TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Tuesday, January 10, 2012

MAANDALIZI MASHUJAA MUSICA SIKU YA IJUMAA YAPAMBA MOTO

 Rais wa Bendi ya Mashujaa Muzika, Kajo Litungu,
 Kutoka kulia ni wacheza shoo wa Mashujaa Musica, Jack Spoila, Baby White, Salma Mwiba, Salma Teketeke, Suzy Mashujaa, na Aisha Twiga, wakati wa maandalizi na mpambano wa siku ya Ijumaa dhidi ya maasimu wao wakuu Mapacha watatu na Extra Bongo, katika Ukumbi wa Bussiness, Barabara ya Mwenge Victoria.
 Baadhi ya wanamuziki wa Mashujaa Musica
 Rais wa Bendi ya Mashujaa Musica, Kajo Litunguru(kushoto) akiongoza wenzake Jado Fid(Jembe) kulia, Pasia Budansi Black Bell wa pili kulia na Raja Radha, wakati wa mazoezi leo
 Wacheza Shoo wa Mawashujaa Musica, Juma Nyamwela(kushoto),Mpasi M-Pesa, na Kelvini Sayona Kill kuu
 Mcheza shoo wa Mashujaa Musica, Salma Teketeke(Mjukuu wa Babu)
 Wapiga Ngoma wa Mashujaa Musica, Sele Kadanse(kulia) na Dulla Ngoma
 Mpiga Kinanda wa Mashujaa Musica, Fredy Manzaka(Picha Zote na Shaaban Mpalule)

-WANAMUZIKI WAKESHA MAZOEZI KUJINDA DHIDI YA WAPINZANI WAO MAPACHA WATATU/EXRABONGO.

-JADO FID (JEMBE), ASEMA LENGO  LIMETIMIA

Aliyekuwa Rais wa Bendi ya Mashujaa Musica ,Jado Fid(Jembe)aliyejiudhuru wadhifa huo wa Madaraka baada ya kumalizika mwaka 2011, amesema kwamba, ameamua kupisha nafasi hiyo ili kuweza kutoa changamoto kwa wanamuziki wengine kupata uzoefu katika idara ya Uongozi kwenye Muziki.
Jado ambaye amekuwa Raisi wa Bendi hiyo tangu alipovuliwa Urais, Eliston Angai, mwaka juzi, ni kati ya wanamuziki wanaotakiwa kuigwa kutokana na Moyo wake wa Ujasiri na Utekelezaji wa Maadili ya Uongozi kwa wanamuziki, baada ya kuitoa katika hali ngumu na yenye misukosuko mingi bendi hiyo hadi alipoamua kustaafu ngazi ya juu ya Uongozi katika bendi hiyo.
"kwa ujuma nimeamua kuwapisha wengine pia ili kuwepo na mabadiliko kimziki, maana uongozi ni sawa na jalala la takataka, watu wengine wakisikia mtu ni kiongozi bila shaka wanadhani kwamba yupo katika hali ya furaha, amani, na hata kuwa mkamilifu kwa kila jambo, kiukweli uongozi ni mzigo, tena unapoona mtu kakaa kwa kipindi kirefu katika kuongoza anatakiwa kuhesimiwa sana, maana hakuna kazi ngumu kama kuongoza binadamu, tena watu wazima, hakika baada ya kusimamishwa Alistoni kwa wakati huo na kisha kubebeshwa nafasi kama ile, ilibidi nifanye kazi ya ziada, ukizingatia ndo tulikuwa katika kutengeneza nyimbo na Albamu za Bendi, so kiukweli namshukuru Mungu, aliweza kuniongoza vizuri hata kuweza kuelewana na kila mmoja wetu wakati wote wa Uongozi wangu, alisema Jado
Ukumbuke kwamba kati ya Nyimbo zinazovuma kwenye kundi la Mashujaa ni ule wa Safari ya Vikwazo, ambao ndiyo unabeba Ujumbe katika Albamu hiyo, Mtunzi ni Jado Fid, ambaye kwa sasa Mashabiki wamempachika jina la JEMBE au Mkapa, na kwa sasa akiendelea kutesa na nyimbo katika baadhi ya Vituo vya Radio na TV, Ukumu ya Mnafiki.
Siku ya Ijumaa katika Ukumbi wa Business uliopo eneo la Victoria, kutawashwa moto kutokana na Bendi tatu kubwa kuwasha moto ndani ya jukwaa moja, yaani MASHUJAA MUSICA, EXTRABONGO,na MAPACHA WATATU.
AKIZUNGUMZIA onyesho hilo, Rais Mteule wa Bendi hiyo, Kajo Litungu, alisema maandalizi yanakwenda vizuri ambapo wanategemea kuwasha moto mkubwa kwa lengo la kuwapa raha mashabiki wao kutoka maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam.
kundi hilo linaundwa na wacheza shoo, Jack Spoila, Baby White, Salma Mwiba, Suzy Joshua, Aisha Twiga, Juma Nyamwela, Mpasi M-Pesa, Kelvini Sayona Kill kuu, Sweety Baby, wapiga vyombo, Fredy Manzaka(Kinanda), Sele Kadanse(Ngoma), Dulla Ngoma, Amosi Nabii Sollo, Profa Kariakoo(Sollo)Baba Isaya Sharobaro(Risimu), Tonton Drama, Kamode Besi na Kassimu Bezi
Waimbaji wanaowakilisha kundi hilo nji pamoja na Jado Fid(Jembe), Kajo Litungu Dasia, Pasia Budansi Black Bell, Raja Radha, Jimmy Adori, Masudi Namba ya Mwisho, Salasini na Tatu, na upande wa Malapa ni pamoja na Ibrahimu Milinda Nyeusi, Yaniki Noha(Sauti ya Radi), na  Zidane Taarifa ya Habari.
chini ya Uongozi wao Makini ukiongozwa na Meneja Hamisi Promota, pamoja na jopo la kamati ya Ufundi, Makala Mbage (Mwanashinyanga)Prince Twalib,Yohana Malasusa na  Mamaaa Sakina,
Kiingilio katika Onyesho hilo kwa mujibu wa Kajo itakuwa shilingi Elfu saba 7,000/= mlangoni.

No comments:

Post a Comment