TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Monday, January 19, 2015

TBL YAFADHILI UCHIMBAJI VISIMA BAGAMOYO

 Mhandisi wa Kampuni ya Al Water Well Drillers, Mohamed Aboud (katikati), akielekeza jambo kwa mmoja ya wafanyakazi wakati wa ukaguzi wa maendeleo ya ujenzi ya miradi ya uchimbaji wa visima vya maji unaofafadhiliwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), katika vijiji vya Nianjema C na Mianzini B, wilayani Bagamoyo, Pwani mwishoni mwa wiki. Kulia ni Ofisa Uhusiano wa TBL, Dorris Malulu.
 Ofisa Uhusiano wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Dorris Malulu (kulia) akielekeza jambo kwa fundi alipokuwa akikagua ujenzi wa mradi wa uchimbaj wa visima vya maji katika vijiji vya Nianjema C na Mianzini B, wilayani Bagamoyo, Pwani mwishoni mwa wiki.Miradi hiyo itagharimu sh. mil.51.7.
 Ofisa Uhusiano wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Dorris Malulu, akijadiliana jambo na  na mkandarasi wa  ujenzi wa visima vya maji katika vijiji vya Nianjema C na Mianzini B,Mohamed Aboud, mwishoni mwa wiki wilayani Bagamoyo, Pwani. TBL inafadhili miradi hiyo kwa gharama ya sh. mil. 51.7.
Mhandisi wa Kampuni ya Al Water Well Drillers, Mohamed Aboud (katikati), akielekeza jambo kwa mmoja ya wafanyakazi wakati wa ukaguzi wa maendeleo ya ujenzi ya miradi ya uchimbaji wa visima.

UFAHAMU MTANDAO WA MALEZI MAKUZI NA MAENDELEO YA WATOTO WADOGO TANZANIA (TECDEN)

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Ndugu Bruno Ghumpi
unnamed
……………………………………………………………………………………………..
Mtandao wa Malezi Makuzi na Maendeleo ya Watoto Wadogo Tanzania – TECDEN ni chombo kinachoundwa na mashirikia mbalimbali yanayofanya kazi za kuhudumia watoto wadogo Tanzania. Mtandao huu ulianzishwa mwaka 2000 na kusajiliwa rasmi mwaka 2004. Makao makuu ya Mtandao huu yapo Jijini Dar es salaam. Hadi kufikia mwaka 2014 Mtandao huu una jumla ya mashirika wanachama wasioungua 200 katika mikoa 14 ya Tanzania bara na Visiwani yanayotoa huduma kwa watoto wadogo Tanzania Lengo kuu la Mtandao ni kuboresha huduma za watoto wadogo Tanzania ili waweze kukua na kufikia utimilifu wao Shughuli Kuu za Mtandao ni pamoja na:- • Kufanya ushawishi na utetezi wa masuala yanayohusu uboreshaji wa huduma na kulinda haki za watoto wadogo ikiwa ni pamoja na kushawishi maboresho ya sera na kufuatilia utekelezaji wa sheria na miongozo mbalimbali inayohusu uboreshaji wa huduma kwa watoto wadogo Tanzania. • Kuhamasisha jamii na watoa huduma kutambua umuhimu wa kuimarisha na kuwezesha watoto wadogo kupata mahitaji na haki zao za msingi. • Kuimarisha mifumo ya upashanaji habari na kuelimishana katika ngazi zote za huduma kwa watoto wadogo. • Kutafiti na kutumia matokeo ya utafiti katika kushauri uboreshaji wa huduma kwa watoto wadogo Tanzania.
Dhana ya Malezi Makuzi na Mendeleo ya Awali ya Mtoto (MMMAM) Malezi, makuzi na maendeleo ya awali ya mtoto ni istilahi ya jumla ya programu na vitendo vinavyoandaliwa kuwasaidia watoto (kuanzia mimba, kuzaliwa hadi miaka 8) ili kukua vizuri kimwili, kiakili, kijamii, kihisia, kimaadili na kiroho. Watoto wanahitaji kuchangamshwa katika nyaja na hatua zote za ukuaji, kiakili kwa michezo, kujifunza kuzungumza, kukaa, kutambaa, kutembea na kupatiwa fursa ya kuanza kujifunza mambo mbalimbali pamoja na utamaduni wao.
Utoaji wa huduma jumui za MMMAM. Huduma hizi hujumuishwa ili kuwawezesha watoto wengi kupata huduma jumuishi za MMMAM zitolewazo na sekta mbali mbali katika mkabala jumui. Huduma hizi zinapaswa kupatikana kuanzia ngazi ya familia ,vituo vya afya ya msingi,vituo vya kulelea watoto mchana, vituo vya Malezi Makuzi ya awali ya mtoto vinavyomilikiwa na Jamii, madarasa ya awali na madarasa ya msingi hususani darasa la kwanza na la pili.
Katika kutekeleza shughuli zake Mtandao wa TECDEN umekuwa ukishirikiana na mashirika mbalimbali ya wabia wa maendeleo ikiwemo shirika la Children in Crossfire kutoka nchini Ireland na shirika la Better Way Foundation kutoka nchini Marekani
Ili kujua habari zaidi za TECDEN na masuala ya utoaji huduma kwa watoto wadogo na faida zake, unaweza kutembelea ofisi ya Mtandao makao makuu iliyopo Jengo la Posta mkabala na Wizara ya Mambo ya Ndani Nchi na Makao Makao Makuu ya Polisi jijini Dar es Salaam.
Unaweza pia kuwasiliana kwa njia ya simu au barua pepe na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Ndugu Bruno Ghumpi kwa namba 0754 690 556 na barua pepe ecdnetwork@gmail.com na ghumpibr@yahoo.com

KATIBU MKUU WA CCM NDUGU ABDULRAHMAN KINANA AMALIZA ZIARA YAKE MKOA WA MAGHARIBI

1Katibu Mkuu wa CCM  Ndugu Abdulrahman Kinana akiangalia mti wa viungo aina ya Mdalasini wakati akipata maelezo kutoka kwa Othman Mohamed  mwenyekiti wa kikundi Kinachoendesha shamba la Spice Solution Farm lililopo Mwakaje  jimbo la Mfenesini Zanzibar  wakati aliposhiriki pia shughuli za upandaji wa miti katika shamba hilo, Katika ziara hiyo ambayo ni ya kukagua na kuhimiza utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi ya mwaka 2010 Kinana Anaongozana na Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM. 2Katibu Mkuu wa CCM  Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kazi ya kupanda miti katika shamba la Spice Solution Farm Mwakaje Mfenesini. 3Katibu Mkuu wa CCM  Ndugu Abdulrahman Kinana akiangalia pilipili zilizolimwa katika shamba hilo huku akipata maelezo.  6Katibu Mkuu wa CCM  Ndugu Abdulrahman Kinana akiangalia viongo mbalimbali vilivyosagwa na kusindikwa tayari kwa kuuza kwa wateja. 7Katibu Mkuu wa CCM  Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kazi ya kufukia mabomba katika mradi wa maji wa Mbuzini jimbo la Mfenesini huku akishirikiana na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mjini Magharibi Ndugu Yusuf Mohamed Yusuf. 8Katibu Mkuu wa CCM  Ndugu Abdulrahman Kinana akimtwisha ndoo ya maji Mama Khadija Issa Kibwana mara baada ya kuzindua mradi wa maji Mbuzini jimbo la Mfenesini.5Katibu Mkuu wa CCM  Ndugu Abdulrahman Kinana akiangalia bidhaa mbalimbali zinazotengenezwa na kikundi cha akina mama wajasiriamali cha Mshikamano Daima Kilichopo Mtopepo jimbo la Mtoni mjini Zanzibar. 10Katibu Mkuu wa CCM  Ndugu Abdulrahman Kinana kushoto na Waziri Kiongozi Mstaafu Mh. Shamsi Vuai Nahodha  wakishiriki katika ujenzi wa ofisi ya CCM tawi la Bububu. 11Waziri Kiongozi Mstaafu Mh. Shamsi Vuai Nahodha  kushoto akiteta jambo na Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM wakati wa mkutano wa ndani uliofanyika kwenye ofisi ya CCM tawi la Bububu. 12Katibu Mkuu wa CCM  Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wajumbe wa Halimashauri kuu ya  wilaya ya Mfenesini. 13 Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Magharibi Ndugu Yusuf Mohamed Yusuf akizungumza katika mkutano huo wa ndani. 14Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Ndugu Vuai Ali Vuai akiteta jambo na Mbunge wa jimbo la Kikwajuni Mh. Masauni Yusuf Masauni. 15Baadhi ya wajumbe wakiwa katika mkutano wa ndani 17Balozi Ali Karume akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya Geji jimbo la Mtoni mjini Zanzibar. 19Baadhi ya wananchi na wana CCM wakiwa katika mkutano huo. 20Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM akiwahutubia wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya Geji Mtoni mjini Zanzibar. 21Naibu Katibu Mkuu Zanzibar Vuai Ali Vuai akizungumza na wananchi katika mkutano huo amewataka wazanzibari kupiga kura ya ndiyo ifikapo aprili 30 mwaka huu ili kuipitisha katiba mpya iliyopendekezwa. 22Baadhi ya wanaCCM wakinyoosha mikono yao juu kukubali kupiga kura ya ndiyo katiba mpya iliyopendekezwa ifikapo Aprili 30 mwaka huu. 23Katibu Mkuu wa CCM  Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wananchi katika mkutano huo.

MKUTANO MKUU WA SABA WA CHAMA CHA MAJAJI WANAWAKE TANZANIA (TAWJA), WAFANYIKA JIJINI DAR ES SALAAM

 Jaji Fredrick Wambali akitoa mada katika mkutano huo.
 Wanachama wa Chama cha Majaji Wanawake Tanzania (TAWJA), wakiwa kwenye mkutano wao mkuu uliofanyika Dar es Salaam jana. Mkutano huo ulihudhuriwa na wanachama kutoka mikoa yote.
Wanachama wa Chama cha Majaji Wanawake Tanzania (TAWJA), wakiwa kwenye mkutano wao mkuu uliofanyika Dar es Salaam jana. Mkutano huo ulihudhuriwa na wanachama kutoka mikoa yote.
……………………………………………………………………………………………
Dotto Mwaibale
 
JAJI Mkuu Mohamed Chande, amewataka wanawake nchini kutoa taarifa katika ngazi husika pindi  wanapoombwa rushwa ya ngono ili sheria ifuate mkondo wake.
 
Akizungumza wakati wa Ufunguzi wa Mkutano wa saba wa Chama cha Majaji Wanawake Tanzania (TAWJA), alisema kunaidadi kubwa ya wanawake ndani ya jamii wanaoombwa rushwa ya ngono lakini wamekuwa wahoga kutoa taarifa.
 
“Katika rushwa ya ngono lazima sheria mahususi zichukuliwe,hivyo tunawasihi wanawake baada ya kufanyiwa matukio hayo wafikishe malalamiko mahakamani au sehemu husika na sheria itafuatwa,” alisema Jaji Chande.
 
Kadhalika, serikali itaendelea kuboresha mazingira ya majaji wanawake ili kukabiliana na mabadiliko yanayoendelea ndani ya mahakama katika ngazi zote.
 
Mwenyekiti wa TAWJA, Engera Kileo, alifafanua katika kesi za rushwa ya ngono mahakama kupitia kifungu cha 25,muhusika atakayebainika kujihusisha na kitendo hicho atatozwa faini au adhabu ya kifungo cha miaka 30.
 
“Mahakama imeweka adhabu hiyo kutokana na ongezeko la matukio  kufanyika ndani ya jamii na wanawake kujengewa woga wa kutoa taarifa kwa wakati, hivyo tunachokifanya kuangalia namna ya kuongeza adhabu kwasababu ngono imetawala katika sekta mbalimbali,” alisema Kileo.
 
Lakini kwa sasa  chama hicho kinatoa elimu juu ya rushwa ya ngono katika jamii na matumizi mabaya ya ngono zembe ili kuwalinda na magonjwa ya kuambukizwa kama Maambukizi ya Ukimwi(VVu), na yale ya zinaa. (Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com)

Vijana jiwekeeni malengo kabla ya kukimbilia mikopo: Kongoye

unnamedMkuu wa Wilaya ya Mpwapwa Bw. Christopher Ryoba Kangoye akizungumza na ujumbe kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo walipomtembelea ofisini kwake kabla ya kukutana na vijana wa Wilaya ya Kongwa na Mpwapwa kwa ajili ya kutoa elimu kuhusu Mfuko wa Maendeleo ya Vijana, Ujasiriamali, Stadi za maisha na ujuzi jana katika Wilaya ya Mpwapwa Mkoa Dodoma.
unnamedKijana Ramadhani Khalid kutoka Kikundi cha Umoja wa Vijana Ng’ambo (UVING’A) kilichopo Wilaya ya Mpwapwa kinachojishughulisha na ufyatuaji wa matofali akishindilia mchanga katika mashine ya kufyatulia matofali kuwaonyesha maafisa waliotembelea mradi wa kikundi hicho jinsi mashine hiyo inavyofanya kazi. Kulia ni Mkuu wa Kituo cha Vijana Sasanda Mbeya Bw. Laurean Masele na wapili kutoka kulia ni Afisa Vijana kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Amina Sanga.
unnamed2 Mkuu wa Kituo cha Vijana Sasanda Mbeya Bw. Laurean Masele akitoa mada ya Uongozi kwa vijana wa Wilaya ya Kongwa na Mpwapwa wakati wa Semina ya Ujasiriamali, Stadi za masiha, Ujuzi na Mfuko wa Maendeleo ya Vijana iliyofanyika jana katika Wilaya ya Mpwapwa Mkoa wa Dodoma. unnamed3Vijana kutoka Wilaya ya Mpwapwa na Kongwa wakifuatilia mada zilizokua zikitolewa wakati wa Semina ya Ujasiriamali, Stadi za masiha, Ujuzi na Mfuko wa Maendeleo ya Vijana iliyofanyika jana katika Wilaya ya Mpwapwa Mkoa wa Dodoma.
unnamed4Afisa Maendeleo ya Vijana kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Amina Sanga akiangalia Cheti cha usajili wa Kikundi cha Wapakaya kinafanya kazi ya kutengeneza Pikipiki kilichopo Wilaya ya Mpwapwa walipowatembelea wanakikundi kwa ajili ya kukagua mradi wa wanakikundi hao. Kushoto ni Afisa Maendeleo ya Vijana Wilaya ya Mpwapwa Bw. Paschal Jeremiah. unnamed5Afisa Maendeleo ya Vijana kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Amina Sanga akishika jiko banifu linalotengenezwa kwa kutumia udongo mfinyanzi kuangalia ubora wa jiko hilo lililotengenezwa na wanakikundi cha Kujiamini kilichopo Wilaya ya Kongwa wakati wa kukagua miradi ya Vijana wa Wilaya ya Kongwa Mkoa wa Dodoma. (Picha zote na: Genofeva Matemu – Maelezo) …………………………………………………………………………
Na: Genofeva Matemu – Maelezo
Vijana kutoka Wilaya ya Mpwapwa na Kongwa Mkoa wa Dodoma wameshauriwa kutokimbilia mikopo inayotolewa kwa vijana kabla ya kujipanga na kuwa na malengo ya matumizi ya mikopo hiyo kwa maendeleo ya Taifa. Rai hiyo imetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa Bw. Christopher Ryoba Kangoye wakati wa ziara ya maafisa kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo walipomtembelea ofisini kwake na baadae kukutana na vijana wa wilaya hizo jana Wilaya ya Mpwapwa Mkoa wa Dodoma. “Vijana wamekua na tabia ya kukimbilia mikopo inayotolewa na taasisi mbalimbali za serikali na zisizo za serikali kabla ya kujipanga hivyo kushindwa kutumia fedha hizo kwa uangalifu na hatimaye kushindwa kurudisha mikopo hiyo kwa wakati”, alisema Bw. Kangoye. Aidha Bw. Kangoye amesema kuwa vijana ni nguvu kazi ya taifa hivyo wanapaswa kujitambua na kutumia nguvu hizo zitakazozalisha matunda mazuri kwani ili mtu aweze kuendelea lazima afanye kazi kwa bidii na kwa ufanisi. Akizungumza kwa niaba ya maafisa kutoka Wizarani waliofika ofisini kwa Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa Mwezeshaji kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi Ester Riwa amesema kuwa Wizara inayosimamia masuala ya Vijana imepanga mikakati mingi ya kuwainua vijana wa taifa hili hivyo kuiomba Wilaya ya Mpwapwa kushirikiana na Wizara inayosimamia vijana kuwaongoza vijana wa Wilaya yao kuwa lulu ya taifa itakayomulika vijana wengine kutoka Wilaya zote nchini Tanzania. Kwa upande wake Afisa Maendeleo ya Vijana kutoka Wilaya ya Mpwapwa Bw. Paschal Jeremiah amesema kuwa vikundi vya vijana kutoka Wilaya ya Mpwapwa vilipatiwa mkopo wa shilingi milioni 10 mnamo mwaka 2009 na urejeshaji wa mkopo huo umefanyika kwa asilimia 90 hali inayoonyesha kuwa vijana wa Wilaya yake wako makini na wanastahili kupatiwa mkopo mwingine kuendeleza shughuli walizozianzisha. Naye kijana Briton Ivan Majele kutoka kikundi cha Umoja wa Vijana Ng’ambo kilichopo Wilaya ya Mpwapwa kinachofanya kazi ya kufyatua matofali amewataka vijana wenzake nchini kutobweteka bali wathubutu na kuamini kuwa mtaji mdogo unaposimamiwa vizuri huzaa na kuwa mkubwa hivyo kuthamini kile kidogo walichonacho na kukiendeleza.

Wampinga Kabila kuwania urais nchini DRC

maandamano Drc Congo
Polisi nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo wamewafyatulia risasi waandamanaji kwenye mji mkuu Kinshasa walio na hasira katika kile kinachoonekana kama jitihada za kutaka kuongoza uongozi wa rais Joseph Kabila.
Watu kadha walitolewa eneo la kati kati mwa mji wakiwa na majeraha ya risasi ambapo pia kulitoka makabiliano kwenye chuo kikuu cha mji huo.
Milio ya risasi iliripotiwa katika maandamano mengine katika mji ulio mashariki wa Goma.
Watu kadhaa walipatikana na majeruhi ya risasi katikati mwa mji huo huku ghasia zengine zikiripotiwa katika katika chuo kimoja kikuu.
rais wa Drc Congo Joseph Kabila
 Viongozi wa upinzani waliitisha maandamano hayo baada ya bunge dogo kuidhinisha sheria siku ya jumamosi inayoagiza kufanyika kwa hesabu ya idadi ya watu kabla ya uchaguzi wa urais utakaofanyika mwaka ujao.
Wabunge hao wa upinzani wamesema kuwa mpango huo utachelewesha uchaguzi huo ambao umekuwa ukingojwa kwa hamu kwa miaka kadhaa.
Rais Joseph Kabila ambaye amekuwa mamlakani kwa miaka 15 amehudumu miula miwili na hawezi kuwania tena urais kulingana na katiba.
Bunge kuu linatarajiwa kuungazia mswada huo wa uchaguzi hii leo.

WANAFUNZI NCHINI WAPINGA KUCHUKULIWA ARDHI YAO

 Wanafunzi wakitawanywa kwa Bomu lililorushwa na Polisi wakati wa Harakati hizo
 Tukio hilo n i baada ya wanafunzi kirejea baada ya Mgomo wa wiki mbili na walimu walimu wa shule za Umma
 wanafunzi wakigonga uzio huo uluikuwa umewekwa na mtu asiyejulikana
 Askari mmoja akiwa anaonekana kujeruhiwa wakati wa pulkushani hizo.
Baadhi ya Wanafunzi wakiwa wanamwelekezea askari  Fimbo wakimtaka kuondoka eneo hilo
========================================================================
Polisi nchini Kenya mapema leo imebidi kutumia Mabomu ya machozi kuwatuliza wanafunzi waliokuwa wakiandamana kupinga kuchukuliwa kwa eneo lao la michezo kutokana na mtu mmoja ambaye alionekana kulichukua na kuweka uzio kitendo kilichosababisha mtafaruku mkubwa baina ya wanafunzi hao na Polisi.

hata hivyo wanafunzi hao ambao inasadikiwa kwamba walikuwa na umri kati ya miaka sita walifanikiwa kuuvunja uzio uliokuwa umewekwa kutenganisha shule yao na eneo hilo la viwanja vya michezo.

wanafunzi hao walikuwa walikuwa wamerejea kutoka majumbani baada ya likizo ya wiki mbili kutokana na mgomo wa walimu wa Umma waliokuwa wameufanya kwa serikali, ambapo kati ya watoto 1000 inasemekana kuwa na umri wa miaka mitatu hadi kumi na nne na ikiwa inamilikiwa na baraza la jiji.

Sunday, January 18, 2015

WAZIRI DR. FENELLA MUKANGARA AKUTANA NA JUKWAA LA WAHARIRI

unnamedWaziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara akiwaeleza wahariri wa vyombo vya habari nchini wajibu na umuhimu wa vyombo vya habari katika mchakato huu wa upatikani wa katiba mpya ikiwemo kutoa elimu kuhusu umuhimu wa mchakato huu kwa mustakabali wa Taifa pia alivipongeza vyombo vya habari katika elimishaji wa wananchi katika mchakato wa Bunge Maalum la Katiba, Wakati wa Mkutano na Wahariri wa Vyombo vya Habari jana Jijini Dar es Salaam.
unnamed1Mwenyekiti wa Jukwaa la wahariri Absalom Kibanda akiongea wakati wa mkutano uliowakutanisha wahariri wa vyombo na Waziri wa Habari, Vijana, Utamduni na Michezo ambapo Dkt. Fenela Mukangara ambapo waliwataka wahariri kuwa wamoja katika masuala ya kitaifa hasa yatakayopelekea kuibomoa nchi yetu pia aliwaasa wahariri kutumia kalamu zao vizuri kuwaelimisha wananchi katika mchakato huu wa kuelekea upatikaji wa Katiba Mpya kushoto kwake ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari Bw. Assah Mwambene, Naibu Waziri Wizara ya Katiba na Sheria Mh.Angela Kairuki na Mwisho ni Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara jana Jijini Dar es Salaam.
unnamed3Mzee Kingunge Ngombale-Mwiru akiongea na wahariri wa vyombo vya habari ambapo ambapo aliwaeleza kuhusu umuhimu wa upatikanaji wa katiba mpya kwa maendeleo ya Taifa ikiwa katiba iliyopendekezwa imezingatia Masuala muhimu ya ukuzaji uchumi wan chi pia uzingatiaji wa makundi mbalimbali katika jamii na alisisitiza umuhimu wa vyombo vya habari kuendelea kutoa elimu kuelekea upatikanji wa katiba mpya kwani katiba ni chombo cha ukombozi wa nchi.
unnamed4Mwenyekiti wa Jukwaa la wahariri Absalom Kibanda akisamiana na Mzee Kingunge Ngombale-Mwiru wakati wa mkutano wa wahariri wa vyombo vya Habari na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara.
unnamed5Mh. Hamadi Rashid Muhamed akiwaeleza wahariri wa vyombo vya habari ambapo alieleza furaha yake kwa katiba inayopendekezwa kujikita katika kutatua changamoto za muungano zitakazopekea kuimarika kwa muungano wa Tanzania bara na Zanzibar.
unnamed6Baadhi wa Wahariri wa Vyombo vya Habari nchini Wakifuatilia Mada zilizokuwa zinawasilishwa katika mkutano huo

BENKI YA KIARABU YA MAENDELEO YA UCHUMI YA AFRIKA ( BADEA)YATOA DOLA ZA KIMAREKANI MILIONI 12.0 WILAYA ZA SAME NA MWANGA

DSCI0191Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa serikali Dr. Servacius Likwelile akiwa na ujumbe kutoka Tanzania wakiwa tayari kutiliana saini mkataba wa makubaliano ya mradi wa maji katika Wilaya ya Same na Mwanga. Aliye kushoto kwake ni Eng. Yousef I. Al-Bassam ambaye ni Makamu wa Mwenyekiti na Mkurugenzi Msimamizi wa mfuko wa maendeleo wa Saudia.Fedha hizo zimetoka BADEA.
DSCI0199Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa Serikali Dr.    Servacius Likwelile akitia saini makubaliano ya mradi wa maji katika Wilaya ya Same na Mwanga. Aliye kushoto kwake ni Eng. Yousef I. Al-Bassam ambaye ni Makamu wa Mwenyekiti na Mkurugenzi Msimamizi wa mfuko wa maendeleo wa Saudia. Aliyeko kulia ni Bi. Suzan Mkapa, Mkurugenzi wa sheria kutoka Wizara ya Fedha.
DSCI0203Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa Serikali Dr.   Servacius Likwelile na Eng. Yousef I. Al-Bassam ambaye ni Makamu wa Mwenyekiti na Mkurugenzi Msimamizi wa mfuko wa maendeleo wa Saudia, wakibadilishana mikataba hiyo baada ya kutiliana saini.
DSCI0204Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa Serikali Dr.   Servacius Likwelile na Eng. Yousef I. Al-Bassam ambaye ni Makamu wa Mwenyekiti na Mkurugenzi Msimamizi wa mfuko wa maendeleo wa Saudia, wakiionyesha mikataba hiyo kwa waliohudhuria sherehe hiyo baada ya kutiliana saini.
DSCI0206Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa Serikali Dr. Servacius Likwelile na Eng. Yousef I. Al-Bassam ambaye ni Makamu wa Mwenyekiti na Mkurugenzi Msimamizi wa mfuko wa maendeleo wa Saudia, wakicheka na kugonga kwa furaha baada ya kukamilisha shughuli ya kusainiana mkataba wa kuweka mradi wa maji wilayani Same na Mwanga
Picha zote na Ingiahedi Mduma-Wizara ya Fedha tukiwa Washington DC.
……………………………………………………………………………
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa serikali Dr. Servacius Likwelile, mchana wa leo ametiliana saini makubaliano ya mkataba wa kuanzisha Mradi wa Maji katika Wilaya ya Same na Mwanga. Dr. Likwelile alisaini Mkataba huo kwa niaba ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Benki ya Kiarabu ya Maendeleo ya uchumi ya Afrika . Aliye wakilisha Benki hiyo ni Eng. Yousef I. Al-Bassam ambaye ni Makamu wa Mwenyekiti na Mkurugenzi Msimamizi wa mfuko wa maendeleo wa Saudia. Aidha katika kutiliana saini Mkataba huo Dr. Likwelile alimueleza Eng. Yousef I. Al-Bassam kuwa Serikali ya Tanzania inatambua kuwa BADEA imetoa Dola za Kimarekani milioni 12.0 sawa na shilingi Bilioni 20.1 za Kitanzania kwa ajili ya kusaidia mradi wa maji katika Wilaya ya Same na Mwanga. Hivyo inatoa shukrani zake za dhati kwa BADEA kwa kusaidia kuchochea maendeleo ya Tanzania. “Msaada huu tulioupata leo utaisaidia Serikali kutatua tatizo la maji katika wilaya ya Same na Mwanga, hii inaonyesha ni jinsi BADEA unaunga mkono na kutekeleza jukumu zima la kushiriki katika masuala ya kijamii na ya kiuchumi kwa nchi yetu ya Tanzania, hivyo tunaomba muendelee kutusaidia”. Alisema Dr. Likwelile. Dr. Likwelile alimueleza Eng. Yousef I. Al-Bassam kuwa, kama anavyofahamu gharama za mapendekezo ya mradi mzima ni Dola za Kimarekani million 110.43 na hii inahitaji uchangiaji kutoka katika mifuko mingine kama mfuko wa maendeleo wa Saudia , Mfuko wa Kimataifa wa OPEC na Serikali kuchangia fedha kusaidia mradi huu. Kwa hili sina wasiwasi nalo kwani ninafuraha kujua kwamba umeshakubaliana na ninaujasiri kuwa jitihada zako zitafanikiwa. “Mradi huu wa maji wq wilaya ya Same na Mwanga unalenga kusaidia kuwepo kwa maji kwenye jamii mbalimbali zilizopo kwenye mradi huo.” Aliongeza Dr.Likwelile. Aliendelea kusema kuwa,mradi huo utakapo kamilika : (i) utaongeza kiwango cha watu wengi kuweza kupata maji safi na salama ya kunywa. (ii) Uchumi wa Same na Mwanga utaimarika pamoja na hali ya afya kwa jamii nayo itakuwa imara hasa kwa maeneo yale yanayoguswa na mradi. (iii) Hali ya maisha ya watu wa Same na Mwanga itainuka. “Mafanikio ya ukamilishaji wa mradi huu ni muhimu sana kwa uchumi wa jamii na maisha bora kwa watu wa wilaya ya Same na Mwanga”. Alisema Likwelile. Dr. Likwelilie alimalizia kwa kusema kuwa“Tanzania na Saudia ni marafiki wa muda mrefu sana, hivyo tutazidi kushirikiana na kuhakikisha kila kitu kinaenda sawa”. Hali ya hewa ya mjini Washington Dc. ni mvua za vipindi na baridi kiasi. Imetolewa na: Ingiahedi Mduma Msemaji – Wizara ya Fedha Washington D.C 11/10/2014