamiria kuiondoa Msumbiji kwenye orodha ya
nchi masikini,pia aliahidi kuwawezesha wakina Mama wa Msumbiji.
Wananchi
wa Msumbiji wanaoishi Zanzibar wakisikiliza sera za Mgombea wa Urais wa
Msumbiji kupitia chama cha FRELIMO Mh.Filipe Nyusi kwenye mkutano
uliofanyika katika Hotel ya Zanzibar Beach Resort.
Mgombea
wa Urais wa Msumbiji kupitia chama cha FRELIMO Mh.Filipe Nyusi
akiongozana na Mwenyekiti wa Jumuiya ya watu wa Msumbiji wanaoishi
Zanzibar Asilia Lunji baada ya kumaliza mkutano wake wa kampeni kwa
wapiga kura wanaoishi Zanzibar,Nyusi aliwaambia kuwa amefanya mkutano wa
kwanza nchini Tanzania kwa sababu ya mahusiano mazuri baina ya Msumbiji
na TanzaniaDK.SHEIN AWAAPISHA WAKUU WAPYA WA WILAYA PEMBA
Azam yadhamini maonesho makubwa ya Keki Dar
Mkurugenzi
wa Kampuni ya Insights Productions Limited, Marion Elias (kulia)
akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya maonesho
makubwa ya keki yanayotarajia kufanyika jijini Dar es Salaam. Kulia ni
Mratibu wa Matangazo na Uhusiano wa Umma wa kampuni ya SSB, Mohammed
Ramadhan wazamini wa maonesho hayo.
Mkurugenzi
wa Kampuni ya Insights Productions Limited, Marion Elias (kulia)
akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya maonesho
makubwa ya keki yanayotarajia kufanyika jijini Dar es Salaam. Kulia ni
Mratibu wa Matangazo na Uhusiano wa Umma wa kampuni ya SSB, Mohammed
Ramadhan wazamini wa maonesho hayo.
Mratibu
wa Matangazo na Uhusiano wa Umma wa kampuni ya SSB, Mohammed Ramadhan
(kushoto) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya
maonesho makubwa ya keki yanayotarajia kufanyika jijini Dar es Salaam.
Kulia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Insights Productions Limited, Marion
Elias.
Mkurugenzi
wa Kampuni ya Insights Productions Limited, Marion Elias (kulia)
akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya maonesho
makubwa ya keki yanayotarajia kufanyika jijini Dar es Salaam. Katikati
ni Mratibu wa Matangazo na Uhusiano wa Umma wa kampuni ya SSB, Mohammed
Ramadhan wazamini wa maonesho hayo na kulia ni Meneja Bidhaa za Azam,
Abubakar Suleiman.
Dar es Salaam
KAMPUNI ya Insights Productions
Limited kwa udhamini wa Kampuni ya Azam Tanzania imeandaa maonesho
makubwa ya keki yanayotarajia kufanyika jijini Dar es Salaam na
kuwakutanisha wadau mbalimbali wa uandaaji na utayarishaji wa keki.
Maonesho hayo yatajulikana kama ‘Azam World of Cakes Exhibition’.
Akizungumza na vyombo vya habari
leo jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Kampuni ya Insights Productions
Limited, Marion Elias alisema maonesho hayo yanatarajiwa kuwakutanisha
wadau mbalimbali binafsi, makampuni na taasisi waandaaji wa keki nchini
Tanzania ikiwa ni sehemu ya kubadilishana uzoefu na kujifunza ubunifu
zaidi wa shughuli hizo.
Bi. Elias alisema dhumuni la
maonesho hayo ambayo yanatarajiwa kufanyika Desemba 6, 2014 jijini Dar
es Salaam ni pamoja na kusherehekea taaluma ya uokaji keki kwa kuonesha
ubunifu na utaalam wa utengenezaji na upambaji wa keki bidhaa
inayopendwa na watu wengi na kutumika katika shughuli anuai za kijamii.
Alisema washiriki wa tamasha hilo mbali na kushindanisha na kuonesha
bidhaa zao za keki pia wanatarajia kupata semina ya mafunzo juu ya
utengenezaji bora wa keki ikiwa na lengo la kuboresha zaidi taaluma zao.
Alisema washiriki hao pia
watafanya maonesho ya utayarishaji wa vyombo vya kutengenezea keki,
utayarishaji wa unga wa ngano kwa ajili ya kupikia keki, kutambua unga
bora wa keki, uchanganyaji wa unga na viungo vingine kwa ajili ya
uboreshaji wa radha ya keki.
Alisema maonesho mengine
yatakayofanywa na wadau hao wa keki ni pamoja na uhifadhi bora wa keki
kwa muda mrefu bila kuharibika na washiriki kuonesha maumbo mbalimbali
ya keki yenye mvuto kwa watumiaji wa keki na jamii nzima.
Alisema maonesho hayo
yanayodhaminiwa na Azam watengenezaji wa unga bora kwa ajili ya
kutengenezea bidhaa hiyo, yatawashindanisha wadau wa uandaaji keki na
pia washindi watakao tajwa na majaji wa maonesho watajipatia fedha
taslimu na bidhaa mbalimbali.
“…Onesho hili litahusisha jamii
yote inayojishughulisha na utengenezaji wa keki, upambaji wa keki,
wauzaji wa keki na wanaojishughulisha na bidhaa mbalimbali zinazotumika
kutengeneza keki kama vile unga wa ngano wa Azam,”
alisema Mkurugenzi wa Insights Productions Limited, Bi. Elias.
Akifafanua zaidi Mkurugenzi huyo
alisema onesho hilo litajumuisha bekari na hoteli mbalimbali, Vyuo vya
taaluma ya hotelia toka Tanzania na majirani (Afrika Mashariki) pamoja
na watengenezaji keki binafsi. Wananchi watakaotembelea maonesho hayo
ambayo hayata kuwa na kiingilio watapata fursa ya kujionea aina na
mitindo mbalimbali ya utengenezaji wa keki pamoja na kuonja bidhaa hiyo
kwenye maonesho ambayo yatafanyika Serena Hoteli jijini Dar es Salaam.
Akizungumzia maonesho hayo Mratibu
wa Matangazo na Uhusiano wa Umma wa kampuni ya SSB, Mohammed Ramadhan
alisema Azam ikiwa ni kampuni inayotengeneza unga bora wa kutengenezea
keki imeamua kudhamini ikiwa ni ishara ya kutambua taaluma hiyo ya
uokaji keki nje na ndani ya Tanzania.
*Imeandaliwa na www.thehabari.com
ILIVYOKUWA JANA WAKATI WA UPIGAJI KURA BUNGE MAALUM LA KATIBA WAENDELEA
programu ya kujitolea kwa vijana yahitimishwa
Picha na Benjamin Sawe
Shirika la Nyumba la Taifa lakabidhi mashine za kufyatulia matofali ya kufungamana Kigoma
Meneja wa Mkoa NHC, Nistas
Mvungi akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Kanali Issa Machibya mashine
32 za kufyatulia matofali ya kufungamana.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma Ujiji akishukuru Shirika kwa kuwapatia vijana mashine ya hydraform.
Wafanyakazi wa NHC na kikundi
cha Vijana Kwanza Group na wageni waalikwa wakisubiria Mgeni Rasmi Mkuu
wa Mkoa Mhe Kanali Issa Machibya.
Meneja wa Shirika la Nyumba
Kigoma Ndg Nistas Mvungi akijadiliana na Mkuu wa Mkoa Mhe Issa Machibya
jambo kuhusiana na Mashine ya matofali ya kufungamana kuhusu ufanisi
wake na ajira kwa vijana.
Picha ya pamoja ya wafanyakazi wa Shirika Mkoa wa Kigoma na Mgeni Rasmi Mkuu wa Mkoa Mhe Kanali Issa Machibya.
Meneja wa Shirika la Nyumba
Ndg. Nistas Mvungi akihutubia wananchi wa Kigoma kuhusu mradi wa mashine
za kufyatulia matofali ya kufungamana 32 zilizotolewa na Shirika kwa
vikundi vya vijana wa Mkoa wa Kigoma
Mkuu wa Wilaya Mkuu wa Wilaya
ya Kigoma, Ramadhan Maneno akikabidhi mashine za kufungamana kwa
Kikundi cha Vijana Kwanza Group. Mwenyekiti wa kikundi Ndg Daniel
George na Katibu wake wakipokea mashine.
Picha ya pamoja ya kikundi cha vijana kwanza group na mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa.
Wananchi wakimsikiliza Mkuu wa
Wilaya ya Kigoma Ramadhani Maneno kwa makini kuhusiana na maelekezo
yake kuhusu umuhimu wa kutumia matofali ya kufungamana na kuondokana na
nyumba za matope.
Subscribe to:
Posts (Atom)



