TAN
Bayport
Kikoa
Myway entertainment
FORE PLAN CLINIC
MPINGA CUP 2016
Mashujaa Fm 89.3, Lindi
Saturday, November 15, 2014
WANAFUNZI WA KENYA WATEMBELEA MAHAKAMA YA HAKI ZA BINADAMU YA AFRIKA KUJIFUNZA
Rais Kikwete atoka Hospitalini Baada ya KUPATA NAFUU
Edward Schaeffer kutoka
Hospitali ya Johns Hopkins alipokuwa amelazwa baada ya kufanyiwa
upasuaji wa kuondoa tezi dume mwishoni mwa wiki iliyopita baada ya kupata nafuu.Kulia nia Mke wa Rais Mama Salma Kikwete. Hali ya Rais Kikwete imezidi kuimarika baada ya kutoka wodini na kuwa mapumzikoni akiuguza kidonda kilichotokana na upasuaji aliofanyiwa, kabla ya kwenda kuondolewa nyuzi siku chache zijazo. Huku akiendelea kufanya mazoezi kila siku, Rais Kikwete pia ameendelea kupokea salamu za Watanzania kwa njia ya ujumbe mfupi (SMS) kutoka kila pembe ya dunia pamoja na salamu za kumtakia nafuu mapema kutoka kwa viongozi mbalimbali wakiwemo mabalozi na wawakilishi wa nchi za nje. Naye amekuwa akizijibu kwa kadri anavyoweza.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na Daktari Edward Schaeffer
muda mfupi baada ya kuruhusiwa kutoka katika hospitali ya Johns
Hopkins huko Baltimore, Maryland nchini Marekani ambapo alifanyiwa upasuaji wa kuondoa tezi dume mwishoni mwa wiki iliyopita. Hali ya Rais Kikwete imezidi kuimarika baada ya kutoka wodini na kuwa mapummzikoni akiuguza kidonda kabla ya kwenda kuondolewa nyuzi siku chache zijazo. Huku akiendelea kufanya mazoezi kila siku, Rais Kikwete pia ameendelea kupokea salamu za Watanzania kwa njia ya ujumbe mfupi (SMS) kutoka kila pembe ya dunia pamoja na salamu za kumtakia nafuu mapema kutoka kwa viongozi mbalimbali wakiwemo mabalozi na wawakilishi wa nchi za nje. Naye amekuwa akizijibu kwa kadri anavyoweza (Picha naFreddy Maro)
Hospitali ya Johns Hopkins alipokuwa amelazwa baada ya kufanyiwa
upasuaji wa kuondoa tezi dume mwishoni mwa wiki iliyopita baada ya kupata nafuu.Kulia nia Mke wa Rais Mama Salma Kikwete. Hali ya Rais Kikwete imezidi kuimarika baada ya kutoka wodini na kuwa mapumzikoni akiuguza kidonda kilichotokana na upasuaji aliofanyiwa, kabla ya kwenda kuondolewa nyuzi siku chache zijazo. Huku akiendelea kufanya mazoezi kila siku, Rais Kikwete pia ameendelea kupokea salamu za Watanzania kwa njia ya ujumbe mfupi (SMS) kutoka kila pembe ya dunia pamoja na salamu za kumtakia nafuu mapema kutoka kwa viongozi mbalimbali wakiwemo mabalozi na wawakilishi wa nchi za nje. Naye amekuwa akizijibu kwa kadri anavyoweza.
muda mfupi baada ya kuruhusiwa kutoka katika hospitali ya Johns
Hopkins huko Baltimore, Maryland nchini Marekani ambapo alifanyiwa upasuaji wa kuondoa tezi dume mwishoni mwa wiki iliyopita. Hali ya Rais Kikwete imezidi kuimarika baada ya kutoka wodini na kuwa mapummzikoni akiuguza kidonda kabla ya kwenda kuondolewa nyuzi siku chache zijazo. Huku akiendelea kufanya mazoezi kila siku, Rais Kikwete pia ameendelea kupokea salamu za Watanzania kwa njia ya ujumbe mfupi (SMS) kutoka kila pembe ya dunia pamoja na salamu za kumtakia nafuu mapema kutoka kwa viongozi mbalimbali wakiwemo mabalozi na wawakilishi wa nchi za nje. Naye amekuwa akizijibu kwa kadri anavyoweza (Picha naFreddy Maro)
Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) afanya ziara kwenye vitengo vya Mawasiliano Serikalini
Katibu, Ofisi ya Rais Sekretariet
ya Ajira katika Utumishi wa Umma Bw. Exavier Daudi (kushoto)
akimkaribisha ofisini kwake Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Bw.
Assah Mwambene wakati alipotembelea ofisi hiyo kwa lengo la kuangalia
utendaji kazi wa kitengo cha mawasiliano.
Katibu, Ofisi ya Rais Sekretariet
ya Ajira katika Utumishi wa Umma Bw. Exavier Daudi akimueleza Mkurugenzi
wa Idara ya Habari (MAELEZO) Bw. Assah Mwambene kuhusu mikakati ya
ofisi hiyo ya kuboresha mawasiliano ya serikali kwa umma wakati wa ziara
ya Mkurugenzi wa Idara ya Habari katika vitengo cha mawasiliano.
SEKTA BINAFSI IHUSISHWE KUTOA HUDUMA ZA AFYA – PINDA
……………………………………………………………………………….
WAZIRI MKUU Mizengo Pinda ameitaka Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii ipanue wigo wa utoaji huduma za msingi kwa kuishirikisha zaidi sekta binafsi nchini.
“Ninawasihi Waziri wa Afya na
Naibu wake kwa vile ni wapya bado wabadili mtizamo wa wizara hii kwa
kushirikisha zaidi wadau wa sekta binafsi kwenye utoaji wa huduma ili
wasaidie kupunguza mzigo mkubwa ilionao Serikali,” alisema.
Ametoa kauli hiyo leo mchana
(Ijumaa, Novemba 14, 2014) wakati akifungua Mkutano wa wa Kwanza wa
Kitaifa wa Sekta ya Afya wa mwaka 2014 ulioanza leo kwenye ukumbi wa
mikutano wa kimataifa wa Mwalimu Nyerere, jijini Dar es Salaam.
Waziri Mkuu ambaye amefungua
mkutano huo kwa niaba ya Rais Jakaya Kikwete aliyeko nje ya nchi kwa
matibabu alisema: “Kuna tatizo la kukumbatia utoaji wa huduma … tunazo
hospitali kubwa za wilaya zinazomilikiwa na taasisi za dini. Hivi ni kwa
nini kama Wizara msiwasaidie kuwahudumia watumishi wao au kuwapa ruzuku
kwenye dawa ili kuwawezesha kutoa huduma kwa ufanisi zaidi?,” alihoji
Waziri Mkuu na kushangiliwa na washiriki wa mkutano huo.
“Hata ukiangalia takwimu kwenye
utoaji wa huduma za afya kupitia mifumo ya bima ya afya utabaini kuwa ni
asilimia 18 tu wananchi wanatumia bima ya afya na kati ya hao, asilimia
15.3 ni mifuko ambayo imeanzishwa na Serikali. Ni kwa nini basi
msiwasaidie wadau wa sekta binafsi ili wachangie huduma hii na idadi wa
watumiaji wa mfumo huu iongezeke haraka?,” alihoji.
Akizumgumzia kuhusu uwiano kati
ya daktari na mgonjwa, Waziri Mkuu alisema uwiano uliopo ni mbaya na
kwamba hakuna njia ya haraka ya kupunguza tatizo hilo isipokuwa kwa
kuishirikisha sekta binafsi kwenye ujenzi wa vyuo vikuu vya elimu ya
tiba na sayansi za jamii.
“Uwiano wa sasa hapa nchini ni
daktari mmoja kwa wagonjwa 75,000 wakati viwango vya kimataifa vinataka
daktari mmoja awahudumie wagonjwa 7,000. Kwa wauguzi, hapa nchini
muuguzi mmoja anahudumia wagonjwa 6,000 wakati viwango vya kimataifa
vinataka muuguzi mmoja ahudumie wagonjwa 500,” alisema.
“Kwa uwioano huu safari bado ni
ndefu. Tunapaswa tuangalie tutafanyaje ili watu binafsi waje kuwekeza
kwenye elimu ya juu ya sayansi na tiba, wajenge vyuo vya tiba, wajenge
hospitali kubwa, na sisi pia kwa upande wa Serikali ni lazima tuseme
tunawapa vivutio gani hawa wawekezaji hadi wakubali kuwekeza kwenye eneo
hilo,” alisema.
“Tunataka mkutano huo uje na
mapendekezo ambayo mnataka Serikali iyafanyie kazi na hatimaye isaidie
kuboresha utoaji wa huduma za afya kwa wananchi,” alisema Waziri Mkuu.
Akizungumza na waandishi wa
habari mara baada ya kufungua mkutano huo, Waziri Mkuu alisema Serikali
inaendelea kudhibiti ugonjwa wa ebola kwenye vituo vya mipakani na
kwenye viwanja wa ndege.
“Mpaka sasa hatujapata kesi ya
ugonjwa wa ebola hapa nchini… changamoto kubwa ni ukubwa wa mipaka yetu.
Si wageni wote wanaoingia nchini wanapita kwenye vituo rasmi, wapo
wanaotumia njia za vichochoroni. Rai yangu ni kuwaomba Watanzania wawe
waangalifu kutambua ni wageni gani wanaingia kwenye maeneo wanayoishi,”
alisema.
Mkutano huo wa siku mbili unamalizika kesho (Jumamosi, Novemba 15, 2014).
Waziri Mkuu amerejea mjini Dodoma kuendelea na kikao cha Bunge.
KUBUNI JEZI MPYA YA TIMU ZA TAIFA MWISHO LEO
Shirikisho la Mpira wa Miguu
Tanzania (TFF) limekaribisha wabunifu, kubuni mwonekano wa jezi mpya za
timu ya Taifa kwa mechi za nyumbani na ugenini ambapo mwisho wa kufanya
hivyo ni leo (Novemba 15 mwaka huu). Ubunifu ni lazima uzingatie rangi
za bendera ya Taifa.
Mshindi wa jezi ya nyumbani
atapata sh. 1,000,000 (milioni moja), na mshindi wa jezi ya ugenini
atapata pia sh. 1,000,000 (milioni moja).
Ubunifu utumwe kwenye anwani ya barua pepe: info@tff.or.tz
au uwasilishwe kwa CD au flash zikiwa katika mfumo wa PDF katika ofisi
za TFF zilizopo ghorofa ya tatu katika Jengo la PPF Tower, Mtaa wa Ohio
na Garden Avenue.
Kwa maelezo zaidi unaweza kuwasiliana nasi kwa simu namba; 0713 210242 au 0714 634838.
MISS TANZANIA 2013 AAHIDI MAKUBWA MASHINDANO YA UREMBO YA DUNIA
…………………………………………………………………………………………
Na Benedict Liwenga, Maelezo-DSM.
MREMBO wa Tanzania wa mwaka
2013, Happiness Watimanywa ameahidi kuing’arisha Tanzania katika
mashindano ya ulimbwende ya Dunia yatakayofanyika mapema mwezi ujao huko
nchini Uingereza.
Akiongea na waandishi wa habari
jijini Dar es Salaam, mlimbwende huyo amewaeleza waadishi kuwa,
kutokana na uzoefu wa kazi zake alizokuwa akifanya kwa jamii kwa muda
kipindi cha mwaka mmoja ikiwemo misaada ya hali na mali anayoipata toka
Bodi ya Utalii Tanzania pamoja na wahisani wengine nchini amewaahidi
Watanzania kuibuka na ushindi katika kinyang’anyiro hicho huko nchini
Uingereza ili kuitangaza Tanzania.
Alieleza kuwa, tayari Ubalozi wa
Tanzania nchini Uingereza utakuwa tayari kumpokea pindi atakapowasili
nchini humo kwa lengo la kuiwakilisha Tanzania katika mashindano hayo ya
ulimbwende yatakayowahusisha walimbwende toka Ulimwengu mzima.
“Nimejifunza mambo mengi hasa
kipindi wakati nasafiri sehemu mbalimbali nchini pamoja na kufanya kazi
za kusaidia jamii katika kipindi chote, hivyo nawaahidi watanzania
ushindi katika mashindano hayo yatakayofanyika huko Uingereza pia
mnipigie kura zenu za wingi”, alisema Watimanywa.
Naye Mkurugenzi wa Lino
International Agency Limited, Bw. Hashim Lundenga ambao ni waandaaji wa
Miss Tanzania, alisema kuwa mashindano ya Urembo wa Dunia ni mashindano
ya Kimataifa ambayo yanawakutanisha walimbwende toka nchi nyingi duniani
ikiwemo Tanzania, hivyo alitoa wito kwa watanzania wote kuunga mkono
kwa kumpigia kura nyingi mwakilishi ambaye ndiye mrembo wa Tanzania kwa
mwaka 2013, Hapinness Watimanywa ili ajinyakulie taji hilo la dunia ili
aweze kuipa sifa Tanzania kimataifa.
Mashindano ya Urembo ya Dunia
yanatarajiwa kufanyika mapema tarehe 14 Desemba, 2014 huko nchini
Uingereza ambapo mrembo huyo wa Tanzania anatarajia kuanza safari yake
ya kuelekea nchini humo tarehe 15 Novemba, 2014 tayari kwa ajili ya
mashindano hayo.
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Kwa mujibu wa taarifa rasmi
iliyotolewa jana na Ofisi ya Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza
Nchini msaada huo umetolewa na Kampuni ya Twiga Cement ya Jijini Dar es
Salaam kufuatia kusainiwa kwa Makubaliano ya kuiuzia Kampuni hiyo madini
ya chokaa katika eneo la Gereza Wazo.
Mgeni rasmi katika tukio hilo
atakuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mathias M. Chikawe(Mb).
Aidha, Wadau mbalimbali toka nje ya Jeshi la Magereza watakuwepo katika
hafla hiyo.
Kuanza kwa mradi wa ujenzi wa
nyumba hizo utapunguza tatizo la muda mrefu la uhaba wa Nyumba zenye
hadhi kwa ajili ya makazi ya Maafisa na askari wa Gereza hilo.
Vyombo vya Habari vinakaribishwa kwenye shughuli hiyo katika muda ulioelezwa.
Imetolewa na;
Lucas A. Mboje, Mkaguzi wa Magereza;
Afisa Habari wa Jeshi la Magereza;
Makao Makuu ya Jeshi la Magereza;
DAR ES SALAAM.
14 Novemba, 2014.
KINANA KUANZA ZIARA YA MIKOA YA MTWARA NA LINDI
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM Taifa Nape Nnauye
akizungumza na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa Sekretarieti,CCM
Ofisi ndogo Lumumba.
……………………………………………………………………………..
Ziara hiyo itakuwa ya siku 16 na itaanza Novemba 15,2015 ,Katibu Mkuu ataambatana na Katibu wa Halmashauri Kuu anayeshughulikia Itikadi na Uenezi Ndugu Nape Nnauye.
Ziara hiyo ya Katibu Mkuu itamwezesha kutembelea na kufanya mikutano ya ndani na ya hadhara katika majimbo yote ya mikoa ya Lindi na Mtwara ikiwa pamoja na kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010 – 2015, kukutana na wananchi, kuwasikiliza na kwa kushirikiana nao kutafuta majibu ya changamoto zinazowakabili.
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana anatarajia kufanya ziara katika mikoa ya Lindi na Mtwara.
Akiongea
na waandishi wa habari katika ukumbi wa Sekretarieti,Lumumba jijini Dar
es salaam Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM Taifa Nape Nnauye alisema
kuwa Ziara hiyo ni mwendelezo wa ziara za Sekretarieti ya Halmashauri
Kuu Taifa katika mikoa mbali mbali nchini kwa ajili ya kujenga na
kuhimiza uhai wa chama na kukagua utekelezazaji wa Ilani ya uchaguzi ya
CCM ya mwaka 2010 – 2015.Ziara hiyo itakuwa ya siku 16 na itaanza Novemba 15,2015 ,Katibu Mkuu ataambatana na Katibu wa Halmashauri Kuu anayeshughulikia Itikadi na Uenezi Ndugu Nape Nnauye.
Ziara hiyo ya Katibu Mkuu itamwezesha kutembelea na kufanya mikutano ya ndani na ya hadhara katika majimbo yote ya mikoa ya Lindi na Mtwara ikiwa pamoja na kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010 – 2015, kukutana na wananchi, kuwasikiliza na kwa kushirikiana nao kutafuta majibu ya changamoto zinazowakabili.
SERIKALI YA TANZANIA NA MAREKANI ZATILIANA SAINI MKATABA YA KUANDAA MIRADI YA SEKTA YA NISHATI
Na:Beatrice Lyimo- Maelezo-DSM.
Serikali ya Marekani na Tanzania
zimetiliana saini kwa ajili ya kuandaa miradi katika sekta ya nishati
itakayofadhiliwa katika awamu ya pili ya Mkataba wa Millennium Challenge
Corporation (MCC).
Utiaji saini wa mkataba huo
ulifanyika katika Wizara ya Fedha jijini Dar es Salaam ambapo Makamu wa
Rais wa MCC Bw. Kamran Khan anayeshughulikia Mikataba na Uendeshaji
wake pamoja na Waziri wa Fedha wa Tanzania , Mhe. Saada Mkuya
ukishuhudiwa na Balozi wa Marekani nchini Mark Childress.
Akiongea wakati wa hafla ya
utiaji saini wa mkataba huo, Waziri wa Fedha, Mhe. Saada Mkuya alisema
kuwa MCC imeipatia Serikali ya Tanzania shilingi bilioni 17 kwa ajili ya
utekelezaji wa mradi wa MCC II ambapo mraadi huo unatarajiwa kuanza
kutekelezwa hapo mwakani ukiwa na lengo la kusaidia miundombinu ya umeme
nchini.
Makubaliano hayo ni muendelezo
wa ubia imara kati ya Marekani na Tanzania kati ya mwaka 2008 na 2013
ambapo MCC ilitekeleza mkataba wa miradi mikubwa ya uwekezaji katika
sekta za maji, barabara, na nishati ya umeme nchini.
Miradi hiyo iligharimu jumla ya
Dola za kimarekani milioni 698, chini ya mkataba huo mtandao wa nyaya za
umeme wenye zaidi ya kilometa 3,000 ulijengwa.
Kwa kuzingatia mafanikio hayo
katika utekelezaji wa wa programu zilizokuwa chini ya mkataba wa kwanza
kuwahi kutolewa na MCC, taasisi hiyo iliichagua tena Tanzania kuingia
katika mkataba wa pili utakaolenga sekta ya Nishati katika miundombinu
pamoja na mageuzi ya kisera na mifumo ya udhibiti na kitaasisi.
Aidha, upembuzi yakinifu
utaiwezesha Tanzania kuandaa miradi itakayoleta mageuzi katika sekta ya
Nishati ikiwa ni pamoja na kuboresha utendaji wa shirika la ugavi wa
umeme Tanzania (TANESCO) na Shirika la Umeme Zanzibar (ZECO) katika
maeneo ya kiufundi, usimamizi wa fedha na uendeshaji na kuongeza kiwango
cha upatikanaji wa huduma ya umeme katika maeneo ya vijijini.
Shirika la Changamoto za Milenia
(MCC) ni Taasisi ya Serikali ya Marekani inayotoa misaada kwa nchi
zinazoendelea, shughuli zake zinajengwa katika misingi kwamba msaada
utaleta ufanisi na matokeo makubwa pale unapoimarisha utawala bora,
uhuru wa kiuchumi na uwekezaji katika watu ambao unakuza uchumi na
kuondoa umaskini.
HABARI ZILIZOTAWALA SIKU YA TAREHE 14/11/2014 HIZI HAPA JIKUMBUSHE
BONDIA THOMAS MASHALI ASAINI KUZIPIGA NA ABDALLAH PAZI JANUAR MOSI 2015 FRENDS CORNER
on November 14, 2014
Bondia Abbdallah Pazi kulia
akitia saini ya kupigana na Thomasi Mashali kushoto baada ya makubaliano
na promota Kassim Texas katikati mpambano utakaofanyika january mosi
katika ukumbi wa frends corner manzese Dar es salaam
Bondia Thomasi Mashali kushoto
akitunishiana misuli na Abdallah Pazi baada ya makubaliano juzi ya
mpambano wao kufanyika January Mosi 2015 katika ukumbi wa Frends Corner
Manzese Dar es salaa
Promota Kassim Texas katikati
akiwainuwa mikono juu mabondia Thomas Mashali kushoto na Abdallah Pazi
kuashilia makubaliano ya mpambano wao utakaofanyika january mosi katika
ukumbi wa frends corner manzese Bondia Thomasi Mashali kushoto akitunishiana misuli na Abdallah Pazi baada ya makubaliano juzi ya mpambano wao kufanyika January Mosi 2015 katika ukumbi wa Frends Corner Manzese Dar es salaa Picha na SUPER D BLOG
===============================================================
WAZIRI WA AFYA NA USTAWI WA JAMII AFUNGUA KONGAMANO LA NHIF NA WAANDISHI WA HABARI MJINI DODOMA
on November 14, 2014
=====================================================================
SKYLIGHT BAND NI MOTO WA KUOTEA MBALI, WAZIDI KUWAPA RAHA MASHABIKI WAO KWA BURUDANI NZURI
on November 14, 2014
Pichani Kutoka kushoto ni Bella Kombo akiongoza mashambulizi ya jukwaa
akipewa sapoti na Digna Mbepera(katikati) na kwa mbaliiiii ni Aneth
kushaba.
Kama kawaida yetu inapofika
mwishoni mwa juma yaani Ijumaa huwa inakuwa ni siku ya furaha na
kubadilishana mawazo, kupunguza stress za kazini…..paleee Thai Village
Masaki.Kwenye Jukwaa Bendi yako matata na inayotikisa Tanzania na Jiji
la Dar Skylight Band wanakuwa wanakupa burudani ya nguvu na iliyoenda
shule.Karibu leo kuanzia saa 3 kamili usiku upate zile Afropop, Zouk,
Lingala,Sebene, Reggae, Naija Flava na zingine kibao!
Aneth Kushaba AK 47 akizipiga vocal za kutoshaaaa ili kuwapa burudani wapenzi wa Skylight Band ndani ya Thai Village Ijumaa iliyopita.
Bella Kombo akitia madaha yake na swagga kibao ndani ya Thai Village.
Digna Mbepera (Mtoto Mzuri) akiimba kwa hisia kali kuwapa ladha wapenzi wa Skylight band ndani ya Thai Village
Anaitwa Hashimu Donode mkali wao akizipiga zile vocal kaliiii na tamuuu kuwapa raha mashabiki wake ndani ya Thai Village
Aneth Kushaba AK 47 akizipiga vocal za kutoshaaaa ili kuwapa burudani wapenzi wa Skylight Band ndani ya Thai Village Ijumaa iliyopita.
Bella Kombo akitia madaha yake na swagga kibao ndani ya Thai Village.
Digna Mbepera (Mtoto Mzuri) akiimba kwa hisia kali kuwapa ladha wapenzi wa Skylight band ndani ya Thai Village
Anaitwa Hashimu Donode mkali wao akizipiga zile vocal kaliiii na tamuuu kuwapa raha mashabiki wake ndani ya Thai Village
UNESCO, SAMSUNG KUJENGA KIJIJI CHA DIGITALI OLOLOSOKWAN
on November 14, 2014
Pichani ni muonekano wa mchoro wa kijiji hicho utakavyokua.
Nyalandu amteua RC Singida Mwenyekiti wa Kikos kzi alichouunda jana.
on November 14, 2014
Waziri
wa Maliasili na utalii Lazaro Nyalandu amemteua Mkuu wa Mkoa wa Singida
Dkt Paseko Kone kuwa Mwenyekiti wa Kikosi kazi kitachofuatilia uundwaji
wa chama cha wafuga nyuki hapa nchini.
Nyalandu alimteua Mkuu wa Mkoa
huo kwa kuwa amekuwa mstari wa mbele katika kuwasaidia wafugaji wa nyuki
katika mkoa wake wa Singida bila kuchoka.
Waziri Nyalandu alitoa uamuzi huo wakati akifuga kongamano la ufugaji nyuki la Afrika lililomalizika Jijini Arusha jana.
Wajumbe Wengine walioteuliwa
katika kikosi kazi hicho ni Juma Shaban Mgoo ambaye atakuwa katibu wa
Kikosi kazi hicho na pia ni Mtendaji Mkuu,wakala wa Huduma za Misitu
Tanzania na ambaye alikuwa mkamu mwenyekiti wa Kongamano atakuwa mjumbe
katika Kikosi kazi hicho,wengine ni Ester Mkwizu Mjumbe.
Wajumbe wengine ni mwakilishi wa
wafugaji nyuki ,mwakilishi wa wasomi na watafiti ili kikosi kazi kiwe
na mchanganyiko wa pande zote.
Walioteuliwa wote watapaa barua
jumatatu kwa ajili ya kuthibitisha uteuzi wao,ambapo waziri nyalandu
alieleza kuwa kuwa uteuzi huo wa wajumbe wanaounda kikosi kazi cha
kushughulikia uundwaji wa chama cha wafuga nyuki ni agizo lililotolewa
na Waziri Mkuu wakati wa ufuguzi wa Kongamano la nyuki kuwa ipo haja ya
kuundwa kwa chama cha wafugaji nyuki ili kiweze kuwaunganisha wafugaji
wote ndani ya nchi na kuwa na mtandao mmoja wenye nguvu na sauti.
Katika hotuba yake alieleza
jinsi Tanzania ilivyojithatitia kuhakikisha inainua ufugaji nyuki na
sekta ya nyuki ili kuwapita nchi ya Ethiopia ambayo ndiyo kinara cha
nyuki cha Ufugaji nyuki Afrika.
Akasema kongamano hili ni la
kwanza kufanyika katika ardhi ya Tanzania na limesaidia sana
katikakuwafumbua macho watanzania hasa wafugaji nyuki hasa katika
masuala muhimu yaliyosisitizwa katika mada zilizojadiliwa kwenye
kongamano hilo yatasaidia kukuza sekta ya ufungaji nyuki hapa nchini.
Kongamano hilo lililojumuisha
washiriki wapatao 550 kutoka katika mataifa ya Ghana,Ethiopia,Zimbabwe,
Afrika kusini,Camerun,Sudani,Kenya,Uganda na Rwanda.
Washiriki wengine walitoka
katika nchi ya Kanada,Marekani,Pakstan,Namibia,Misri,
Zambia,Ubelgiji,Uturuki na mengine.limekuwa la kufana sana,mada 88
zilikuwepo,mada 45 zilijadiliwa,katiyake mada 26 zilihusu tafiti za
nyuki,mada 17 zilijadiliwa kwa wafugaji nyuki.
Awali akimkaribisha waziri
Nyalandu Mwenyekiti wa Kongamano hilo SelestinKisimba alieleza kuwa
katika kongamano hilo wameondoka na mapendekezo sita mambyo wataenda
kuyafanyia kazi mara moja ili kuinua sekta ya nyuki.
Baadhi ya Mapendekzo hayo ni
kuwa ufugaji nyuki lazima uweb endevu kwa manufa ya wafugaji
wote,,umuhimu wa ufugaji nyuki na maendeleo,tatizo la ukosefu wa
mitaji,uendelezaji wa rasilimali zilizopo , kuongeza uzalishaji wa
thamani ya asali,ambapo mapendekezo hayo yatasaidia kuboresha ufugaji
nyuki.
Washiriki wamepata nafasi ya
kutembelea maeneo ya ufugaji nyuki katika mikoa ya Singida,Dodoma na
Ngorogoro Mkoani Arusha kuweza kujifunza na kuona hali halisi ya
mazingira yalivyo hasa katika maeneo yanayofugwa nyuki.
Subscribe to:
Posts (Atom)
